BAADHI YA WAJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM WAKIWA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA'WHITE HOUSE' KATIKA MAKAO MAKUU YA CCM MJINI DODOMA MUDA MFUPI KABLA YA KUANZA KWA KIKAO CHAO LEO NOVEMBA 22, 2011.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. BADILISHENI RANGI YA "UNIFORM" ZENU KAMA SEHEMU YA KUJIVUA GAMBA..Ah tangu naimba oooh TANU yajenga nchi...1977,mama yangu akiwa amenibeba mabegani ili nimwone Nyerere(R.I.P)alipokuja wilayani kwenu mwaka huo.

    David V

    ReplyDelete
  2. haya jamani karne ya 21 hii ni mikutano,kula marupurupu,wizi hali duni za wananchi ni pale pale.

    ReplyDelete
  3. Kama kweli CCM inataka kuzingatia wosia wa Mwalimu, wanukuu pia aliyosema baada ya huo mwaka 1990, kwa mfano katika kitabu chake cha "Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania," kilichochapishwa mwaka 1993.

    Baada ya huo mwaka 1990, Mwalimu aliendelea kuishutumu CCM, na huo ndio ukweli ambao CCM haisemi. Kuendelea kunukuu maneno ya 1990 tu ni kuchakachua wosia wa Mwalimu. Na kwa vile wa-Tanzania ni wavivu wa kusoma vitabu, inakuwa rahisi kwa CCM kuendelea na huu uchakachuaji. Nchi hii imeshafika pabaya.

    ReplyDelete
  4. Mbona kama vile hawapo serious, mara wengine wana-text sasa how can you concentrate on issues.

    ReplyDelete
  5. Nyerere alikuwa kaisuka vema CCM. Si mchezo. Chama Makini. Lakini magamba yamezidi.

    ReplyDelete
  6. Hapo bwana Mbele sijakuelewa. Unataka kusema Nyerere alibadili maneno ya huo usia uliowekwa ukutani au unawapa CCM changamoto kupitia maneno ya Nyerere kwa karibu na kuangalia contradictions? Nachofahamu mimi kwa kiongozi aliyekuwa opinionated kama Nyerere ni wazi kwamba mambo aliyosema lazima yangepingana hasa kuzingatia muda mrefu aliokuwa kiongozi. Huwezi kuwa consistent kwenye opinion za siasa kwa zaidi ya 30 yrs!

    ReplyDelete
  7. nape anafurahia cheo mpaka kesho wanandika andika tu kwenye facebook maneno ya kijinga tuuu, fanya kazi achana na show. Kweli watanzania wako nyuma sana, Mungu Awafumbue kwahili.

    ReplyDelete
  8. Hapo wamejibrekisha ndio maana na picha zimepigwa. Kikao kikiwa in session hakua vurugu za flash wala beep.

    ReplyDelete
  9. Oooh afadhali kumbe hali poa kabisaaa, maana sie tulio nje ya kikao tulifikiri kwamba kazi ya kutoana gamba ingeua mtu lakini kwa jinsi wajumbe wanavyoonekana MAMBO MSWANO. HONGERENI BASI!

    ReplyDelete
  10. Madu unayenitaja hapa juu, ni kwamba huo mwaka 1990, Mwalimu alikuwa bado na imani kuwa CCM ndio nguzo ya Taifa hili, na ndio maana akawa amesema kuwa bila CCM madhubuti, nchi itayumba.

    Lakini baada ya huo mwaka 1990, kama inavyoonekana katika hiki kitabu cha "Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania," Mwalimu Nyerere aliendelea kuona jinsi uongozi wa CCM ulivyokuwa unazidi kuwa mbovu, kiasi cha kuwa tishio kwa hatima ya Tanzania. Hali hiyo ilimfanya Mwalimu akasema kuwa angetamani pawe na chama cha upinzani chenye nguvu na makini ili kiweze kutawala nchi badala ya CCM. Isipokuwa, kwa mtazamo wake, chama cha aina hiyo kilikuwa bado hakionekani (uk. 66).

    Jambo la kuzingatia ni hiyo kauli ya chama cha upinzani kuingia Ikulu, jambo ambalo Mwalimu Nyerere alilikubali, katika hicho kitabu cha 1993, kwa manufaa ya Taifa.

    CCM hawako tayari kwa suala hili la wapinzani kuingia Ikulu. Wao wamekuwa wakikipiga vita chama chochote ambacho kilikuwa kinajijengea nguvu na umaarufu. Mifano ni CUF na CHADEMA. CCM hawataji kuwa baada ya huo wosia wa 1990, Mwalimu alikubali wazo la chama cha upinzani makini kuingia Ikulu. CCM wanaishia hapo kwenye wosia wa 1990, na ndio uchakachuaji ninaosemea.

    Mwaka jana, nilikuwa Tanzania wakati CCM walipokuwa na mikutano yao ya kitaifa kule Dodoma. Niliwasikia wakiimba wimbo ambamo walisema kuwa wapinzani kuingia Ikulu haiwezekani. Hapo sasa CCM sio tu wachakachuaji, bali wapinzani wa mtazamo wa Mwalimu Nyerere.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...