Ukiwa safarini kutokea jijini Dar na kuelekea mikoani,basi ni lazima humo barabarani utawaona vijana hawa ambao wanafanya biashara ya kuuza mayai ya kienyeji wakiwa wamesimama pembezoni mwa barabara huku wakionyesha bidhaa yao hiyo kwa watu wapitao kwenye magari,hali hii ni ya hatari sana kwa vijana hawa kutokana na namna wanavyosimama kwenye barabara hiyo,maana mara nyingi hupenda kujitokeza ghafla barabarani wakitokea sehemu wanazokuwa wamekaa pindi wasikiapo milio ya magari na ikitokea dereva hayuko makini barabarani anaweza hata akamgonga.
Home
Unlabelled
vijana wafanyao biashara ya mayai ya kienyeji katika barabara za mikoani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hao vijana ni noma.Siku moja nilikuwa nadrive kutoka Arusha kwenda Dar niliwakuta mitaa ya MBEWE nadhani, katikatika ya Chalinze na Segera.Nikanunua hayo Mayai..nilipofika Dar kuyafungua mazima yalikuwa manne tu mengine....!!!
ReplyDeleteDavid V
David hayo mengine ungepeleka kwa mganga wa kienyeji, deal.
ReplyDeleteHapana hawa vijana ni matapeli tu wa vijijini, mayai mengi wanayoyauza ni ya kunguru na bundi, na hata wakati mwingine uuza mayai ya nyoka.
ReplyDeletekuleni kuku mayai mboga samaki maziwa...na kujenga nyumba safi pa kulala pawe bora....
ReplyDeletemayi ya nyoka? Duh, kudadeki!
ReplyDelete