Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na Rais Yoweri Museveni wa Uganda huku Katibu Mtendaji wa Kamati ya Kimataifa ya Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) anayemaliza muda wake Balozi Liberata Mulamula akitega sikio katika siku ya pili ya mkutano huo wa viongozi wakuu wa ICGLR wa kupinga unyanyasaji na ukatili wa kijinsia hoteli ya Speke Commonwealth Resort kitongojini Munyonyo, Kampala, leo.
Rais Jakaya Kikwete akimuwekea chaneli ya kupata lugha Rais Mwai Kibaki wa Kenya katika siku ya pili ya mkutano huo wa ICGLR wa kupinga unyanyasaji na ukatili wa kijinsia hoteli ya Speke Commonwealth Resort kitongojini Munyonyo, Kampala, leo.
Rais Jakaya Kikwete akichangia mada katika siku ya pili ya mkutano huo wa ICGLR wa kupinga unyanyasaji na ukatili wa kijinsia hoteli ya Speke Commonwealth Resort kitongojini Munyonyo, Kampala, leo.
Rais Jakaya Kikwete akiongea na Rais Michael Satta wa Zambia na mkewa usiku wa kuamkia leo, muda mchache kabla hawajaelekea Ikulu ya Entebbe ambako Rais Yoweri Museveni aliandaa chakula cha usiku kwakatik wajumbe mkutano huo wa viongozi wa ICGLR wa kupinga unyanyasaji na ukatili wa kijinsia hoteli ya Speke Commonwealth Resort kitongojini Munyonyo, Kampala, leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa ukosefu wa ajira kwa vijana wa Afrika ni jambo kubwa, linalohitaji majawabu makini na ya haraka na hatua kubwa zisizohitaji kucheleweshwa tena kutoka kwa viongozi wa Bara hilo.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa uharaka wa kupata majawabu ya tatizo hilo yanatokana na ukweli kuwa kila nchi ya Afrika inazalisha jeshi kubwa la vijana wasiokuwa na ajira wanaoingia katika soko la ajira kila mwaka baada ya kumaliza shule.

Rais Kikwete ametoa rai hiyo nzito na kubwa kwa viongozi wenzake wa Afrika jioni ya jana, Alhamisi, Desemba 15, 2011, wakati alipokuwa anashiriki katika mjadala kuhusu mada ya Ukatili wa Kijinsia katika nchi za eneo la Maziwa Makuu kwenye siku ya kwanza ya mkutano wa mwaka huu wa wakuu wa nchi wanachama wa eneo hilo.

Mkutano huo wa siku mbili kwenye ukumbi wa Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, nje kidogo ya mji mkuu wa Uganda wa Kampala, unawashirikisha wakuu wa nchi na Serikali pamoja na wawakilishi wa nchi 11 za Umoja wa Nchi za Maziwa Makuu wa International Conference on Great Lakes Region (ICGLR)

Wakati wa mjadala wa mada hiyo, suala la ukosefu wa ajira kwa vijana wa Afrika na athari lake lilijitokeza kutokana na moja ya mapendekezo ya azimio la mada hiyo ya Ukatili wa Kijinsia na ndipo Rais Kikwete alipoingia katika kwenye mjadala huo na kuwaambia wakuu wenzake wa nchi na Serikali:

“Suala hili la ukosefu wa ajira kwa vijana wetu katika Afrika ni suala kubwa sana na linalohitaji majawabu ya haraka na majibu makini kutoka kwetu sote tuliopewa wajibu wa kuongoza nchi zetu. Tunao wajibu wa kutafuta na kupata majawabu sahihi ya tatizo hilo.”

Kuhusu pendekezo kuwa wakubwa wa ICGLR wajadili tatizo hilo katika kikao kijao cha wakuu wa nchi hizo katika miaka miwili ijayo mjini Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), Rais Kikwete amewaambia wakuu wa nchi na Serikali wenzake:

“Suala hili ni suala la haraka. Linahitaji mjadala wa kina na makubaliano makini na majawabu sahihi ya jinsi ya kupambana na jeshi la vijana linaloingia katika soko la ajira kutoka shule na vyuoni kila mwaka. Hatuwezi waheshimiwa viongozi kuendelea kusubiri miaka miwili kujadili suala hili.”

Kufuatilia pandekezo lake, viongozi hao wa ICGLR wamekubaliana kuwaagiza mawaziri wao wanaohusika na ajira na sekta zinazohusiana na ajira kukutana haraka katika muda wa miezi sita ijayo kujadili na kutoa mapendekezo kwa Serikali za nchi wanachama wa ICGLR kuhusu namna gani nchi hizo zinaweza kukabiliana na changamoto hiyo ya ukosefu wa ajira kwa vijana na hata watu wengine.

Marais sita wanawakilishi nchi zao katika mkutano huo wa siku mbili. Mbali na Rais Kikwete, viongozi wengine wanaohudhuria mkutano huo ni Rais Yoweri Museveni, mwenyezi wa mkutano huo na mwenyekiti mpya wa ICGLR, Rais Michael Sata wa Zambia ambaye amemaliza muda wake wa uenyekiti wa Umoja huo, Rais Mwai Kibaki wa Kenya, Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi na Rais Francois Bozize wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).

Nchi nyingine wanachama wa ICGLR zilizowakilishwa na viongozi wengine waandamizi ni pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Jamhuri ya Congo (Brazzaville), Rwanda, Angola na Sudan. Mkutano huo umepangwa kumalizika jioni ya leo.

IMETOLEWA NA:
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Desemba 16, 2011
KAMPALA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Safiiiiii...JK akimfundisha MK jinsi ya kutumia vifaa vya kielektroniki...kwa watani hakuna!!!!

    ReplyDelete
  2. Kibaki looks old and tired! Museveni looks a bit disinterested with that arrogant smile! Kikwete looks enthusiastic...THE EAST AFRICA COMMUNITY HEAVYWEIGHTS. Photo speaks 1000 words3!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...