Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Akiba kwa Wafanyakazi Serikali (GEPF), Daudi Msangi akipokea cheti cha ushindi kutoka kwa Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudensia Kabaka wakati wa uzinduzi wa wiki ya Hifadhi ya jamii katika viwanja vya Mnazi mmoja,jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akisoma hotuba wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Hifadhi ya Jamii,katika viwanja vya Mnazi mmoja,jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizindua rasmi Wiki ya Wizara kujitangaza na Uzinduzi wa Wiki ya Hifadhi ya Jamii jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Akiba kwa Wafanyakazi Serikali (GEPF), Daudi Msangi akimkaribisha Waziri wa Kazi na Ajira Gaudensia Kabaka alipokuwa akiwasiki kwenye Banda la Mfuko wa Akiba kwa Wafanyakazi Serikali kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akisaini kitabu cha Wageni alipotembelea banda la mfuko wa Akiba kwa Wafanyakazi Serikalini.
Mrisho Mpoto 'Mjomba' akitumbuiza katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Wizara kujitangaza na Uzinduzi wa Wiki ya Hifadhi ya Jamii.
Meneja Masoko wa Mfuko wa Akiba kwa Wafanyakazi Serikalini (GEPF), Aloyce Ntukamazina akitoa maelezo ya jinsi ya kujiunga na mfuko huo kwa wadau waliotembelea banda lao.
Wanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wakiangalia mchoro wa daraja la Kigamboni.Picha na Francis Dande wa Globu ya Jamii.
Wekeni njia za kutosha za watembea kwa miguu na waendesha baiskeli (miguu miwili, mitatu, na bajaj). Itakuwa vema kama mtaomba maoni ya watumiaji barabara.
ReplyDeleteNaungana na mtoa maoni wa kwanza. Pia wekeni parking spaces za dharura, sio gari ikiharibika basi ndio inaziba njia hadi kesho.
ReplyDeleteHuu mradi bado upo kiganjani tu hadi leo????
ReplyDeletewawekeeni sehemu na watu wanaotaka kujiuwa kwa kujitosa
ReplyDeleteTwende mbele turudi nyuma,hilo vazi alilovaa mjomba mpoto linaonekana ni vazi la kike.
ReplyDelete*michuzi weka hii
ILA MPANGO WA DARAJA LA KIGAMBONI UWE WA UKWELI ....USIWE WA ''MANYAU NYAU''...kama ile DART (Dar Rapid Taransport) ...yaani mabasi yaendayo KASI!.
ReplyDeleteMPENI TENDA MCHINA. MWISHO WA YOTE. WENGINE MTAKULA HASARA KAMA RELI YA KATI. (TRC)
ReplyDelete