Rais Jakaya Kikwete akimkaribisha Ikulu Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt Wilbroad Slaa usiku huu pamoja na viongozi wengine wa chama hicho katika muendelezo wa mazungumzo yao na serikali juu ya mchakato wa kuundwa katiba mpya. Viongozi hao wa CHADEMA walitinga Ikulu milango ya saa kumi na mbili unusu za jioni, na wakaendelea na mazungumzo hadi saa tatu  usiku walipogawanyika kila kundi kwa mijadala ya ndani kabla ya kuendelea tena. Mkutano huu umemalizika saa Tano na robo usiku huu huku kila upande ukikubaliana na mwingine kuendelea kutafakari vipengele kadhaa vya kufanyiwa marekebisho ili mchakato utapoanza rasmi kusiwe na malalamiko ya aina yoyote yale 
Rais Jakaya Kikwete akiukaribisha Uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) usiku huu Ikulu jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Dkt. Wilbrod Slaa (kushoto) akifafanua jambo kwa Rais Jakaya Kikwete kuhusu mchakato wa Katiba Mpya ikulu Jijini Dar es Salaam leo.Katikati ni Mwenyekiti wa Chama hicho,Mh. Freeman Mbowe.

Chama Cha National Convention for Construction and Reform-Mageuzi (NCCR-Mageuzi) kimempongeza Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kusimamia suala la Katiba vizuri na kwa umakini mkubwa.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Bwana James Mbatia ametoa pongezi hizo leo jioni alipofika Ikulu, akiongoza ujumbe wa viongozi wenzake sita(6), kuja kujadili suala la Katiba Mpya ya Tanzania.
"Tunakupongeza kwa kusimammia suala la Katiba vizuri, ni suala zito ambalo litatupa uhai vizazi na vizazi vijavyo". Amesema kama utangulizi wa ujio wao Ikulu.
"Upinzani sio uadui, tunahitaji kufanya marekebisho ya Katiba kwa amani na hoja bila kuvuruga amani yetu” Bwana Mbatia amesema na kuongeza kuwa “suala la Katiba linahitaji ushirikiano wa pamoja kwa nia njema, kwani taifa hili ni letu sote" ameeleza.
Akiwakilisha hoja ya NCCR-Mageuzi kwa Rais Kikwete, Mkuu wa Idara ya Sheria wa NCCR-Mageuzi Dkt. Senkondo Mvungi amesema, NCCR - Mageuzi inatambua ukubwa wa jambo hili la wa Tanzania kupata Katiba.
"Ni jambo kubwa sana, wewe ndiyo Rais wa kwanza kutengeneza sheria ya kupata katiba mpya na kuanzisha Mchakato wa kupata Katiba Mpya.
Kikao cha leo cha Rais na viongozi wa NCCR-Mageuzi ni mwendelezo wa jitihada za Rais Kikwete, kusikiliza, kuchukua maoni na mawazo ya wadau mbalimbali kutoka vyama vya siasa, asasi za kijamii na makundi mbalimbali katika kuelekea mchakato wa kupata Katiba Mpya ya Tanzania.


Rais amesema kuwa nchi hii inayo Katiba ambayo imelilea vizuri na kulifikisha Taifa la Tanzania hapa lilipo, lakini pia Taifa linahitaji Katiba inayoendana na wakati na itakayoweza kulilea Taifa hili kwa miaka mingi ijayo.
Mara baada ya kumaliza kikao na viongozi wa NCCR-Mageuzi, Rais Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ikiwa ni mwendelezo wa mazungumzo yao yalioanza mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka 2011, kuhusu Katiba Mpya ya Tanzania.
Katika mazungumzo haya na Vyama vya Siasa Rais amesisitiza kuwa lengo la mazungumzo haya yote ni kuhakikisha kuwa hatimaye Watanzania wote watakiri kuwa Katiba Mpya ni yao wote na hatimaye ifikapo mwaka 2015 nchi iweze kufanya uchaguzi wake na Katiba Mpya.


Kwa picha zaidi BOFYA HAPA



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Nalipenda sana squad la chadema, ni kama timu ya dunia ya ushindi.

    ReplyDelete
  2. Lol mzee mzima kaona isiwe tabu nimeonekana naendekeza na nina kinyongo nisije kupoteza mashabiki bure wacha niende nikajikoshe. Au Yosefine amekwambia safari hii uende nini?

    ReplyDelete
  3. Hii ni demokrasia ya kweli na tushukuru haya mambo yanafanyika kwa amani with smiles on their faces. Nchi nyingi Africa wapinzani hawakutani kihali hii! Mungu tubariki watoto wa Tanzania nina imani tutafika. Vijana na wasomi kina Lissu na wengine kwenye msafara vijana wenzenu tunawasupport it time muafaka kufanya mabadiliko mengi nchini ya kisheria yaendane na wakati.

    ReplyDelete
  4. Washabiki tulikuwa hatuelewi huyu babu bifu mpaka lini. Bora ajikoshe maana tulishaanza kumtoa maanani. Phew!

    ReplyDelete
  5. historia uhukumu watu.MARK MY WORDS, RAISI JAKAYA KIKWETE INGAWA UWA SIMFAGILII.ILA KWENYE HILI LA SIASA NA KATIBA. AMEKUWA MWEREVU NA MJANJA WA KISIASA KWA FAIDA YA TAIFA (IN THE LONG TERM)NA KWA CCM (IN THE SHORT TERM).
    TUNAMBEZA SASA HIVI (NAMI NIMO) ILA NAJUA IN FEW YEARS TIME TUTAMKUMBUKA.
    jIULIZE WANA -CCM VIKONGWE WALIO MADARAKANI WANAFURAHIA AU KURIDHIKIA NA ANACHOKIFANYA JK KWA SASA? NANI ANAPENDA KUACHIA MADARAKA?
    IT IS TRICKY SITUATION FOR JK, DOES HE HAVE TO LEAD FOR THE BENEFIT OF THE NATION OR CCM? NOW IT LOOKS HE HAS MADE UP HIS MIND...AND THE TANZANIA HISTORY IM SURE WILL BE KIND TO HIM...(wabongo tuwe bayana, twajua JK ana mapungufu yake ila kwa hili tumpe heko na tumsapoti...kumbukeni sio viongozi wote wa CCM wanamuuunga mkono kwa hili analotaka kufanya. BIG UP JK! MAKE A REAL CHANGE, AND WE A HOPE IS A GENUINE ONE!

    ReplyDelete
  6. Safi sana Rais..Ndiyo katiba ni suala muhimu hahitaji ushabiki wa Kisiasa.

    David V

    ReplyDelete
  7. CAPTAIN STEPHEN WASIRA YUPO WAPI THIS TIME..TUMEKUMISS SEBULENI KWA KIKWETE..

    ReplyDelete
  8. Fellow Tanzanians......hizi ni siasa za kujenga nchi hatuna sababu za kuhubiri vurugu kama alivofanya mbunge wa Arusha,hapana na hatuwezi kuruhusu hili kama tunaipenda nchi yetu,imefikia wakati sasa tuiweke mbele nchi yetu na ndo anachikifanya JK ktk swala la katiba lazima tumuunge mkono japo wapo wachache wasiopenda Tanzania au hawana upendo wa nchi yao wanakuwa wanafiki!
    Vijana tuwe msitari wa mbele kuweka utaifa mbele zaidi kuliko wanasiasa wanaohubiri vurugu na kutojadili ufumbuzi wa haya yanayotukuta ikiwepo maandalizi ya katiba mpya

    ReplyDelete
  9. AMA KWELI MTU SI MBWA! NAONA DK SILAHA KAONA BORA SASA AANZE KUONGOZWA NA AKILI ALIZOMPA MUNGU BADALA YA ZILE JAZBA NA CHOYO ZA SHETANI! HIZI NI DALILI NJEMA ZINAZOASHIRIA AMANI KWA CHADEMA KUMTAMBUA JK. SASA U MAKE SENSE. NAKUPONGEZENI SANA KWA KUZINDUKA KUTOKA USINGIZI WA UBINAFSI, WIVU NA CHOYO. VICHWA VYENU CHADEMA NAAMINI VIMEANZA KUJAA AKILI KAMILI SIO ZILE ZA KITOTO ZA EGOISM NA VIOLENCE. HATA MAANDAMANO MMEACHA SASA. MMEKUA, MMEANZA KUMLAANI SHETANI, MNAANZA KUKUBALIKA. HONGERA DK SILAHA KWENDA KUOMBA RADHI KIUTU UZIMA, YOU'RE MAKING A CHAPTER IN HISTORY. UMEONESHA KUTHAMINI NA KUKUBALI KUWA TZ SI YA CHADEMA NA CCM TU BALI NI YA WOTE SO HATA WAZEE WETU NA NDUGU ZETU WASIO NA VYAMA WANA HAKI YA KUISHI BILA VURUGU. Mndengereko, ukerewe

    ReplyDelete
  10. Huu ni ukomavu wa siasa nchini. Hongera sana Mzee mzima JK. Pia hongera zangu sana kwa Mkuu Slaa kwa kukubali kufanya amani na Mkuu wa nchi, hili ni jambo zuri sana na la Kihistoria. Tanzania tudumishe amani na umoja...tutafika tu tuendapo! Bila kuwa na papara za ajabu ajabu na kutaka mambo yaliyo nje ya uwezo wetu.....cha muhimu sana tukomeshe na kuzibiti ipasavyo Mafisadi.

    HONGERA SANA MZEE MZIMA JK....HONGERA SANA DKT.SLAA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...