mbunge wambeya mjini Josephy Mbilinyi ambaye ni mkuu wamsafara wa Tamasha la Anti virus akiwa anaongea na waandishi wahabari kuhusiana na tamasha hilo ambalo linafanyika december 18 katikaviwanja vya Triple A jijini Arusha

Na Woinde Shizza,Arusha

Wasanii mbalimbali wakiongonzwa na mbunge wa jimbo la Mbeya mjini,Joseph Mbilinyi wanatarajia kufanya Tamasha lijulikanalo kwa jina la Anti virus mapema desemba 18 mwaka huu katika uwanja wa ukumbi wa TripleA uliopo jijini hapa .

Akiongea na waandishi wa habari msemaji mkuu wa kundi hilo, Joseph Mbilinyi alisema kuwa Tamasha hilo linaambatana na uzinduzi wa albamu ya Anti virus ambayo itawashirikisha wasanii mbalimbali wa kizazi kipya wa mjini hapa pamoja na wasanii wengine mbalimbali .

Alisema kuwa nia ya tamasha hilo ni kutangaza matatizo ya wasanii kwani wamelalamika kupitia nyimbo zao lakini wameona haifai ndo maana wakaamua kutangaza matatizo haya kupitia tamasha hilo.

Alisema wanampango wa kutangaza tamasha hilo nchi nzima ili kuweza kuwapa moyo wasanii ambao wapo mikoani lakini bado hawajaweza kusikika.

Alibainisha kuwa anti virus ni muungano wa wasanii ambao wameamua kupambana kwa ajili ya kuwakomboa wasanii wenzao ambao wana vipaji lakini wameshindwa kujiinua pia kundi hili linajihusisha na kurekodi albamu ambazo zinaelezea matatizo ambayo wasanii wanayo na wanakaa na kuweza kujadili nini kifanyike ili waweze kukomboa maisha ya wasanii.

"wote tunajua kuwa katika sekta ambazo zimetelekezwa ni hii ya wasanii hivyo tamasha hili linajitaidi kufanya hivi ili kutafuta watu wa kuwasaidia kwa kupitia vitu hivyo ikiwa ni wanarekodi na pia tunachukuwa wasanii wa kiwango cha chini "Alisema mbilinyi

Alibainisha kuwa katika tamasha hilo wanaahidi kuwa watafanya kitu ambacho hakijawahi kufanyika katika mji wa Arusha na itakuwa ni mara ya kwanza kufanyika.

Aliwataja baadhi ya wasanii ambao watakuwepo ni pamoja na yeye mwenyewe ambaye anaongoza kundi hili la Ant Virus Sugu wengine wakiwa ni MKoloni,Rama dee,Suma G, Coin,Isaya Family, peen Lawyer ,Danny Msimamo pamoja na Mapacha wajanja sapplaya.

Alisema kuwa pia kutakuwa na wasanii wengine ambao hawajashiriki katika albamu hiyo ya Anti virus ambao aliwataja kuwa ni Sister P,mabaga fresh na pia alisema kuwa kwa upande wa wasanii wadogo wametoa nafasi kwa wasanii wa hapa hapa mkoani Arusha ambapo alisema kuwa watakuwepo Mo kweli ,jambo Squid,,pamoja na Bu nokos .

"unajua asilimia tisini na tisa pointi tisa wanatutia moyo na wanatusaidia ila si unajua watu wote hawawezi kuwa manesi ndo maana kuna walimu nadhani jinsi tunavyoenda wataongezeka bwana"alisema Sugu

Alimalizia kuwa tamasha hili ni maalumu kwa ajili ya kupigania wasanii warudi kazini wasikae mitaani tu bila kazi na wajitaidi kufanya kazi maana ukombozi upo.

Alisema kuwa Tamasha hili ni endelevu kwakuwa ni tamasha la mkusanyiko wa wasaniii tofauti tofauti na tamasha hili sio biashara bali mi maendeleo na litaendelea hadi mwisho.

Alitoa wito watu wa Arusha kujitokeza kwa wingi kushiriki katika tamasha hili ili wasanii wao waone kuwa wamejitokeza kuwainua na alibainisha kuwa tiketi zitauzwa kuanzia saa sita mchana na shoo itaanza saa kumi jioni hadi saa sita usiku huku kiingilio kikiwa ni sh. 5,000 na katika masaa hayo kutakuwa na sektioni mbili ambapo wasanii wataimba moja kwa moja kwa mdundo huku lisaa limoja likitumika kwa ajili kuzindua albamu hiyo ya anti virus.

Alisema kuwa hali ya usalama iko vizuri kabisa kwani wanajaribu kuwa aminisha watu kuwa wanaweza pasipo shida

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. more fire VINEGA, you guys deserve kila aina ya pongezi.nawatakia kila la kheri kwenye kumkomboa msanii wa TZ...much love

    ReplyDelete
  2. palipo na haki ushindi ni lazima ANT-VIRUS ni wakili mziki in utetea

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...