Mlezi wa Hospitali ya CCBR, Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa Hopsitali hiyo mara baada ya kuzindua ujenzi wa Jengo jipya la Hospitali hiyo jana katika Hafla ya Kuadhimisha miaka 10 ya CCBRT.
Mkurugenzi wa wataalam wa Tiba toka CCBRT Ndg. Tom Boures akimweleza Mlezi wa Hospitali hiyo, Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) kuhusu ramani ya majengo mapya yatakayojengwa katika Hospitali hiyo.
Mtumishi wa Hospitali ya CCBRT akimonesha Mlezi wa Hospitali hiyo Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) moja wapo ya ripoti zenye taarifa mbalimbali kuhusu magonjwa ya watu wenye ulemavu nchini ambapo Mhe Spika alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo hapa nchini.
Mlezi wa Hospitali ya CCBR, Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) akifurahi na mmojawapo wa watoto waliofanyiwa upasuaji wa Jicho na kuwekewa jicho bandia na wataalam uwa macho katika Hospitali ya CCBRT.
Dk Luijisyo Mwakalukwa Mtaalam wa maswala ya viungo katika Hospitali ya CCBRT akimonesha Mhe. Spika aliyekuwa mgeni rasmi katika kuadhimisha miaka 10 ya CCBRT mmoja wapo wa watoto waliofanyiwa ukarabati wa viungo. Mtoto huyo amefanyiwa ukarabati wa sura na mkono baada ya kuungua kwa ajali ya moto iliyopelekea kupoteza baadhi ya viungo vyake vya mwili.
Meneja Miradi ya Jamii wa CCBRT Bi. Brenda Msangi akimuonesha Mlezi wa Hospitali ya CCBR, Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) baadhi ya vifaa vya watu wenye ulemavu vinavyotolewa na Hospitali hiyo.
Mlezi wa Hospitali ya CCBR, Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) akimsikiliza kwa makini afisa Ushawishi wa CCBRT Ngd. Fredrick Msigala ambaye ni Mlemavu kuhusu umuhimu wa kuwa na sera kuhusu walemavu mahali pa kazi. Mhe. Spika alikuwa mgeni katika hafala ya kuadhimisha miaka 10 ya CCBRT nchini.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na waanzilishi wa Hospitali ya CCBRT mara baada ya kuwatunukia tuzo ya heshima katika hafla ya kuadhimisha miaka 10 ya Hospitali hiyo hapa nchini. Kutoka kushoto ni Ndg. Erwin Telemans Mkurugenzi Mkuu wa CCBRT, ndg. Eliyuko Mnyone, Mkurugenzi Mkuu wa chama cha wasioona nchini, Ndg. BK Tanna Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi CCBR, Mhe. Dr. Wilbroad Slaa, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi CCBR na Ndg. Geert Vanneste aliyekuwa Mkurugenzi wa CCBRT.Picha na Owen David.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. hiko wapi??? inajengwa wapi??? vp habari nusu nusu....

    ReplyDelete
  2. Mwandumbya unaogopa jina lako mwenyewe? Watanzania mna vituko sana

    ReplyDelete
  3. MIAKA 50 MIAKA 50 UTAFIKIRI HIYO NCHI INAMUUMA KWELI HEHEHEHE VIONGOZI HAWA BWANA WIZI MTUPU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...