
Bonanza hilo linalofanyika kila mwaka ifikapo Januari 1, 2012 huandaliwa na Chama cha mchezo wa mazoezi ya Viungo Zanzibar( ZABESA).
Katika maandalizi hayo, leo yaliandaliwa mazozi ya pamoja kwa vilabu vyote vitakavyoshiriki katika Bonanza hilo, ambapo vilabu husika vilipangwa kufanya mazoezi kwa kanda kulingana na maeoneo vilabu vinamofanyia mazoezi.
Bonanza hilo litavishirikisha vilabu zaidi ya 24 vya mazoezi ya viungo Mjini na Vijijini ambavyo kwa kawaida huwa vinafanya mazoezi katika maeneo mbali ya Zanzibar.

Katika wiki ya Bonanza, kwa kushirikiana na Benki ya Damu na Zanzibar Outrech Programme (ZOP) kutakuwa na huduma za kuchangia damu pamoja na kupima afya za wanamazoezi, hasa kupima sukari, presha, macho, koo na masikio na wananchi bila ya malipo.

Mgeni rasmi katika Bonanza hilo atakuwa ni Makamo wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad ambae atayapokea rasmi maandamano ya vilabu hivyo katika uwanja wa Amani na kuwahutubia wana mazoezi na wananchi kwa jumla.

Maandamano ya wanamazoezi yataanza saa 12 kamili asubuhi siku ya Jumamosi ya tarehe 01 Januari 2012, katika bustani ya Michenzani-Muembekisonge kuelekea uwanja wa Amani, kupitia Kijangwani, Mfereji wa wima, Mikunguni na kuishia Uwanja wa Amaan na kutakuwa na matembezi ya mchaka mchaka.
Wito unatolewa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika kushiriki Bonanza ikiwa ni katika kujiunga na matembezi, kushuhudia au kutuo michango mbali mbali itakayofanikisha shughuli hiyo.
FANYA MAZOWEZI, IMARISHA AFYA YAKO
Hongera kwa kuwa ufahamu wa umuhimu wa mazoezi kwa afya. Pia msisahau kuangalia ulaji wenu. Msisahau kupia Mchamba Wima!!
ReplyDelete