Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Martin Manyanya (MB) akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi mradi wa umeme unaotumia nishati ya upepo katika Chuo cha Ualimu Rukwa (Rukwa Teachers Collage). Mradi huo wa Umeme umebuniwa na mjasiriamali kutoka Rukwa wa Kampuni ya Ulaya Hydro and Windmill Technology. 
Mradi huu wa umeme utatumika katika chuo hicho cha ualimu kwa shughuli mbalimbali ikiwemo chumba cha kompyuta, mabwenini na madarasani. Mkuu huyo wa Mkoa alifarijika na kutoa ushauri kwa wajasiriamali kuonyesha uwezo wao kwa kubuni miradi mbalimbali ambayo ina manufaa ya moja kwa moja kwa jamii.
Sehemu ya mtambo huo wa kuzalishia umeme. Mtambo huu una uwezo wa kuzalisha umeme wenye kilowatts tatu (3)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. michuzi hapo ni kilowatt au megawatt?

    kilowatt tatu utatosheleza kuendesha chuo?

    ReplyDelete
  2. hongereni ila ingepatikana windmill ya pili kubwa ili iweze kukidhi mahitaji

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...