Mkazi huyu wa Mswaha Darajani akipita katika maji baada ya mto Mkomazi kujaaa maji na kisha maji hayo kupita juu ya daraja hilo katika eneo la Kijiji hicho kiasi kusababisha wananchi kushindwa kupita na kuwa kero kwao.
Mkuu wa wilaya ya Korogwe bw. Erasto Sima (kulia) akionyeshana eneo ambalo mtu mmoja Alfred boniface alipoliwa na mamba na kufariki na maiti yake kutopatikana na badala yake ilipatikana Mapafu ambayo familia yake ilimzika.
Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini Mh. John Tendwa (kulia) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mkameni ambako mimea kadhaa ya mazao imechukuliwa na mafuriko hatua ambayo imesababisha wananchi hao wakose chakula, kulia kwake ni mbunge wa jimbo hilo Profesa Majimarefu.
maji yakiwa yamejaa katika barabara na eneo hilo pia kuna mamba hivyo wavukaji wanatakiwa kuchukua taadhali kubwa.

Na Mashaka Mhando,Korogwe

WANANCHI wa kata ya Mkomazi wilayani hapa, wamewaomba wabunge wa jimbo la Korogwe Vijijini Bw. Stephen Ngonyani 'Profesa Majimarefu' na mbunge wa jimbo la Same Mashariki Bi Anna Kilango, kufuatilia suala la ujenzi wa bwawa la Kalimawe ambalo litasaidia kupunguza mafuriko katika vijiji vingi vilivyopo katika wilaya hizo.

Akizungumza juzi wakati Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Bw. Stephen Ngonyani 'Profesa Majimarefu' alipofika kuangalia athari za mafuriko yaliyosababishwa na kujaa kwa mto Mkomazi akiwa pamoja na Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini Bw. John Tendwa, Katibu Kata wa Chama Cha mapinduzi (CCM) wa kata ya Mkomazi Bw. Twalib Ngoto alisema bwawa hilo lililopo Gonja Maore, awali lilijengwa lakini sasa linahitaji kukarabatiwa ili kuzia maji kusambaa eneo kubwa.

"Mheshimiwa mbunge wetu tunakuomba ukutane na mbunge mwenzako wa mama Ana Kilango (Mbunge wa Same mashariki) mkae mzungumze suala la kuiomba serikali ilitengee fedha na kulijenga upya bwawa la Kalimawe ambalo haya mafuriko unayoyaona huku kwetu yanasababishwa na maji kukosa sehemu ambayo yamehifadhiwa ili yasipiti kwa kasi kubwa kama haya," alisema Bw. Ngoto.

Akielezea athari za mafuriko hayo tangu maji hayo yafike kwenye kata hiyo ya Mkomazi, yameweza kuharibu takribani ekari 1,776.34 zilizokuwa na mazao mbalimbali ambayo mengine yalikuwa karibu kuvunwa hatua ambayo sasa imewaacha wananchi wasijue cha kufanya baada ya mashamba yao kujaa maji.

Akizungumza katika mkutano huo Msajili huyo wa vyama vya siasa, aliwataka viongozi wa serikali wa kata hiyo kufanya tathimini ya mafuriko hayo kisha kuhakikisha wanafikisha taarifa hiyo kwa viongozi wa wilaya ili kuangalia uwezekano wa serikali kuweza kusaidia wananchi ambao kimsingi kwa sasa watahitaji misaada ya chakula na mbegu kwa ajili ya msimu ujao wa kilimo.

"Chamsingi Katibu mtendaji wa kata hakikisha mnafanya tathinmini ya mafuriko kujua kiasi kilichoharibika katika mimea na kama kuna nyumba ambazo zimezingirwa na maji mseme maana mnapokuwa na takwimu sahihi mnaisaidia serikali kujua ianzie wapi katika kuwasaidia wananchi," alisema Bw. Tendwa.

Akizungumza katika mkutano huo, Mbunge wa jimbo hilo alisema kuwa mafuriko hayo yamesababisha athari nyingi kaika upande wa mazao ya wananchi ikiwemo baada ya maeneo watu wameliwa na mamba hivyo akawataka wananchi hao kuhakikisha wanachukua taahadhari katika shughuli mbalimbali katika mto huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. jamani ndugu zangu poleni sana. hata hivyo ningependa kumuelewesha muandishi kwamba hili bwawa haliko gonja maore lipo kati ya kkihurio na ndungu. maore kuna mto unaitwa hingilili unaotoka gonja bombo katika msitu wa shengena.tujitahidi kundika vitu kulingana na jiografia ya mahali husika

    ReplyDelete
  2. Wewe maji marefu mwangalie sana huyo tendwa anataka kiti chako cha ubunge ohooo shauri yako

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...