TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Gazeti la Mwananchi la leo, Jumanne, Januari 31, 2012 limeandika habari zenye kichwa cha habari – JK abariki posho mpya za Wabunge: Kila mmoja kulipwa sh 330,000 kwa siku.

Habari hizi siyo za kweli na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inataka kutoa ufafanuzi ufuatao:

Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu suala hili yako wazi kabisa na hakuna mahali ambako Rais Kikwete amebariki posho hizi.

Maelekezo ya Mheshimiwa Rais kuhusu suala hili ni kama ifuatavyo:

Kwanza, Mheshimiwa Rais Kikwete anakubali haja ya kuangalia upya posho kwa Wabunge lakini amewataka wabunge kutumia hekima na busara katika kulitafakari suala hili.

Pili, Mheshimiwa Rais Kikwete amewataka Wabunge kutumia Kikao cha sasa cha Bunge kulizungumza upya suala hilo.

Mwisho.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
31 Januari, 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. Hili la wabunge na madaktari ni funzo kubwa kuhusu ubinafsi wa watanzania. Madaktari kwa upande wao wamejiona wao ni bora kuliko watu wa sekta zingine na kuamua kudai maslahi makubwa kuliko wengine. Hata hao wabunge walitumia udhaifu huohuo wa ubinafsi kudai maslahi yao wenyewe kana kwamba wao ndio wazalishaji wakubwa nchi hii. Kwakuwa wabunge wana maamuzi kuhusu hili, ndio maana kwao hakukuwa na vuta nikuvute na spika akatangaza kabisa kuwa ni haki yao. Kwa madaktari hali imekuwa tofauti kwa vile hawana maamuzi ya juu. Hatutafika kwa ubinafsi huu!

    ReplyDelete
  2. SO hapa nani muongo, ni Gayeti la mwaananchi or Pinda?. Mwananchi liliandika hivi
    WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amesema tayari Rais Jakaya Kikwete amesaini kuidhinisha ongezeko la posho za vikao (sitting allowance) kwa wabunge kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000.

    Je Pinda yeye anasemaje?

    ReplyDelete
  3. mmezidi upole, Hamna meno au mnahofu na ukweli? Kila kukicha mnakanusha habari za mwananchi, kwa nini msilichukulie hatua? Na ungekuwa wakati wa ze-ukapa, wangekuwa wamekwisha tokomea mbali tumewasahau!

    ReplyDelete
  4. Kwa nini aangalie Posho za Wabunge wakati Wanaodai mabadiliko ni MADAKITARI?

    ReplyDelete
  5. Kwa (Labor Economists) Wanauchumi wa Nguvu Kazi Waliobobea huko kwa wenyewe wakifanya mahesabu na wakachora grafu (curve) ya kubaini kiwango anachostahili Mbunge kulipwa kwa Vigezo vya Kitaalamu itatokea grafu itaonyesha:

    MBUNGE alipwe posho (isiozidi) Tsh. 4,500/= kwa siku wakati DAKITARI ndio alipwe Tshs.200,000/= kwa siku au zaidi...

    Kwa Kigezo cha kwanza DOCTOR/ POPULATION RATION ni 1:>1,500 (Katika Tanzania DAKITARI MMOJA ANAHUDUMIA WATU ZAIDI YA 1,500) !!!!

    SASA HII LABOR ECONOMICS INAYOMPA MBUNGE POSHO KUBWA ZAIDI YA DAKITARI NI ,,,LABOR ECONOMICS YA KIZARAMO!

    ReplyDelete
  6. Hapo tumekuelewa! Sasa Bw. Pinda na Bi. Makinda wameongea kisichoeleweka. Siyo gazeti tu la mwananchi limeandika hilo ila karibu vyombo vingi vya habari. Kwa hilo Rais yupo sahihi, hiyo posho italeta mtafaruku mkubwa..tumeona wabunge na mawaziri walivyokuwa wakikimbilia hizo posho lakini hakuna wanachokifanya zaidi ya kujali maslahi yao. wanataka kuwapiga wanaopinga posho hizo. Big up Makamba, Zitto, Kigwangala na majority wa CHADEMA

    ReplyDelete
  7. Hili gazetini la mwananchi linamilikiwa na nani???. Mana kama linatoa habari za uongo linapaswa kuwajibishwa kwa kupoteza umma wa tanzania wote. Hii ni kinyume na maadili ya uwanahabari na kosa kubwa sana linafikia kuisemea uwongo serikali.Linawapotoza wananchi kwa namna hii.

    ReplyDelete
  8. wabunge hawakutumia hekima mara ya kwanza? mbona hamueleweki?

    ReplyDelete
  9. this is very interesting kwa kweli, inakuwaje basi hata PM anaseka Mhe. Rais amebariki posho hizo. tatizo nilionalo hapa ni mkanganyiko wa mawasilianao ndani ya serikali.

    ReplyDelete
  10. Ikulu mbona habari yenyewe haina hata nguvu..hamkutakiwa hata kujihangaisha na kujibu hiyo habari.Gazeti limewaingiza mtegoni

    Kubariki ni nini??Nani ana uwezo wa kubariki kitu??Tukishapata majibu ndiyo tuliongelee hilo suala.

    David V

    ReplyDelete
  11. KULETA SIASA KWENYE MAMBO MAKUBWA YA KITAIFA YATAIANGAMIZA SERIKALI YA CCM NA TUNASHUKURU SASA TUNAJUA NANI ANA NIA YA KUTULETEA MAENDELA NA NANI HANA.KULENI HIZO KWA MARA YA MWISHO,INAWEZEKANA WENGI WENU TUKAWAPIGA CHINI UCHAGUZI UJAO.
    WATENDAJI WA SERIKALI AMBAO PIA SI WANASIASA ACHENI KUJIPENDEKEZA KUJIBU VITU KIJINGA NASEMA KIJINGA KWA SABABU RAISI KAOGOPA KUKATAA,KAWARUDISHIA WABUNGE NA WAO WAMESEMA HAWANA LA KUBADILI ILA WANACHOTAKA NI PESA HIYO ILIPWE.
    HAPO UNATAKA KUJENGA HOJA GANI ILI WATANZANIA WA KARNE HII WASIKUONE WEWE NI MJINGA NA KIONGOZI USIYE NA MWEREKEO BALI UNAFANYA VITU KWA KUFUTATA UPEPO.
    MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  12. nnandika huku nikiwa na majonzi makubwa,kuona nchi inaendeshwa ktk mfumo wa kijiwe cha kahawa au fitina kati ya simba na yanga. hakika imedhihiri kwamba nchi haina uongozi, bali inajiendesha kwa uweza wake mwenyezi wake mola.kwa kuwa na kauli tatu tofauti kwa suala moja, sasa ni wakati kwa watanzania kutazama upya yule aliepewa dhamana, kwanza kaisha lewa madaraka, pili hajitambui anapaswa kufanya nini kwa boss wake(wananchi). bali sasa anafanya ya kwake akiwa anajiamini kwamba yuko salama.tafakari mwananchi ,chukuwa hatua.

    ReplyDelete
  13. Haya sasa...msikilizeni sana Zitto, alikwishasema taarifa alizonazo ni kwamba JK hajasaini posho mpya...na si Pinda wala Makinda walikuwa wanalijua hilo. Huo ndio umakini wa CHDM.

    ReplyDelete
  14. Tumwamini nani? Kila kiongozi anasema stori yake. Spika: wabunge wamelipwa
    Katibu wa Bunge: posho mpya hazijalipwa
    Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu: posho hazijalipwa, ila wabunge watumie busara kujadili
    Waandishi: Raisi abariki posho za wabunge.
    Wabunge wanapambana na kkumana kwenye vyombo vya habari 'live' wakitetea posho.
    VIONGOZI WETU HAWANA MAADILI, WANAKUWA IGEUGEU. KILA MMOJA NI MWIZI WA WAZAZI WAKE NA JAMII YAKE ILIOMLEA

    ReplyDelete
  15. Sa ndo mmesema nini?? WTF?

    ReplyDelete
  16. kwa kweli mwananchi wameudanganya umma wa watanzania si Tanzania pekee ila duniani kote. sasa basi inabidi kuwepo adhabu ili iwe fundisho kwa wengine ikizingatiwa kuwa kuna mgomo wa madokta hii ingeweza kuleta/ imeleta athari zaidi.

    Steven- NW4 London

    ReplyDelete
  17. Pinda na Makinda ni waongo? au hawana mawasiliano na Ikulu?

    ReplyDelete
  18. Mimi nafikiri ifike sehemu tuwe serious sasa maana wananchi tumechoka na habari zinazopingana. Bunge linasema hivi na Ikulu inasema vile. Sasa sisi watu wa kawaida tuelewe kipi au tumuamini nani? Suala la posho kwa kipindi kigumu kama hiki, mbona Wabunge wa Ugiriki walikubali posho za kukatwa na zingine kuondolewa kwa manufaa ya nchi? Hivi Wabunge watakuwa na faida gani wapo kupata hiyo mihela wakati madaktari wanaotutibu sisi wanyonge wakitupwa na kuwekwa kando kana kwamba sio muhimu? Hapa nafikiri, Rais afanye maamuzi magumu ambayo pia nachelea kusema, sijui kama ataweza maana suala hili limechukua muda mrefu na bado amekaa kimya,,,,,

    ReplyDelete
  19. Sasa hwa waandishi wa mwananchi wametoa wapi hizo habari za JK kubariki posho za wabunge?? haya magazeti sasa yameshakuwa ya kimagumashi utata...

    Terry

    ReplyDelete
  20. Chakushangaza Rais anatuma vimemo pale panapokuwa na mazungumzo yanayohusu maslahi ya wabunge, lakini hatujawahi kuona akitoa vimemo pale panapokuwa na madatizo kama yaliyopo sasa ya mgomo wa madaktari, vilevile hatujawahi kuona vimemo pale zinapotekea vurugu nchi, sasa tumelewe vipi ni mambo gani hasa anayapa kipaumbele!!! Kwahiyo inamaanisha waziri mkuu amemdanganya mwandishi wa habari wa gazeti hili? Je ni hatua gani itachukuliwa na Rais ili kudhibitisha kweli hizi ni habari za uongo wabune hawajaongezewa posho. Mbona huko bungeni wanatupiana maneno kuhusiana na hizo posho tuwaelewe vipi. Na badala Rais awaambie wabunge wakae ili kutafuta solutions za mfumuko wa bei na hali ngumu ya maisha kwa wananchi anawataka wakae chini wajadili kuhusu posho zao!!! Kwahiyo badala ya kujadili mambo muhimu ya wananchi waendelee kuweka vikao vya kujadili posho!! You must be kidding us you are not sereous you don't even care about your people!

    ReplyDelete
  21. Nadhani ni wakati wa vunja jungu sasa umefika. Wanaosema amebariki waje na ushahidi; yaani alipoandika hilo. Na Mh. JK avunje ukimya atuambie wananchi ukweli. TUNATAKA KUJUA UKWELI WA JAMBO HILI.

    ReplyDelete
  22. Siasa hizo, hatutaki siasa wakati huu.hivi kweli mkaa kitako na pia msinziaji anapewa posho hii wakati mtoa huduma, tena za afya anapuuzwa! itabidi tukutane kwenye "tahriri square" yetu soon kuhusu ili suala.
    Imefika wakati sasa wananchi tunapata dhambi kwa mungu kushindwa hata kutetea mambo yanayotuhusu, mungu anapenda ukionewa ujitetee.
    Mdau Mbegu

    ReplyDelete
  23. JE hizo posho zilishaanza kulipwa au bado?
    kama bado jibu mnalo wenyewe na kama tayari majibu tunayo sisi

    ReplyDelete
  24. viongozi wa kibongo mara wapatapo madaraka wanawaza tu jinsi ya kukandamiza wananchi kwa manufaa yao, na si kuleta maendeleo inatia hasira sana viva tunisia, egpty etc

    ReplyDelete
  25. Mimi sioni mwananchi kadanganya wapi. Utaratibu wa posho za Wabunge unabarikiwa na rais. Juzi jumatatu Makinda kawatangazia wabunge kuwa posho zimepitishwa na waendelee kulipwa na pinda kaunga mkono. Kwa mantiki hiyo utasema ni nani kabariki. Mwenye uwezo wa kupitisha, karudisha kwa wale wale eti watumie busara. Alikuwa na uwezo wa kukataa lakini kakataa kutumia uwezo huo. Sasa nani mwongo ?

    ReplyDelete
  26. wote vigeugeu, nimwamini nani!!! kigeugeu!! I LOVE THAT SONG wananigeukia!!!

    ReplyDelete
  27. Inaonesha kulikuwa na matumaini ya Raisi kusaini na kuyaonesha Waziri mkuu na Mama Makinda..baadae akashtukia dili! sasa wao wameota????

    ReplyDelete
  28. Kwa hili, Lowasa anatufaa kuwa Rais 2015.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...