Kaimu Rais wa Dominica,Mhe.Dr. Edward I Watty akizungumza na wabunge toka CPA Tawi la Tanzania walipomtembelea katika makazi yake, Mhe. Watty anashikilia kwa muda nafasi ya urais wa Dominica kwa kuwa Rais wa nchi hiyo, Mhe. Liverpool yuko nje ya nchi kikazi, Nafasi ya Rais wa Dominica hushikiliwa na Rais yeyote mwandamizi (senior citizen) na hakuna cheo cha makamu wa Rais, Mtendaji Mkuu wa Serikali ni Waziri Mkuu ambae pia kikatiba ndio Mwenyekiti wa CPA wa Tawi la Nchi hiyo. Tanzania huchagua Mwenyekiti wake waCPA kila mwanzo wa uhai wa Bunge na nafasi hiyo hushikiliwa kwa miaka mitano.
Spika wa Bunge la Dominica na Mwenyekiti wa Dunia wa Chama cha Wabunge Wanawake wa Jumuiya ya Madola,Mhe. Alix Boyd Knights akitoa maelezo ya mfumo wa Bunge la Dominica na mipango yake juu ya Chama cha Wabunge wanawake wa Jumuiya ya Madola kwa wabunge kutoka Tanzania, kutoka kulia ni Mhe. Mussa Azzan Zungu, Mbunge wa Ilala na Mwenyekiti wa CPA Tawi la Tanzania, Mhe. Beatrice Shellukindo, Mbunge wa Kilindi na Makamu Mwenyekiti wa Tawi la Tanzania, Mhe. Lucy Owenya, Mbunge wa Viti Maalum na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Mhe. John Paul Shibuda, Mbunge wa Maswa Magharibi na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji. Wabunge wa Tanzania wako Dominica katika ziara ya tathmini (benchmarking) ambayo hufanyika baina ya matawi wanachama wa CPA duniani.
Wabunge wa Tanzania wakipata maelezo toka kwa Meneja wa Kituo cha Nyaraka na Kumbukumbu za Kabila la Kalinago(mwenye fulana ya njano), Wa kwanza kulia ni Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia masuala ya Wakalinago nchini Dominica, Mhe. Graneau alieongozana na wabunge kutoka Tanzania.
Wabunge wa Tanzania wakiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia Masuala ya Wenyeji wa Asili wa nchi hiyo (Kalinago), Mhe. Graneau (wa tatu kushoto) na Chifu wa Kabila hilo (nne kushoto) walipotembelea makazi rasmi ya Wakalinago, Wa tatu kulia ni Katibu wa Bunge la Dominica, Bi. Vernanda Raymond.Wabunge wa Tanzania wapo katika ziara ya mafunzo na walikuwa wakitembezwa katika maeneo ya asili ya Dominica. Kabila la Kalinago ndio wenyeji wa asili katika maeneo mengi ya Carribbean ikiwemo Barbados, Trinidad, Antigua na St. Lucia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...