TAARIFA ya iliyotufikia hivi punde katika inaeleza kuwa mbunge wa jimbo la ARUMERU kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mh. Jeremia Sumari (pichani) amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili mara baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Mh. Jeremia Sumari ni mbunge wa pili kufariki dunia kwa mwaka huu 2012 kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kutanguliwa na Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Morogoro,Marehemu Regia Mtema aliyezikwa nyumbani kwao Ifakara Mkoani Morogoro jana na mazishi yake yaliongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Kikwete.
Globu ya Jamii inaendelea kufuatilia taratibu zote za msiba huu na tutaendelea kutoa taarifa kadri zitakavyokuwa zikitufikia.
Mungu ailaze roho za marehemu mahala pema peponi
-Amen
haya Tendwa lalamika sasa kuwa ni bilioni 19 nyingine hizo za uchaguzi!
ReplyDeletePoleni familia ya marehemu,ndugu jamaa na marafiki na vyama vyote vya siasa,mungu awape muongozo ktk msiba huu.
ReplyDeleteDuh,poleni familia, poleni serikali,BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIBARIKIWE
ReplyDeletethis is another tragedy. Poleni sana familia ya mzee sumari. Haya yote ni mambo ya mungu, wote safari yetu ni mmoja.
ReplyDeleteNB MSILETE SIASA KWENYE MAMBO YA VIFO.ISSUE YA TENDWA HAPA IS IRRELEVANT. THOUGH YOU HAVE RIGHT TO TALK. ALICHOKIZUNGUMZA TENDA NI KWAMBA KAMA TUNAWEZA KUEPUKA KUTIMUANA INA BORA ZAID. SASA MAMBO VIFO TUTAYAEPUKA VIPI. HACHENI HIZO BWANA.
poleni sana wafiwa
ReplyDeletetendwa alijihusisha kwa kulalamika kuwa cuf inasababisha ghalama nyingine za uchaguzi
hakuweza kufahamu kuwa jambo lolote linaweza kutokea iwe kisheria au kwa mkono wa mungu
sasa kuna majimbo mangapi yanahitaji uchaguzi?
ni ghalama ngapi zitatumika kufanikisha zoezi hilo?
viongozi wetu sio mnakurupuka tu kwa kutoa hoja binafsi zisizo na point yeyote sasa hapo utamlalamikia nani?
mungu ibariki tanzania wabariki na watu wake
mungu waongoze viongozi wetu wa tanzania njia bora na imara yenye mafanikio kwa taifa na wasiwe wabinafsi.
Eee Mwenyezi Mungu ILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI. AMINA.
ReplyDeleteMdau wa kwanza sielewi kwa nini umeunganisha sababu za kifo na za kufukuzana. Wewe mwenyewe unajuwa kifo ni swala ambalo binadamu hana udhibiti nalo na tendwa kusema vile alikuwa na maana kuwa vyama vinatumia vibaya nafasi waliyopewa ya kudhamini wabunge ndo maana akawalamikia kuwa ni gharama kwa serikali kwa kuwa kufukuza wabunge hovyohovyo kunasababisha kuwa na chaguzi ndogo ambayo ni gharama kwa serikali. Lakini kamwe hakuhusisha na vifo vya wabunge. Poleni wanfamilia na watanzania kwa ujumla mwenyezi mungu haulizwi mbele kwake nyuma kwetu
ReplyDeletePole Mama Sumari poleni watoto kisali, sioi, Joan na wengine kwa msiba huu mkubwa WA Baba yenu Mpenzi Bwana ametoa na bwana ametwaa jinalake na lihimidiwe.(Ndugu yenu wa LJS) POLENI SANA.
ReplyDeleteWe anon wa Thu Jan 12,12:16:00 pm 2012 Funga domo lako wewe mwenyewe unaendeleza siasa hapa ivi ungekaa kimya ingekuwaje ungekuwa na akili na busara usingetoa hoja hiyo ambapo tayari ulisha ona kuwa ni tatizo.
ReplyDeleteMay He Rest In Peace.
ReplyDeletecjui baba rizi na huu ataenda??maan huwa nafikiria sie 2naofanya kaz kwa wahindi 2ngekuwa 2naaga na kuhudhuria misiba ka baba riz cjui ka 2ngekuwa na kazi hadi leo??maana baba rizi anaanzia dar hadi tanga analalia....mungu aiweke roho yake pema pepon
ReplyDeleteIts so sad! Mungu ampumzishe kwa amani,Amen.
ReplyDeleteDuh hizi nywele nilifikiri MWAPACHU niliposoma ndio nikakuta SUMARI, poleni wafiwa.
ReplyDelete