Mkuu wa Kikosi cha usalama barabarani mkoani Tanga, Mrakibu wa Polisi (SP) Abdi Isango, akizungumza na waendesha pikipiki maarufu bodaboda na watu wengine, akiwafafanulia jinsi sheria za barabarani zinavyopaswa kufuata hasa kwa waendesha pikipiki ambapo katika msako uliofanyika jana, jumla pikipiki 140 zilikamatwa kutokana na makosa mbalimbali.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali waliofika katika kituo hicho cha polisi cha usalama barabarani eneo la mabawa kupata taarifa za operesheni iliyoendeshwa na kikosi hicho kutoka kushoto ni Oscar Assenga (Mtanzania), Amina Omari (Mtanzania), Suzan Uwinga (Mtanzania) na William Mngazija (ITV na Radi One).
sehemu ya pikipiki zikiwa zimehifadhiwa kwenye eneo maalumu katika kituo cha polisi cha usalama barabarani kilichopo eneo la Mabawa Jijini Tanga baada ya kikosi hicho kuendesha zoezi la kuwakamata watu waliokuwa na makosa ya usalama barabarani yakiwemo kosa la kutokuvaa kofia ngumu 'helments'.
Na Mashaka Mhando,Tanga
WATUMISHI watano wa serikali Mkoani hapa wamepoteza maisha kwa nyakati tofauti katika kipindi cha mwezi mmoja kutokana na ajali za pikipiki zilizosababishwa na mwendo wa kasi usiozingatia sheria za usalama barabarani na uvaaji wa kofia ngumu, (Helment).
Akizungumza na Waandishi wa Habari Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Tanga , Bw. Abdi Issango kufafanua operesheni maalumu ya kuwakamata madereva wa pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda wanaokiuka sheria wawapo kazini, alisema watumishi hao wamekufa kwa ajali za pikipiki.
Bw. Issango ambae tangu ameshika wadhifa huo amekuwa akipambana na madereva wazembe wanaoendesha vyombo vya moto, alisema ajali za pikipiki zimekuwa tishio kwa maisha ya binaadamu na kueleza kuwa kwa kipindi cha mwezi Novemba pekee watumishi watano wa serikali wamepoteza maisha kutokana na ajali hizo.
Aliwataja watumishi hao kuwa ni pamoja na askari polisi aliyemtaja kwa jina la PC Herman , Paul Sakwa aliyekuwa mkuu wa shule ya Dindira Wilayani Korogwe, Shaban Mtoi mwalimu shule ya msingi Korogwe, Chlement Kinyasi aliyekuwa mtendaji Kata Wilaya ya Muheza na Issa Nyonanje aliyekuwa mtumishi wa mamlaka ya maji safi na taka Jiji la Tanga.
Hata hivyo alieleza kuwa ajali zote hizo zilitokana na mwendo kasi wa pikipiki walizokuwa nazo marehemu na kwamba kutokana na hali hiyo jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani limeanza operesheni ya kuwakamata wale wote wanaokiuka sheria za usalama barabarani.
Alisema katika operesheni hiyo iliyoanza mapema wiki hii zaidi ya pikipiki 120 zimekamatwa kwa siku mbili huku waendeshaji wa vyombo hivyo wakikabiliwa na makosa mbalimbali na ambayo wanalazimika kulipa faini ama kwenda jela kwa kujibu wa sheria.
Aliyataja baadhi ya makosa ambayo yamepewa kipaumbele kwa kutazamwa katika zoezi hilo kuwa ni pamoja na wale wasiyo na leseni ya udereva, kutotumia kofia ngumu wanapoendesha pikipiki na hata abiria wanaowapakia, bima na ubora wa chombo chenyewe.
Alitoa wito kwa watumia pikipiki wote mkoa wa Tanga kuzingatia sheria za usalama barabarani kwa kuendesha mwendo wa kawaida, kuwavalisha kofia abilia na wao wenyewe na kwamba kila muendesha pikipiki analazimika kuwa na vielelezo vyote stahiki ili aweze kuvionyesha kwa maafisa wa polisi watakapo vihitaji.
hongera sana jeshi la polisi kwa zoezi hilo kama itawezekana zoezi hilo lije na dar es salaam hapa madereva wengi wa bodaboda hawazingatii sheria, wanaendesha pikipiki zao zaidi kwa kuangalia pesa kuliko maisha ya abiria wanao wabeba.
ReplyDeletekofia ngumu kwa kidhungu inaitwa HELMET, thio helement. Masikini wabongo kiswahili mnadobanga kiingereza manabananga, mwawezani nyie?
ReplyDelete