Mbunge wa Jimbo la Mvomero,Mh. Amos Makalla (wa tatu kulia) akikabidhi bati kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mpapa ikiwa ni sehemu ya msaada alioutoa kwa shule hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero,Mh. Amos Makalla, mwenye suti, akiangalia kupakuliwa kwa mabati kutoka kwenye gari kubwa kwenda ndogo baada ya kukwama njiani wakati likipeteka bati hizo shuleni hapo.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero,Mh. Amos Makalla, akiagalia jengo la nyumba ya mwalimu wa shule ya msingi Mpapa, Wilaya ya Mvomero.
Mwanamke wa Kijiji cha Mpapa , Kata ya Hembeti , Wilaya ya Mvomero, akisaidia kubeba bati , msaada wa Mbunge Amos Makalla , kwa shule ya Mpapa.
Baadhi ya watoto ambao ni wanafunzi wa shule ya Msingi Mpapa, Wilaya ya Mvomero.Picha na John Nditi.
Kamanda MAKALA, HONGERA, naona unaendelea kutafsiri UONGOZI KWA VITENDO.
ReplyDeleteUtawala Bora TZ utafanikiwa sana iwapo Medani ya Kati ya Uongozi itatekeleza majukumu yake kikamilifu, na kwa kuongeza UBUNIFU zaidi ktk Nguvu Kazi.
Taifa linatudai sisi Vijana Mapinduzi na Marekebisho ya Kweli.
MAINA A. OWINO
CCM UK
Mhe. Amos Makalla hizo fedha ulizonunulia mabati umezitoa wapi? Hii dhana ya baadhi ya wabunge kudhani kwamba wanaweza kutatua matatizo ya majimboni mwao, kwa kutoa fedha mifukoni mwao sio sahihi. Wabunge wanapaswa washirikiane na wananchi, serikali na taasisi zingine kuleta maendeleo kwa wananchi na KUSIWE NA DHANA KWAMBA NI MBUNGE AMELIPA KUTOKA MFUKONI MWAKE. Mbunge awe mhamasishaji na mfuatiliaji wa kuleta maendeleo jimboni na si kuleta maendeleo kutokea mfukoni mwake. Mh. Makalla na wabunge wengi wanajitahihidi kutuonyesha sisi wananchi kwamba wanatoa sana misaada kutoka mifukoni mwao kitu ambacho ni makosa, huwezi kuwa mwakilishi wa wananchi kwa kutumia fedha zako za mfukoni. Si haki kwako na si haki kwa wananchi
ReplyDeleteWabunge wanapewa na serikali milioni 5 kila mwezi kwaajili ya maendeleo ya jimbo. Mdau inaeleka hulifahamu hilo?!
ReplyDeleteMdau anony wa Mond Dec 19 09:57=
ReplyDeleteNami nakubali kuwa mbunge sio mtatuzi wa KERO za wananchi kwa kutumia gharama zake mwenyewe toka mfukoni bali ni mwakilishi na mshiriki mhamasishaji.
Lakini kuna DHAMBI gani iwapo Mbunge amehamasika kama mwananchi kwa Ubunifu wake mwenyewe na msaada wa wadau wachache akadunduliza fedha/rasilimali kwa njia mbali mbali akachangia ktk miradi yenye vipaumbele kwa wananchi km Elimu, Afya na Ratibu za kupunguza umaskini?
siku zote tunasikia serikali ina uwezo mdogo na wachangiaji wa misaada wamepevuka kwa KEJELI. Ndio maana CCM iliagiza kuwa Serikali ijenge Usharika, uwezo na mazingira ya Serikali na Asasi binafsi kusukuma gurudumu la maendeleo.
Nawe pia mchangie tu Ndg Amos Makalla aendeleze Mapinduzi ya Maisha Bora kwa wana Mvomero.
MAINA ANG'IELA OWINO.