MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI NA RAIS WA CHUO KIKUU CHA KILIMO NA UFUNDI CHA FLORIDA NCHINI MAREKANI DK.JAMES H. AMMONS WAKITIA SAINI MKATABA WA MASHIRIKIANO KATI YA CHUO KIKUU CHA FLORIDA { FAMU } NA CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR { SUZA }.
MKUFUNZI WA CHUO KIKUU CHA KILIMO NA UFUNDI CHA FLORIDA { FAMU } DR. LEONARD PERRY AKIMUONYESHA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI MOJA YA INJINI ILIYOBUNIWA NA WATAALAMU WA CHUO HICHO.
DR. SUBRAMANIAN RAMAKRISHNAN AKIMTEMBEZA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI KATIKA MOJA YA MAABARA KUU YA CHUO KIKUU CHA KILIMO NA UFUNDI CHA FLORIDA { FAMU }.

Na Othman Khamis Ame - OMPRZ

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetiliana Saini Mkataba wa Mashirikiano kati yake na Chuo Kikuu cha Kilimo na Ufundi cha Florida { FAMUJ } Nchini marekani.

Mkataba huo una lengo la kubadilishana uzoefu na Utaalamu kati ya chuo hicho na chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar { SUZAZ}.

Utiaji saini huo umefanyika katika Majengo ya Chuo hicho cha Florida yaliyopo katika mji wa Tallahassee ambapo kwa upande wa Zanzibar umewakilishwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na ule wa Florida umewakilishwa na Rais wa Chuo hicho cha { FAMU } Dr. James ammons.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyoshuhudiwa pia na wanafunzi wa fani fofauti chuoni hapo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameshauri taaluma inayotolewa na chuo kikuu cha Florida iingie katika nchi changa ili kuleta mabadiliko ya kilimo na ufundi.

Balozi Seif alisema Mataifa mengi yanayoendelea hasa yale ya Bara la Afrika bado yanashindwa kukabiliana na changamoto zinayoyabaliki licha ya kwamba Mataifa hayo yanategemea Kilimo kwa asilimia zaidi ya 70%.

“ Florida University iwe kiungo cha kuunganisha Taaluma katika vyuo vikuu vya nchi changa kikiwemo kile cha suza ”. Alisema Balozi Seif.

Mapema Rais wa Chuo Kikuu cha Kilimo na Ufundi cha Florida

{ famu } Dr.James Ammons alisema Chuo hicho kinalenga kujenga nguvu ya Taaluma katika kuona kizazi cha sasa kinapata Elimu inayokwenda sambamba na mabadiliko ya kasi ya Sayansi na Teknolojia Duniani.

Dr. ammons alisema Chuo hicho kilichoanzishwa miaka 125 iliyopita kimefungua masomo ya Taaluma ya Madawa na Sheria yakianguliwa nay ale ya Kilimo na Ufundi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alipata fursa ya kukitembelea kitengo cha Ufundi cha Chuo hicho cha Florida { FAMU -FSU }.

Mkuu wa Kitengom hicho cha ufundi Dr. Regional Perry alimueleza Balozi Seif na ujumbe wake hatua waliyofikia chuoni hapo ya kifanya utafiti katika masuala ya Madawa na Wanaadamu.

Dr. Perry alisema wataalamu wa chuo hicho tayari wamefikia hatua ya kutengeneza Injini za vyombo vya moto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...