Hoteli hii iliyopo Mtaa wa Ohio, Dar es Salaam ambayo wakati inafunguliwa ilikuwa inaitwa Sheraton na baadaye kuitwa  Movenpick Royal Palm sasa inaitwa jina lingine la Serena. Picha hii imepigwa leo jijini Dar es Salaam na Kamanda Mwaikenda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 35 mpaka sasa

  1. Mimi nasema kama bado mchezo wa kusamehe kodikwa miaka mitano unaendelea.Serikali wajue wanatengeneza bomu litakalowalipukia siku moja.Kila jambo lina mwanzo na miwsho wake,haiwezekani ni nchi gani ulishenda ukakuta hotel zinabadilishwa majina kama kubadili nguo?
    Nahisi huu ni mchezo mchafu tuuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  2. wizi mtupu

    ReplyDelete
  3. Ka imebadilishwa tena,kweli nchi yetu ni kichwa cha mwendawazimu.

    ReplyDelete
  4. ukwepaji kodi ulikidhiri.

    ReplyDelete
  5. Yaani mimi nimechoka kabisa na haka kamchezo ka kukimbia kodi kiasi hiki. Sasa huyu naye atapewa miaka yake ya kusamehewa, then jina litabadilishwa tena.

    ReplyDelete
  6. WIZI, WEZI, WIZI, WEZI WAKABAJI, WAPORAJI, VIBAKA, VIKWAPURA, VI YOU NAME IT NA SIRI KALI IMEKAA KIMYA KAMA MAMBUMBUMBU VILE.

    SIPIGI KURA YANGU MIE KUPOTEZA WAKATI, KUKAA FOLENI ISIYO NA MPANGO KUPIGWA MABOMU KISA...SERENA HOTEL

    CHUKUENI VYOOOOOTE MPAKA MCHOKE MWISHOWE MTATEMBEA UCHI KAMA GREECE.

    ReplyDelete
  7. mwandishi ueleze vizuri kwamba sheraton , movnpick, na sasa ni serena ni kampuni ambazo zinameneji hoteli, mfano miyhupu anaweza kujenga hotel yake inayoitwa MITHUPU HOTEL(hapa unaandika jina la kampuni inayomaneji hoteli yako ambayo mnatiana mkataba kwa muda gani) hivyo basi mithupu unaweza kuchagua kampuni za kumeneji hotel kama vile kempinski, movenpik, sheraton au accor group, pale unapoona kampuni flani ya management ya hotel haina mvuto unaweza kubadilisah muda wowote kama mkataba ukimalizika, lakini hoteli inakua bado ni yako na sio umeuza ni kwamba umebadilisha maagement tuu, sasa la muhimu ni kueleza ukweli, je ni kweli wanavyobadilisha management, na sio jina la hotel kama watu wanavyodhani, kilimanjaro imebadilisha management ya kempinski na sasa inatumia management ya HYATT, hivyo bado jina lake hilihilo , kilimanjaro hyatt, tuelewe kati ya mmliki kubadilisha managenet ya hitel yake na kuiuza, unaweza kubadilisha management wakati wowote kutokana na group lipi la m]hotel management linapendwa na watalii, katika hospitaliyi industry unafanya chochote kile ambacho customer anataka na sio wewe unachotka kumuuzia customer, hivyo wamiliki huangalia management group ipi inapendwa na wageni wakati huu na inalipia, kutokana na huduma bora wanzotoa. naishia hapa, ila muwe mnaweka mambo sawa, mtazidi kuwafanya watazanai kuwa na mafrasi bure, na watanza kuiasi nchi yao

    ReplyDelete
  8. kAMUA KAMUA WATZ KWEPA KODI KWENDA MBELE! WAGENI KIJUA NDIO HIKI MSISUBIRI WATZ WAAMKE...

    CHUMA CHUMA HARAKA PELEKA KWENU. BADO TZ USINGIZI WA PONO.

    ReplyDelete
  9. Mh, tunaona, tunaogopa na tutazidi kudhulumiwa.

    ReplyDelete
  10. KWANI HIYO HOTEL ILIKUA YA SERIKALI AU MTU BINAFSI KAMA NI BINAFSI NA WAMEAMUA KUIUZA HOTEL YAO KUNA SHIDA GANI?DUNIA YA SASA NI YA USHINDANI WA KIBIASHARA.KIKUBWA NINACHOKIONA HAPO NI KUZINGATIA MIKATABA MIZURI TU YA KULIPA KODO SABABU WAKO KTK ARDHI YA TZ,.....

    ReplyDelete
  11. It has nothing to do with taxation, as a matter of fact, the government made money from this deal..Serena bought out the previous owners and the hotel is fully owned by them now. Movenipick were managing the hotel on behalf of the owners..nafikiria wenyewe walikuwa ni wahindi..hao ndio wameuza hoteli..The owner of Kilimanjaro is Mr Ally Bawardi..amewatumia Kempinski hapo Dar kumanage hotel yake, sasa kama alivyoandika huyo juu, nii sahihi..Management company ya sasa ni Hyyatt..Watu wengine msiandike kitu Kama hujui..kazi mnalaumu Serikali kumbe hamjui kitu..Ulizeni kwanza, au njooni Zanzibar tuwafundishe...maana huku maswala kama hayo, hata mawaiters watawapa darasa..

    ReplyDelete
  12. Nilielewesheni wandugu, hii ina maana gani? Mbona hii hotel imekuwa ikibadilishwa jina kila kukicha?

    ReplyDelete
  13. Ilianza SHERATON Hotel, ikafuatia ROYAL PALM Hotel, halafu MOVENPICK ROYAL PALM Hotel na sasa DAR ES SALAAM SERENA. Hii ni mara ya 4 kwa hii hotel kubadili jina/ management.

    ReplyDelete
  14. Upumbavu huu hadi lini?...Biashara kubwa kama hizi kupata uwezekano wa kukwepa kodi!!!...sasa hivi kodi ya VAT ni kama kiama kwa biashara za kawaida kwanza mashine yake ''unauziwa'' na ni ghali sana sio chini ya US$ 1,000 kwa mashine moja!, huku nchi zingine ukisajili kuwa mlipaji au mkusanyaji wa kodi ya serikali unapewa uwezekano wa hilo kwa kila kitu bure, kama ni mashine na facility zingine zinajilipa kadri unavyokusanya kodi!

    ReplyDelete
  15. jamani watz ni wagumu kuelewa nani kawaambia kubadili jina ni kukwepa kodi madau hapo juu amejaribu kufafanua kirefu na kwa ufasaha kuwa kuwa kubadili jina ni kubadili management lkn kwa hili la serena ya sasa ni kwamba si management tu ni kuwa hoteli hii imeuzwa kwa asilimia 100% kwa mmiliki wa hotel ya Serena ambaye ni HH Aga Khan hivyo hotel hii itabaki kuwa serena for good labda na yeye aamue kuiza na si kubadili uognozi kama ilivyozoeleka.

    ReplyDelete
  16. yani hii nchi basi tena mambo gani haya jaman, tumekaa tuu viongozi nyie mnafanya nini hawa watu kila siku wanakwepa kodi,nchi hii ufisadi mtupuuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  17. Da! Tunaiba tunapora na tunazidi kuwa masikini

    ReplyDelete
  18. mzee mantiakis huyo na longo longo lake..mgirki huyo hapendi kulipa kodi kabisa kama walivyo wagirki wenzake huko kwao ugiriki na ndio maana nchi yao ya ugirki inaflilsika sasa tunaye bongo na amekuwa anaendeleza utapeli wake kwa muda mrefu sanaaa..mfichueni huyo mmiliki wa hilo jengo kwani tabia yake ya kubadilisha majina ya hii hotel inaendena janja kwa kukwepa kodi, kwa kuaidiwa na maafisa walafu wa serekali na wahasibu na wanasheria wajanja..bongo kichwa cha mwendawazimu, kila mtu anajifunza namna ya kunyoa !! AIBU !!!

    ReplyDelete
  19. Naungana na mdau ya kwamba hapo hakuna WIVI bali ni swala la kuajiri MENEJIMENTI mpya tu ambayo mmiliki ataona inamanufaa kibiashara zaidi ila suala la kodi lipalepale cha msingi serikali isikae kimya budi iwaelimishe raia wake kuhusu mtindo huu hakuna cha kufaidi TAX HOLIDAY kama wadau wanavyo lalama kila kona ni suala la managerial bandungu!!!!.....

    ReplyDelete
  20. HAWAIBI BANA NI SWALA LA UTAWALA TU!

    ReplyDelete
  21. Kweli TZ imeshindikana kwa 10% percent.

    ReplyDelete
  22. Maswali ya kujiuliza, ni kwa nini wabadilishe majina kila mara? na kwa nini tunawapa masamaha wa kodi kila kwa miaka 5? kwa nini watuzidi ujanja?

    ReplyDelete
  23. Sheraton -> Royal Palm -> MovenPick -> Serena >???????Break Point au Simba Kapakatwa

    ReplyDelete
  24. MMILIKI WA HOTEL NI YULEYULE JINA TU LINABADILIKA HILI ASILIPE KODI..NI SAWA SAWA NA KAMA MAKAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI..UBADILISHA MAJINA KILA SIKU..

    ReplyDelete
  25. yale yaleeeeeeeeeeeee, na viongozi wetu wanaojifanya vijana wajanja kumbe mabwege tu, hata akili ya hilo hawalioni! shame on u!

    ReplyDelete
  26. mmiliki sio huyo huyo fanyeni utafiti acheni porojo kulalamika tuuuuuuuuu. Mmiliki wa Hoteli kwa sasa ni Prince Aghakan ambaye ndio mwenye serena hotel hata ile ya arusha.

    ReplyDelete
  27. Baadhi ya Wadau watakataa ubadilishajiwa MANAGEMENT unaashiria uwezekanowa kukwepa kodi!.

    Kimsingi nfano wewe mtu A unaendesha biashara ya genge gharama ,madeni, na ada zote utawajibika nazo kwa kipindi ulichokuwa na umiliki wa genge,,,halafu ukiniuzia genge mimi mtu B je madeni yako, gharama na ada ulizoacha nyuma nitalipa mimi? ...kimsingi mimi nitaanza moja na HUU NDIO UKWEPAJI WENYEWE WA KODI!

    ReplyDelete
  28. watazuguka wee watarudia jina la mwanzo sheraton hotel

    ReplyDelete
  29. ujue jengo kama lile linaingia direct katika icon ya jiji, sasa umapochange jina daily ni ukengeufu wa jiji unapoonekana, leo ktk ramani imeandikwa kona ya royal palm kesho mov,pick juzi sheraton leo serena kesho hilton au Samaki samaki,, ni kufanyana wajinga, kama mtu akipewa apewe na masharti hakuna kuchange jina laa jiji litoe jina lake liwe la kudumu, kama biashara inalipa inalipa tu! mbona zikina Sea cliff zipo tu nayo tena ingeitwa Sanaa Hotel ( nshawapatia jina hapo)

    ReplyDelete
  30. WAUNGWANA NYAMAZENI WANACHADEMA TANGU LINI WAKAELEWA KILA SAAAA LAWAMA SERIKALI YATAWASHINDA.

    HUYO JICHO UPANDE WENU ANAE

    ReplyDelete
  31. mmm mi napita tu hapa naenda chooni nikirudi ntacomment

    ReplyDelete
  32. Ni nafuu serene wamechukua wenyewe wananunua 100%. wanazo hotel nyingi east africa. kwa tanzania hiyo itakuwa ya sita au saba. hawana mambo ya kukwepa kodi

    ReplyDelete
  33. Poleni wandugu. Dunia ndivyo iliyo.

    ReplyDelete
  34. Tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbeleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.

    ReplyDelete
  35. Mimi nina swali moja tu je huu ubarishwaji wa jina/management wasemaji mliosema kwamba hamna ukwepaji wa kodi mna uhakika?????????? Siyo issue za Taxholiday ndo zinakwepwa???? au tufanye uchunguzi ili tuweze kubaini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...