Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar, limefanikiwa kuzima jaribio kubwa la ujambazi lilokuwa lifanyike mara baada ya kuchukuliwa kwa mishahara ya watumishi wa hoteli moja ya Kitalii.
Afisa Habari wa Jeshi hilo Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema kuwa jaribio hilo limezimwa na Polisi jana Alhamisi Desemba 29, 2011 majira ya saa 7.00 mchana baada ya makachero wa Jeshi la Polisi kupata taarifa mapema na kuweka mtego uliowanasa majambazi watatu kati ya sita.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar ACP Aziz Juma Mohammed, amesema kuwa majambazi wapatao sita wakiwa na silaha aina ya SMG walijipanga kumteka mhasibu wa Hoteli ya Kitalii ya Blue Bay iliopo Kiwengwa huko Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Kamanda Aziz amesema majambazi huo walipanga kufanyika uporaji huo mara baada ya kuchukuliwa kwa mishahara hiyo ya watumishi wa Hoteli ya Blue Bay na tukio hilo lingefanyika njiani wakati mhasibu huyo akitokea katika Tawi la Benki ya Barclays lililopo eneo la Kinazini Mjini Zanzibar na Hoteli ya Blue Bay ya Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amesema majambazi hayo yalifika eneo la tukio wengine wakiwa kwenye gari dogo na wengine wakiwa kwenye pikipiki za kukodi mbili za kukodi vyombo ambavyo viliegeshwa pembeni mwa barabara inayoelekea Bububu wakimsubiri Muhasibu wa Hoteli ya Blue Bay atoke Benki ili wampore fedha hizo ambazo zilikuwa za kigeni.
Hata hivyo Kamanda Aziz amesema kuwa katika tukio hilo ulifanyika ukamataji salama ambao haukuhusisha matumizi ya silaha na hivyo kunusuru maisha ya majambazi kwa upande mmoja lakini pia na kwa Polisi.
Kamanda Aziz amesema Polisi wamefanikiwa kuzima tukio hilo baada ya kuwa na taarifa za kutosha kutoka kwa wasiri wake ambao ni wananchi.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi, kwa kupitia falsafa ya Polisi Jamii, walipatie taarifa sahihi zitakazowezesha kukamatwa watuhumiwa waliotoroka na
kuwataka watu wote wanaokwenda Benki kwa dhamira ya kuweka au kuchukuwa fedha nyingi wawe wasiri na kutoa taarifa Polisi ili wapatiwe usindikizaji salama wa fedha zao.
mi nahisi mnalipwa kwa hilo na hamstahili pongezi kwani ni wajibu wenu. hamna haja ya kujitangaza, mnatafuta approval? kwa nini? kwa kuwa mnajuwa hamfanyi kazi ipasavyo na rushwa ndo suna yenu.
ReplyDeleteMambo ya kulipana mishahara dirishani ishapitwa na wakati, watu siku hizi wanalipwa kupitia akaunti zao!
ReplyDeleteIsiwe Ohhh Ujambazi Zanzibar unafanywa na (Machogo) yaani watu wa Bara.
ReplyDeleteKumbe vitu kama Umalaya, Wizi,Uhalifu na mengine havina mwenyewe!
Pana makundi ya Wapemba huku Dar au Bara wana aina mpya ya wizi, wanatumia magari wanapaki kwa kubanana ktk maegesho huku majirani wakiwa hawapo wanashusha vioo wanavunja madirisha ya magari ya jirani wanaiba vitu vya ndani halafu wanaondoka.
Unaweza kumuona mtu akawa anaonekana kama mtu wa Dini au Kiongozi wa Dini kumbe kwa siri ni Mhalifu!
Kamanda habari yako imetushibisha kabisa na huku bara pia waige mfano wa jinsi ya kutoa taarifa kama hizo, huku bara wangeficha jina la hoteli, bank, na huyo cashier ati watapoteza ushahidi kwani upelelezi bado.yanini sasa kutoa habari inayo kuwacha hewani.
ReplyDeleteTaharifa hii imekamilika na huna dukuduku la maswali mengi. bravo kamanda.
UTEKELEZAJI WA PILISI JAMII:
ReplyDeleteImekaa vizuri kwa kutoa taarifa zote kukamilika ktk tukio hilo la ujambazi kama jina na Benki,jina la Hoteli na Maeneo husika.
Kwa msaada wa kuwaia mbaroni hao walitoroka ingefaa picha na majina yao vianikwe ili kusaidia kuwasaka!
Namuunga mkono anon wa pili,twende na wakati jamani,fungulieni wafanyakazi accounti kama hawana,hata ma house gal wana account,tuache kulipana dirishani
ReplyDelete