Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Taifa Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai,katika viwanja vya Ofisi kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar alipohudhuria kikao cha kamati Malum ya Halmashauri Kuu ya CCM.
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,pia Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Amaani Abeid Karume,akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Magharibi Yussuf Mohamed ,alipowasili katika viwanja vya CCM Kisiwandui kuendesha kikao cha kamati maalum ya Halmashauri kuu ya CCM Zanzibar,kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo leo.
Rais Mstaafu wa Tanzania,pia Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi Mzee Ali Hassan Mwinyi,akisalimiana na viongozi wa CCM Ofisi ya chama hicho Kisiwandui Mjini Zanzibar,ambapo jana kilifanyika kikao cha kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Rais na mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi,aliposalimiana na Viongozi wa CCM Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui, alipohudhuria kikao cha kamati Maalum ya Halamashauri kuu ya chama hicho,kilichofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa jengo la Ofisi hiyo Mjini Zanzibar.
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,pia Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Amaani Abeid Karume (katikati) ,akiendesha kikao cha kamati maalum ya Halmashauri kuu ya CCM Zanzibar,kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo,(kushoto) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa,Dk Ali Mohamed Shein,na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai,(kulia).
Baadhi ya wajumbe wa CCM wa Kikao cha kamati maalum ya Halamashauri kuu ya CCM Zanzibar,wakisikiliza mada zilizotolewa katika kikao hicho kilichofanyika jana katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi kuu ya Chama hicho Kisiwandui Mjini Zanzibar.Picha na Ramadhan Othman IKULU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kasi inayokwenda CCM kupoteza majimbo mawili Unguja uchaguzi uliopita, 2015 CUF twaingia Ikulu. Tukaze kamba makomredi!!

    ReplyDelete
  2. Huyo Karume vipi, yeye hana hata jozi moja ya sare za Chama Cha Mapinduzi? Au ndio kwa vile kwa kiasi kikubwa kafanikiwa kukiangamiza huko Zanzibar kwa kukusudia ndio kaamua kuachana nazo kabisa? Fanyeni mumuondoe mbona mmnamchelewesha?

    ReplyDelete
  3. Saleh Ferouz aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu CCM -Taifa ZNZ yuko wapi siku hizi? au ndio ameshatoswa?

    ReplyDelete
  4. Wakati umefika kwa Wadanganyika nasi tuwe na nchi yetu kama ilivyo Zenji wanavyojivunia kuwa na nchi yao. Kama ni kuungana basi iwe ni mashirikiano ya kikanda na siyo kuunganisha nchi. Muungano huu hauwasaidii wananchi ila viongozi walio madarakani wanaoutetea kwa nguvu zao zote ili kudumisha ulaji wao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...