Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba,Nestory Timanywa (katikati) akishirikiana na Waziri wa habari Vijana Utamaduni na Michezo,Dk Emmanuel Nchimbi na Paroko wa Parokia ya Kasambya,Christopher Mwoleka wakikata keki katika ibada hiyo maalum.ambayo Waziri Nchimbi ndie alikuwa Mgeni rasmi katika hafla ya Jubilee ya Miaka 75 ya Parokia ya Kasambya Kyaka iliyopo Wilayani Misenyi Mkoani Kagera.
Baba Askofu Mkuu Nestory Timanywa wa Jimbo la Bukoba akipanda mti katika eneo la Parokia ya Kasambya ikiwa ni ishara ya Parokia hiyo kutimiza miaka 75 ya utendaji wake wa kanisa.
Waziri wa habari Vijana Utamaduni na Michezo Dk Emmanuel Nchimbi wa pili kutoka kushoto ambaye alikuwa mgeni rasmi katika jubilee hiyo akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu wa kanisa katoliki jimbo la Bukoba kutoka kulia ni Padri Christopher Mwoleka, Askofu msaidizi jimbo kuu la Bukoba Methodius Kilaini, mfadhili wa Parokia ya Kasambya Dionis Malinzi, Askofu Mkuu Nestory Timanywa wa Jimbo la Bukoba kanisa Katoliki na mwisho kushoto ni Askofu Askofu Arimatius Rweyongeza wa jimbo la Kayanga.
Watoto wa kwaya wakiimba katika ibada hiyo.
Waumini mbalimbali wakiwa katika ibada hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...