Wadau wa habari kutoka nchi 23 zinazoendelea duniani wakiwa katika hifadhi ya taifa ya mlima Tianzi wenye urefu wa meta 1290 katika mji wa Zhangjiajie (inatamkwa njanjajie) huko kusini magharibi ya China. Wadau hawa wa habari wapo nchini China kwa mafunzo ya mwezi mmoja ya uongozi na uendeshaji wa vituo vya Televisheni.
Vibajaji vya angani (cable cars) ambavyo hutumika kusafirisha watalii kuelekea kilele cha mlima huo zikiwa katika foleni kuwahisha watalii. Usafiri wa aina hii ambao hutumia dakika 6 kufika kilele cha mlima umerahisisha huduma kwa watalii wanaopenda kutembelea sehemu mbalimbali za mandhari ya mlima huo.
wadau wa habari kutoka Televisheni ya zanzibar na Ofisi ya Waziri Mkuu
Baadhi ya wageni wakiwa katika usafiri wa treni wakitembelea mandhari ya mlima huo ambao ndipo ilipoandaliwa filamu ya 'Avatar'
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...