SHANGWE KUANZIA MÜNCHEN hadi BERLIN HAKUNA KULALA MTU !

LIVE ! Ngoma Africa Band aka FFU ,Jumamosi 3 Dec 2011,MÜNCHEN

Jumamosi 10-12-2011 Berlin, Live Ngoma Africa band

Watanzania wanaoishi nchini Ujerumani wanaanza kusherekea sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara,kwa vishindo na vilivyochanganyika na shangwe zisizo mfano,kuwa siku ya Jumamosi 3 -12-2011 Uzinduzi wa sherehe hizo utaanzia mjini München,katika mtaa wa Siebold Str,11,majira ya saa 10 alhasiri, na usiku bendi maarufu ya muziki wa dansi Ngoma Africa Band wanatarajiwa kutumbuiza katika sherehe hizo za kihistoria.

Huko Mjini Berlin ,ambako ndio makao makuu ya ujerumani,kuanzia siku ya 9.Dec.2011 mji huo utatingishika na sherehe hizo siku ya JUMAMOSI 10 Dec 2011 ndio siku ambayo watanzania na marafiki wa watanzania,wakiwemo wahisani ,watajimwaga uwanjani kusherekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania bara, bendi ya muziki kikosi kazi cha NGOMA AFRICA BAND aka FFU ambacho kinatazamiwa kumwaga burudani ya muziki kitakuwepo uwanjani,katika usiku usiokucha, Ngoma Africa band pia wanatamba na CD mpya ya "Shangwe 50 Uhuru Anniversary",ambayo imeshaanza kutingisha katika vituo mbali mbali vya Redio ndani na nje ya Tanzania,pia inasikika
at 

WATANZANIA WANAOMBWA KUJITOKEZA KWA WINGI ! Kama wahenga wanavyosema
CHEREKO ! CHEREKO ! NA MWENYE MWANA !

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. naona kikosi cha FFU wapo tayari tayari kwa gwaride,kazi ipo si mchezo

    ReplyDelete
  2. ngoma africa band au ffu,leo nimesikia cd yenu ya shangwe za miaka 50 ya uhuru,muziki wenu umetulia shughuli mnaiweza,mbarikiwe huko ughaibuni

    ReplyDelete
  3. HONGERA WATANZANIA HUKO UJERUMANI!!!!!!!::::::;

    Hatua hii tokea tupate Uhuru hadi sasa licha ya changamoto zilizopo, itakuwa ni kipindi chenye manufaa kwetu tukikitumia iwe ni kipimo cha utendaji wetu ili tujipange sawasawa na sio sababu ya kutengana, kukorofishana na kulaumiana!

    Ni vizuri kuuenzi Utaifa na kuitambua thamani ya UHURU WA TANZANIA licha ya mapungufu yanayo zungumzwa na baadhi yetu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...