Familia ya SAMSON MARUNDA WOISO inatoa shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa, marafiki, majirani na wengine wote waliotufariji, kututia moyo na kuwa nasi kipindi chote cha msiba wa mama yetu mpendwa DOROTHEA EUNICE SAMSON WOISO (pichani).

Marehemu alifariki tarehe 7/10/2011 kwenye Hospitali ya KCMC Moshi, baada ya kuugua kwa muda mfupi na kuzikwa tarehe 11/10/2011, Usseri, Rombo. Misaada yenu na jinsi mlivyoguswa na kuomboleza msiba huo, lilitupa nguvu ya kupokea kifo cha mpendwa wetu.

Ni vigumu kumshukuru kila mtu, tunaomba kwa moyo mkunjufu kila mmoja apokee shukrani zetu za dhati kwa misaada yenu mlioitoa wakati wa kumuuguza marehemu wakati alipokuwa amelazwa KCMC na kipindi chote cha msiba. 

Tungependa kutoa shukrani za pekee kwa madaktari na wauguzi wa KCMC; Jumuiya ya Mtakatifu Martha (Parokia ya Reha);  Muungano wa Jumuiya nne ya Mtakatifu Christogone (Parokia ya Reha); Wafanyakazi wa NMB, Moshi; Wafanyakazi wa Kiliwater Company Limited, Mkuu, Rombo; G32-KNCI JVE Limited; Tarakea Rural Cooperative Society Limited; Kikundi Wazee Wastaafu, Tarakea; Wafanyakazi wa Kilimanjaro Cooperative Bank; Wafanyakazi wa WIOMSA, Zanzibar; Wafanyakazi wa TCMP, Bagamoyo; Wafanyakazi wa Departments of Zoology and Wildlife Conservation na Aquatic Sciences and Fisheries, University of Dar es Salaam; na Wanachama wa Kikundi cha MIBS.
Pia tunawashukuru kwa huduma za kiroho za Mapadre wa Makanisa ya KCMC Hospital na Parokia ya Reha (Rombo) na Wachungaji wa Kanisa la KKKT, Usharika wa Karanga, Moshi Mjini.
Tunawaomba nyote muungane nasi katika kumuombea marehemu apate punziko la milele

MUNGU AMETOA, MUNGU AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...