Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Mkutano wa 18 wa Hali ya Siasa Tanzania unaofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Ubungo Plaza kuhusu Demokrasi na Mageuzi ya Kijamii Tanzania, leo Desemba 16, ulioandaliwa na Taasisi ya REDET.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima AFP, Said Sud Said, leo Desemba 16 wakati akiagana na wadau waliohudhuria Mkutano wa 18 wa hali ya Siasa Tanzania, unaofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Ubungo Plaza kuhusu Demokrasi na Mageuzi ya Kijamii Tanzania, ulioandaliwa na Taasisi ya REDET.
Baadhi ya wadau waliohudhuria Mkutano wa 18 wa Hali ya Siasa Tanzania, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia mkutano huo ulioanza leo Desemba 16, katika Ukumbi wa Ubungo Plaza kuhusu Demokrasi na Mageuzi ya Kijamii Tanzania, ulioandaliwa na Taasisi ya REDET.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya wadau waliohudhuria Mkutano wa 18 wa Hali ya Saiasa, kuhusu Demokrasi na Mageuzi ya Kijamii Tanzania, ulioandaliwa na Taasisi ya REDET, ulioanza leo Desemba 16, katika Ukumbi wa Ubungo Plaza kuhusu Demokrasi na Mageuzi ya Kijamii Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau waliohudhuria Mkutano wa 18 wa Hali ya Siasa Tanzania.Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Dakta Bilal huyu ni mtaalamu wa Fizikia na Nyuklia sasa ni vipi anawajibika kitaaluma zaidi ya majukumu ya Kiserikali na ki Siasa?
ReplyDeleteAmesoma Harvard University -Marekani moja ya vyuo nguli duniani, ingefaa hata angalau asipopewa majukumu au madarasa ya kufundisha utaalamu huo ,angalau atoe makala au vitabu, kwa vile ni wakati sasa nchi imeingia ktk udau wa nyuklia kwa kuanza uchimbaji wa madini ya Urani.
Umejengeka utamaduni mbaya wa kumtupa jongoo na mti wake kwa Wanataaluma wanapoingia ktk siasa na majukumu ya ki serikali!
Tumemuona Sugu pamoja na Ubunge wake na Siasa ktk uzinduzi wa album yake anti virus amepanda jukwani akamwaga mistari!