HABARI ILIYOTUFIKIA HIVI PUNDE INAELEZA KUWA,ALIYEKUWA MTANGAZAJI WA ITV/RADIO ONE MIAKA YA NYUMA NA BAADAE KUHAMIA KWENYE SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA UINGEREZA (BBC),BW. JOHN NGAYOMA AMEFARIKI DUNIA MAPEMA LEO ASUBUHI.

HAYATI NGAHYOMA AMBAYE AMEFIKWA NA MAUTI LEO AKIWA HOSPITALI AMBAKO ALIKUWA AKIPATIWA MATIBABU YA MARADHI YALIYOKUWA YAKIMSUMBUA KWA MUDA MREFU AMBAPO ALIENDA MPAKA NCHINI INDIA KWA MATIBABU YA MARADHI YAKE HAYO BILA MAFANIKIO.

MSIBA UPO NYUMBANI KWA MAREHEMU MAENEO YA TABATA SEGEREA NA TARATIBU ZOTE BADO ZINAENDELEA KUFANYIKA.

HIVYO TUTAENDELEA KUPEANA TAARIFA KADRI TUTAKAVYOKUWA TUNAZIPATA.

GLOBU YA JAMII IMEPOKEA KWA MASIKITIKO MAKUBWA SANA TAARIFA HIZI ZA MSIBA WA MPIGANAJI WA SIKU NYINGI KATIKA TASNIA HII YA HABARI,BW. JOHN NGAHYOMA NA INATOA POLE KWA NDUGU WOTE WA MAREHEMU NA TUKO PAMOJA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU CHA MAJONJI.

TUNAMUOMBEA KWA MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI.

AMEIN.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Mjomba kwake ni Tabata Segerea, na sio Mbagala.Ukifika Segerea mwisho unaenda mbele kidogo unaacha mitaa nne kulia kwako wa tano ndio mtaa wake,au ukitokea kinyelezi baada ya njia ya kwenda gerezani mtaa unaofuata kushoto. Au tuseme ni njia amabayo inatumiwa na wakazi wanaoenda kisukulu baada ya njia ya gereza kupigwa marufuku.

    ReplyDelete
  2. Jamanii... RIP John Ngahyoma, alikuwa bosi mzuri sana alipokuwa newsroom ya ITV... Poleni sana wafiwa pamoja na wapiganaji wote

    ReplyDelete
  3. Pumzika kwa amani John, pole kwa familia wanahabari woote na aliowahi kufanya nao kazi. Nimesikitishwa sana ila tukumbuke kuwa kila nafc itaonja mauti, haikwepeki.

    ReplyDelete
  4. Ee Mungu tunusuru tufike hiyo Jumapili

    ReplyDelete
  5. sisi wote niwafiwa ingawa familia inahusika zaidi Mungu ailaze pema roho ya marehemu

    ReplyDelete
  6. RIP John,ulikuwa mcheshi pale tulipokuwa tunafanya kazi ITV,nakumbuka sauti yako ilivyokuwa ukisoma jiji letu na habari za biashara saa za news.mungu aieke roho ya marehemu mahali pema peponi amen.

    ReplyDelete
  7. Jamani mbona mwaka unamalizika vibaya John kweli umekwenda?? so sad

    ReplyDelete
  8. R.I.P John ngayoma mchangia mada hapo unayeomba tufike j'pili be serious hapa si mahali pa matani muda wote grow up

    ReplyDelete
  9. POLENI WAFIWA..TULIMPENDA LKN MUNGU AMEMPENDA ZAIDI. TULIE KWA IMANI.

    ReplyDelete
  10. Pole Winnie kwa kufiwa na baba yako.

    ReplyDelete
  11. Ni huzuni sana. John tunakukumbuka sana na tutaku-miss. Mungu akupumzishe kwa amani, na pia aifariji familia yako na kuwalinda daima.
    Its soo sad, really sad, umetutoka.
    Mchango wako mkubwa katika sekta ya habari kamwe hautasahaulika!!!

    ReplyDelete
  12. Jazba mbaya jamani kumwomba Mungu atufikishe mwaka 2012 kuna utani gani lakini? R.I.P John. ingekuwa ni uchafuzi wa hali ya hewa ankal asingeweka ai kuelewa mambo kazi!!

    ReplyDelete
  13. R.I.P John Ngahyoma. Mwenyenzi Mungu amekupenda zaidi.

    ReplyDelete
  14. Ee MWENYEZI MUNGU WAPOKEE VIUMBE WAKO HALIMA NA NGAHYOMA.

    ReplyDelete
  15. R.I.P uncle John, Cc tulikupenda lakini mungu amekupenda zaidi, Pole sana Faith ni kazi ya mungu, Pole sana DrUpendo na Dr Edmond mungu awatie nguvu na awape moyo wa uvumilivu, tunaelewa kuwa inauma sana lakini tunaamini kungu atawapa roho ya ujasiri na uvumilivu, manzishi ni lini na wapi?

    ReplyDelete
  16. r.i.p Poleni sana wafiwa, poleni sana familia ya akina Ngahyoma

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...