Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wafuatao kuwaMabalozi:-

(i) Mhe. Phillip MARMO, ameteuliwa kuwa Balozi nchini CHINA. Kabla ya hapo Mhe. Marmo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge.

(ii) Dkt. Deodorus B. KAMALA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini BELGIUM. Kabla ya hapo Mhe. Kamala alikuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

(iii) Dkt. Batilda S. BURIAN, ameteuliwa kuwa Balozi nchini KENYA. Kabla ya hapo Mhe. Dkt. Burian alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira).

(iv) Dkt. Ladislaus C. KOMBA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini UGANDA. Kabla ya hapo Dkt. Komba alikuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii.

(v) Bibi Shamim NYANDUGA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini MSUMBIJI. Kabla ya hapo Bibi Nyanduga alikuwa Naibu Mkuu wa Itifaki, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

(vi) Bibi Grace J.E. MUJUMA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini ZAMBIA. Kabla ya hapo Bibi Mujuma alikuwa Kaimu Mkurugenzi, Ushirikiano wa Kikanda (Regional Co-operation), Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

(vii) Bwana Mohamed H. HAMZA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini MISRI. Kabla ya hapo Bwana Hamza alikuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, ZANZIBAR, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

(viii) Ndugu Ali A. SALEH, ameteuliwa kuwa Balozi nchini OMAN. Kabla ya hapo Bwana Saleh alikuwa Balozi Mdogo (Consul General) nchini Dubai.

2. Uteuzi huu unaanzia tarehe 12 Oktoba, 2011. Wataapishwa tarehe 19 Desemba, 2011 saa 03.00 Asubuhi.

(Phillemon L. Luhanjo)
KATIBU MKUU KIONGOZI
IKULU,
DAR ES SALAM.
16 Desemba, 2011

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hongereni nyote mulioukwaa ubalozi. Mwenyezi Mungu awape imani muwakilishe nchi kwa usalama.

    ReplyDelete
  2. KWAHIYO CONSUL. WA DUBAI ATAKUWA NANI SASA?...MBONA MMETUPA MSHTUKO WATU WA DUBAI...NADHANI ATAPATIKANA CONSUL GENERAL MZURI KAMA BWANA ALI SALEH...

    ReplyDelete
  3. Hii habari haikukamilika. Hao mabalozi waliokuwepo hizo nchi ni kina nani na sasa wanakwenda wapi? Au hizo nchi hatukuwa na mabalozi?

    ReplyDelete
  4. Mhe Rais Kikwete,
    Hongera na ahsante kwa uteuzi wa mabalozi hawa.

    2.Kwa jitahada na mafanikio ya miaka 50 ya (Uhuru wa Tz Bara na) wizara ya Mambo ya Nje, iko haja ya makusudi kwa Balozi zetu kufanya Retirement na Review ya kila miezi 6 kuainisha kwa uyakinifu vivutio vya kibiashara/uchumi toka Tanzania ambavyo Balozi zimezijengea mazingira katika masoko ya vituo vyao vya kazi nje na vile vile mitaji ya uwekezaji toka ktk vituo vyao kwenda Tanzania ambavyo vitakua na manufaa mapana kwa Uchumi wetu.

    Taarifa hii iwe ya WAZI ili wadau wa maendeleo ya TZ wapate kuchangia ktk kuboresha chelezo ya biashara ya kimataifa hasa wakati huu ambapo mkono wa misaada unateremkia kwenye KUFRU na unashinikiza masharti ya KIKAFIRI huku tunahitaji Biashara Sawia baina ya mataifa.

    3.Dr Kamala D, Ubelgiji ni kituo cha kimkakati sana hasa kwa Uchumi na teknolojia ya usafirishaji wa majini na upakuzi wa bandari. Tafadhali tumia FIKRA YAKO TENDAJI ulisaidie Taifa kutokana na ADHA na DHIHAKA iliyo ya makusudi ktk Upakuzi DUNI wa mizigo Bandari. Taifa bado halijajikomboa na linagugumia hasara kubwa ktk HUDUMA YA BANDARI.

    MAPINDUZI DAIMA.

    MAINA ANG'IELA OWINO.
    UK.

    ReplyDelete
  5. Tunaona baadhi wakipewa pole baada ya kushindwa ubunge na kurudi kwenye baraza la mawaziri,na asante kwa utumishi wa awamu ya kwanza ya jk.Nchi hii inataji fikra tofauti kuiongoza.!

    ReplyDelete
  6. Hongera sana DK. Batilda.

    ReplyDelete
  7. Mheshimiwa Kamala Hongera Sana.

    ReplyDelete
  8. Nakupongeza Kamala. Ubeligiji itabidi niwe nakuletea matoke

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...