Meneja Uhusiano wa Benki ya Posta Tanzania (TPB),Noves Moses (kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 2 ikiwa ni mchango wa Benki hiyo kuisaidia shule ya msingi Temeke ambayo mbali na kuwa na wanafunzi wa kawaida pia inakitengo cha wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia ( Viziwi). kukabiliana na changamoto zake mbalimbali.Kulia kwake ni meneja wa kitengo cha mikopo benki ya posta Abdallah Mtandika,Mwenyekiti wa kamati ya Shule ya msingi Temeke,Rajab Ndunda na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Temeke Bakir Makele.
Meneja Uhusiano wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Noves Moses (kulia) akikabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 2 kwa Mkuu wa shule ya msingi Temeke,Said Mbolembole (kushoto). Fedha hizo ni kwa ajili ya kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo. Katikati ni mwenyekiti wa kamati ya shule Rajab Ndunda na Meneja wa kitengo cha mikopo benki ya Posta Abdallah Mtandika.
Meneja wa kitengo cha mikopo benki ya Posta Tanzania Abdallah Mtandika akitoa maelezo kuhusu umuhimu wa wadau mbalimbali kuchangia elimu ya watoto wetu kwenye hafla ya kukabidhi msaada wa shilingi milioni 2 kwa shule ya Msingi Temeke.Kulia ni Meneja Uhusiano wa Benki ya Posta Noves Moses na mwenyekiti wa kamati ya shule Rajab Ndunda,kushoto ni mkuu wa shule hiyo Said Mbolembole.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. acheni utani nyinyi, yaani the whole freakin kikao na press for just two million?? get serious guys, hio milioni mbili ndio mmesaidia nini? kuandaa hio hafla na expenses zote zinafikia hio milioni 2, hebu fanyeni vitu kwa kujenga nchi sio mazoea.
    Che

    ReplyDelete
  2. Bank ni ya Posta ambayo inatoa msaada, Hundi inayotolewa ni ya NBC :-) aahahha! kweli mnatukanisha Bank yenu!! Kwanini hundi isingekuwa ya Bank yenu kuendeleza Brand????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...