Hii ndio bei mpya ya Mafuta iliyopangwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ambayo imekuwa ikileta kizaa zaa katika vituo vingi vya kuuza mafuta hapa mjini.kwani vituo vingi haviuzi mafuta kwa madai kwamba hakuna.lakini cha ajabu ni kwamba bei ikipanda hata sasa hivi basi vituo vyote vinakuwa na mafuta hata kama ni muda huo huo wametoka kusema hakuna.
Hiki ni Moja ya Vituo vilivyoanza kuuza mafuta jioni ya leo na kupelekea msongamano mkubwa wa magari.
Askari wa Usalama Barabarani nae akiwa kwenye foleni ya kununua mafuta katika Kituo hicho cha BP kilichopo Mtaa wa Kaluta na Indira Gandhi jijini Dar ambacho ndio kilianza kutoa huduma hiyo jioni ya leo.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa jioni ya leo katika kituo hiki cha BP.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...