Vijana wa Chipukizi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika mazoezi ya kutembea kwa ukakamavu, wakati ma mazoezi ya maandalizi ya gwaride maalum la vijana wa CCM kwa ajili ya kilele cha miaka 35 ya CCM, leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Vijana wa kike wakionyesha ukakamavu wao wakati wa mazoezi ya gwaride maalum la umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) kwa ajili ya sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 35 ya CCM zitakazofanyika Kitaifa jijini Mwanza.
Brass band itakayoongoza gwaride maalum la Vijana wa CCM, ikiwa katika mazoezi leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Vijana wanaofanya mazoezi ya gwaride maalum wakitoka kwenye Uwanja wakati wa mapumziko baada ya mazoezi hayo leo.
Vijana wanaoshiriki mazoezi kwa ajili ya gwaride maalum la sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 35 ya CCM wakipumzika baada ya mazoezi leo asubuhi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Vijana hao wanaoshiriki mazoezi ya gwaride maalum la miaka 35 ya CCM, tangu waweke kambi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, hupata mahitaji yao hapo ikiwemo chakula. Pichani chakula kikiandaaliwa kwenye Uwanja huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Uwanja huo siyo wa CCM tena..ubadilishwe jina

    David V

    ReplyDelete
  2. Uchafuzi wa mazingira na uharibifu wa uwanja kwa kupikia uwanjani.
    Na nyie vijana mnaelewa hasa mnachokifanya au mmeingizwa tu kichwa kichwa?

    ReplyDelete
  3. mtinda wa vyama vya kisiasa kupewa mafunzo ya kijeshi ni hatari kwa usalama wa taifa,vijana kama hao huweza kutuiwa kuleta ghasia pindi vyama vyao vikishindwa ktk chaguzi za kitaifa.magamba watapinga lakini kumbuka walisha onywa!!!!

    ReplyDelete
  4. Watu wa mazingira mpoo, hizo kuni zimetoka wapi? miti hiyo inakatwa na sisi tunazitumia kama kawa

    ReplyDelete
  5. Umasikini unatumaliza kakyanani... whatever happened to INTEGRITY and RESPECT! Ni kutumiana na kutokana na ugumu wetu wa maisha,duh!

    ReplyDelete
  6. inashangaza sana kwa miaka yote hiyo watu bado wanafanywa wajinga...badala watoto kuwapa elimu mnawaita kwenye uchipukizi...bless my parents walikuwa hawataki ujinga kama huu zaidi ya kusikia natafuta marafiki tukasome.

    ReplyDelete
  7. hivi jamani wapi tunaelekea?viwanja vya mpira vinahitaji utunzaji wa hali ya juu na sio kufanyiwa sherehe katikati ya uwanja wa mpira watu wanapika halafu wahusika wapo kimya kwa hali hii kweli tutafika?

    ReplyDelete
  8. Huu ndio utamaduni wa kTZ kutokujali thamani ya vizuri. Iweje pasiwepo pahali maalumu pa kupikia chakula na iwe ndani ya uwanja na sihivyo tu tena kwa kuni.

    ReplyDelete
  9. Hawa vijana chipukizi kweli kiboko, wengine wanaanza kutoka vipara bado ni chipukizi?

    ReplyDelete
  10. Hivi kweli tuko serious? hawa vijana wanaweka kambi uwanjani kucheza gwaride badala ya kufanya shughuli za kuzalisha mali? hivi idadi hii ya vijana wangetumia nguvu hii kuzalisha mali si wangekuwa mbali?

    ReplyDelete
  11. siasa za bongo zinatia kichefuchefu sana!

    ReplyDelete
  12. "Hivi kweli tuko serious? hawa vijana wanaweka kambi uwanjani kucheza gwaride badala ya kufanya shughuli za kuzalisha mali? hivi idadi hii ya vijana wangetumia nguvu hii kuzalisha mali si wangekuwa mbali?"
    Anony ukweli ni kwamba hawa vijana hawana kazi. Ni vijana wanaozurura tu mjini bila kazi- hivyo wamekusanywa kufanikisha hiyo shughuli na wao kuambulia mlo na pengine buku moja moja au mbili kila siku. Kwa maneno mengine kwao hii ni ajira ya muda!!! Hii ndio Bongo.

    ReplyDelete
  13. Chipukizi gani hao. Maana ya chipukizi ni kitu kinachochipukia yaani kichanga hivyo wanatakiwa angalau wawe chini ya miaka 16. Sasa hao hapo uwanjani akimama watu wazima na mibaba iliyojukuu bado mwawaita chipukizi?

    Kwenye shughuli za chama tawala shaba halikai mbali na hicho ndicho walichofuata hapo uwanjani.

    ReplyDelete
  14. Watakuja kujua wanapoteza muda wao wakati its too late.

    ReplyDelete
  15. SAFI SANA! CCM NI IMARA NA ITAENDELEA KUWA IMARA; WALE WANAOKIUNGA MKONO KILE CHAMA CHA UPINZANI CHA CHUKI, UONGO, UDINI NA VURUGU WATENDELEA KULIA MACHOZI YA MAJONZI. MUNGU IBARIKI CCM, MUNGU IBARIKI TANZANIA. AMIN.

    ReplyDelete
  16. Jamani hapo juu mmeongea na mimi nawaunga mkono. Lakini hawa wazee wa Magamba wanaelewa? Kusikia kwa kenge mpaka atoke damu.

    ReplyDelete
  17. inawezekana wanapoteza muda lakini kama kweli hao wanapoteza muda kwa mazoezi ya sherehe za chama chao kweli je unasemaje kwa wale wanaoandamana kila kukicha na hata kudai mikesha hadi kieleweke? ACHENI HIZO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...