Meneja wa Huduma kwa Wateja na Uhusiano wa Bohari ya Madawa (MSD), Salome Mallamia (kushoto) akimkabidhi Ofisa Muuguzi wa Zamu wa Hospitali ya Temeke, msaada wa aina 107 za dawa zilizotolewa na bohari hiyo chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa ajli ya wagonjwa mbalimbali wanaohudumiwa na hospitali hiyo. Dawa hizo zilizotolewa hospitalini hapo , ni zile zilizobaki baada ya kuwahudumia wagonjwa kwenye Kijiji cha Wizara hiyo wakati wa Maonesho ya miaka 50 ya Uhuru, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam. Katikati ni Ofisa Huduma kwa Wateja wa MSD Dodoma, Lucas Chagula.
Mwandishi wa Habari, Mwandamizi wa gazeti la Jambo Leo, Grace Michael, akisalimiana na Ofisa Muuguzi wa Zamu wa Hospitali ya Temeke, Rolester Kinunda.
Moja ya makasha ya dawa hizo.
Salome wa MSD, akisoma risala kuhusu msaada huo.
Makasha ya dawa hizo yakishushwa kwenye gari yakipelekwa Store ya hospitali hiyo.
famasi za mitaani zitajaa dawa sasa!
ReplyDelete