Mjiofizikia Mwandamizi toka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) akimweleza Waziri Mkuu mstaafu Bw.Edward Lowassa juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na wakala huo.
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa akioneshwa majiko yanayotumia kuni mbadala (biomass fuel liquids) ambazo zinatengenezwa na takataka zenye asili ya mimea ambazo zinapatikana kwa wingi kwenye masoko, viwanda vya mbao, viwanda vya kukamua mafuta, kutengeneza unga n.k.
Waziri Mkuu mstaafu, John Samwel Malecela akipata maelezo katika banda la Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) , Wakala huo una lemgo la kuhakikisha kwamba Serikali inapata mapato stahili kutoka kwenye shughuli za uzalishaji na biashara ya madini nchini kupitia usimamizi na ukaguzi makini wa shughuli za uchimbaji na kuhakikisha kuwa shughuli hizo zinafanyika kwa kuzingatia uhifadhi na utunzaji thabiti wa mazingira katika maeneo ya migodi.
Mtaalamu toka Shirika la Madini la Taifa Bw.Sadiki Lusewa akiwaonyesha watoto “diamond bit” kifaa ambacho kinachimba miamba kwa ajili ya kupata sampuli ya madini ili kujua madini husika yanapatikana katika urefu upi ardhini.
Mtaalamu toka Wizara ya Nishati na Madini Bi Winnie Mrema akimweleza mwananchi kuhusu masuala ya usimamizi wa mazingira, afya na usalama katika migodi ikiwa ni miongoni mwa mambo ambayo yameelezwa kwa kina katika Sera mpya ya madini ya mwaka 2009.
TEMBELEA KOTEE, FANYA YOTE HATA NA CHADEMA UNAO WAFADHILI KUPITIA SABODO ILA URAIS 2015 SAHAU TENA FUTA KABISA AKILINI.
ReplyDeleteCCM NI YA WOTE NA MWL NYERERE TUNGEMSIKILIZA HAKIKA.........
huyu ndie raisi mtarajiwa CCM imemchafua ile mbaya lkn iko siku ukweli utabainika.mmempikia majungu kumchafua mkamengenezea na yule mtoto Mnauye amuadhiri baba wa watu, eti kisa alitaka kuuangusha JK 2010 jamani wakaona wamuundie majungu kumchagua lol wenyewe kwa wenyewe wanakulana nyama.
ReplyDeletewapi mamaa winnie! nawaona wapendwa, nimewamisi saaaana tu. @ Mariam vp mdogo wangu? Chapeni kazi. Mbona Kisuju na Marwa siwaoni jamani?!
ReplyDeleteBy Mdau.