SAKATA la nauli mpya ya kivuko cha mv Magogoni limechukua sura mpya baada ya mfanyabiashara maarufu nchini, Azim Dewji (pichani) kuwajia juu wabunge wa mkoa wa Dar es Salaam, akiwataka kuacha kumshambuliaji Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli na badala yake wahangaike kutatua matatizo ya msingi ya wananchi katika majimbo yao.
Wabunge hao wakiongozwa na Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, juzi walizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa, kitendo cha Magufuli kutangaza ongezeko nauli ya kivuko hicho kwa asilimia 100 bila kushirikisha wananchi, hakina tofauti na udikteta.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Dewji alisema wabunge hawapaswi kupinga kila jambo kwa lengo la kujijenga kisiasa na kusisitiza kuwa Magufuli ana hoja za msingi, hivyo aungwe mkono kwa lengo la kuboresha usafiri wa majini katika eneo hilo na jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi.
“Jamani, ongezeko la sh 100 linaleta chokochoko za nini? Leo hii hata ombaomba ukimpa sh 100 anaweza kukurushia usoni. Wanalalamikia shilingi 100 wakati wao walijiongezea posho za laki mbili hawakuona ubaya wowote…nadhani wabunge wa Dar es Salaam walipaswa kumuunga mkono Magufuli ili kivuko kijiendeshe na kutoa huduma bora na za kudumu, badala ya kila kitu kutegemea kitoke serikali kuu.
“Hivi kila kitu kikitoka serikalini, fedha nyingine za maendeleo zitatoka wapi, kama si kuishia kuziba mapungufu kama yanayojitokeza kwenye vivuko vyetu vinapoharibika?” alihoji na kusema kama fedha zisipokusanywa, na vivuko vikapata hitilafu na kushindwa kutoa huduma, watakuwa wa kwanza kudai serikali imewasahau wana-Kigamboni.
Alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa, pesa zitakazokusanywa kutokana na nauli mpya zitachangia pia kulipa ongezeko la posho za wabunge, kwa kuwa ni fedha za wananchi na wabunge wanalipwa kutokana na fedha za walipakodi.
“Daladala zinapanda kila kukicha, hatusikii kelele, sasa angalia, Waziri Magufuli amesema kwa mara ya mwisho bei ya kuvuka kwenda na kutoka Kigamboni ilipandishwa miaka 14 iliyopita, hawaoni kuwa bei hiyo imepitwa sana na wakati?
“Na mbaya zaidi nasikia wanataka wakabidhiwe kazi ya kuendesha kivuko, mbona baadhi yao majimbaoni mwao tayari mambo yameanza kuwa ya shingo, hayaendi kabisa. Nadhani wangejikita katika kustawisha majimbo kwanza, wakishamaliza ndipo waombe kusaidia kazi za wengine, huu kwao si wakati sahihi wa kutoa msaada,” alisema na kuhoji kwanini wasizungumze kumaliza kero nyingine za jijini, ikiwemo foleni.
Kauli ya Dewji, aliyekuwa anazungumza kwa hisia kauli, huku akisisitiza wabunge kuacha kudandia mambo kwa lengo la kupata umaarufu aliouita wenye kuwajenga zaidi kisiasa badala ya kuwanufaisha wananchi wa kawaida, imeibuka huku kukiwa na mjadala mkali tangu kupandishwa kwa nauli za kivuko cha Magogoni.
Jumapili iliyopita, Dk. Magufuli alitangaza kuwa, serikali imeamua kupandisha nauli hiyo kutoka kati ya sh 50 na Sh 100 hadi sh 200 kwa safari moja ya kivuko hicho, kutokana na gharama za uendeshaji kuwa juu. Alisema nauli iliyokuwapo ni ya tangu mwaka 1997, huku nauli ya vivuko vingine zaidi ya 30 nchini imekuwa ikipanda mara kwa mara.
Magufuli alisema kivuko cha Magogoni kimekuwa kikitoza nauli za chini ikilinganishwa na Chato, kinachotoza sh 300, Pangani Sh 200, Kisorya Sh 300, Lugolora Sh 500, Nyakarilo Sh 300, Chato-Bukombo Sh 2,000, Kirambo sh 500 na Utete Sh 300, huku wanafunzi wakisafiri bure.
Sambamba na upandishaji nauli kwa watu, pia nauli ya magari imepanda ambapo madogo yatatozwa Sh 800 na Sh 1,500, pick up sh 1,000 na Sh 2,000 na yale ya kuanzia tani tatu na nusu Sh 5,000 hadi Sh 7,500.
Big up Azim. Hawa wabunge wamekosa busara. Hizi nauli ni toka 1997. Tujiulize katika muda huo kweli nauli hazijapanda sehemu zingine?
ReplyDeleteOngezeko la sh 100 ni wastani wa sh 6,000 kwa mwezi. Au sh 200 kwa siku. Ni kweli hii ndiyo kero kubwa ya wakazi wa Kigamboni? Wabunge wafikirie mikakati ya kuinua hali za wananchi wao ni siyo kulilia sh 200!!
umesema ukweli kabisa hao wabunge hawana jipya yao ya majimbo yanawashinda myika huyo kaka kutafuta umaarufu wakati jimbo lake kunasehem kibao maji hakuna wala umeme na barabara hazipitiki kaka tu kiumbea walengwa wakubwa kwenye hicho kivuko na ni muhim ni wanafunzi ambao hawana kipato na nitegemezi wirara imewafikiria wasafiri bure sioni tatizo jamani maendeleo hayaji kwa unafuu wa maisha wabunge tuache umbea ili muonekane mnawajali wananchi wenu umasikini umewashinda kuuondoa mmebaki mnatafuta umaarufu wa kisiasa hamna jipya kwani mkikaa kimya hamtaonekana?mbungo mwenye jimbo lake anatosha
ReplyDeletenamuunga mkono Dewji ,Magufuli yuko sahihi kabisa,tatizo lake ni ile kauli ya kusema wananchi ''WAPIGE MBIZI '',nilishikwa na mshangao pia .........kwa hili kama yeye ni muungwana awaombe radhi wananchi wa Kigamboni ,na pia mambo kama haya ilibidi awaachie mamlaka zinahusika na kupandisha nauli walisemee.
ReplyDeleteMtanzania
Hivi serikali kila inalopanga linapingwa,iwe ni jambo la maendeleo linapingwa,hivi Tanzania serikali yetu inaongozwa na watu wangapi.Wabunge wameshindwa kabisa kuangalia sehemu muhimu ambazo zinaumiza wananchi wanaangalia kupanda kwa nauli shs 100,kuna wananchi wanaumia kwa mfano wakulima,kila siku dawa zinapanda bei hakuna anayefuatilia hilo,ila sh 100 ya kigamboni inaleta mtafaruku,hao wabunge wa Dar wanaleta usanii,wasimkwaze kabisa Maghufuli,acha achape kazi,na nina imani kama hicho kivuko kingekuwa cha mtu binafsi,watu wa kigamboni wangekuwa wanalipa shs 500 na hakuna ambaye angelalamika,juzi usafiri kutoka Dar kwenda mikoani ulikuwa juu sana hakuna mbunge aliyekwenda ubungo kusaidia wananchi,wananchi waache ushabiki wa kisiasa,hao wabunge wanaweka mazingira ya uchaguzi 2015, na sio kama kweli wanayohaja ya kumsaidia mwananchi bila kuwa ni kujaribu kuchelewesha maendeleo.Angalieni mingine ya lazima kiuchumi.Na hao wananchi wanalalamika lakini kila jioni watu mamejaa kwenye mabar na majumba ya starehe,angalia majumba yaliyojengwa kigamboni ni ya gharama kubwa,sasa leo unatetea serikali ku[pandisha nauli.Enyi wabunge tunaomba mtafakari kabla ya kuingia kwenye vyombo vya habari na kulaumu.
ReplyDeletenafikiri tatizo ni moja tu,la mawazo, watu wa kigamboni wanavyolalamika upandaji wa nauli wana sababu, watu wengi wanadhani mtu anapovuka toka kigamboni kuja upande wa pili inakuwa ndo mwisho wa safari,la hasha, hicho ni kivuko jamani, anatoka kwake anapanda daladala,anafika kivukoni analipia,akifika upande wa pili anapanda tena daladala zaidi ya moja,analipa nauli,hiyo ni kwenda tu,bado hajarudi,na mwananchi wa kawaida.
ReplyDeleteMara ya mwisho ilitolewa takwimu kuwa mapato yatokanayo na ushuru wa kivuko ni milioni 30 kwa mwezi, hiyo ni miaka minne iliyopita,cha kushangaza mpaka leo mapato ni hayohayo,wakati kigamboni watu wameongezeka sana,tena sana.
Serikali iangalie jinsi gani ya kusimamia mapato hayo na kuwaumiza wananchi kwa kuwaongezea nauli. Wahusika wenyewe wananielewa vizuri.
Ongera sana bwana Dewji apo umenikuna ukizingatia wewe uliwahi kukumbana na nguvu ya Magufuri unajuwa uzarendo wake.
ReplyDeleteKuhusu Kigamboni ni swala la wabunge kutokuwa na Hekima kwani juzi wamejiongezea mipesa chungu nzima leo hii kama hatukubuni mbinu ya kuboresha miundo mbinu unategemea tutapata wapi pesa?Haohao wanafilisi nchi kwa kuwa wanaunga mkono mambo hasi na chanya wanapinga.
Ivi kama watu hawawezi kulipa 200 hao ni binadamu wa aina ipi kwa karne hii.
Tunafahamu ugumu wa maisha lakini sio kiasi hicho.
Tusihishi kwa kutaka kudra naomba tufanye kazi na tuwe na mwelekeo.
Nauri natamani ifike mia tano angalau tuongeze mapato na swala la watu kuzurula bila shuguri mjini life,
Kuhusu wizi tafuta njia za kuwabana na sio kumlalamikia Magufuri.
Kama Magufuri atakuwa mbaya nani katika baraza zima la mawaziri atakuwa safi zaidi yake yeye?
kwa taharifa huyo ndo kabeba jahazi.
Mkilitoboa mmezama mwenye masikio na asikie.
Asante sana kwa mawazo manyoofu ya aina yake. Kwa kuongezea, ongezeko hili ukilinganisha na hali ya gharama za maisha sio mbaya, na hususani kwa soko hilo la huduma kutawaliwa na mtoa huduma mmoja!(monopoly)!, Ila ingekuwa ni busara zaidi kama sambamba na upandishwaji wa bei, ingeelezwa mpango madhubuti wa kuboresha huduma pia, kama kufunga mitambo ya kisasa ya kudhibiti matumizi ya kivuko kwa mpangilio, nn ukusanyaji wa mapato! Isiishie kupandisha pei tu!
ReplyDeleteUnajua tatizo ni kupenda jazba, ulitegemea magufuli angesema kitu kipi, na wakati anaongea watu wanamzomea. Mkuki kwa nguruwe.......
ReplyDeleteTuwe tunasikiliza hoja inayotolewa na sio kuzomea tu.
Mimi nadhani kama huyu Mbunge wa kigamboni anajaribu kuwaziba macho wapiga kura wake!
ReplyDeleteBadala ya kushughulikia suala la daraja na huo mpango wa mji mpya ambao unatunyima usingizi anakwenda kupigia kelele mambo ambayo sio ya msingi!..Mimi nachoka kabisa mambo ya huyu NDUGULILE.
Kilichowachanganya watu si mia mbili bali usafirishaji wa bidhaa zao, hasa watu wa kipato cha chini na wale wenye biashara za vyakula madukani na magengeni. Kupandisha gharama kwa usafiri wa baiskeli ya matairi matatu kutoka 200 mpaka 1800 na magari madogo kutoka 800 mpaka 1300 hapo ndio wananchi wanahitaji kujua uhalisia upi uliotumika kwa hilo. Tukizingatia zaidi suala zima la usafiri kwa wakazi wa kigamboni watakuwa wanatumia kiasi cha Shs 1000 na pengine zaidi kwa usafiri wakuja na kutoka upande mwingine kwa siku. Tutambue kwa wakazi wasio wanafunzi watapaswa kuvuka (kuingia na kutoka) kwa kiasi cha Shs 400, bila kufikiri kwamba watahitajikaa kupanda usafiri mwingine baada ya kivuko iwe kuelekea kariakoo, Mwenge, Tegeta, Tabata kwa shughuli zao za kila siku ama safari zao za kawaida. Pia tukirudi nyuma watokako sidhani kama wakazi wote wa kigamboni huishi kando ya mahala kivuko kilipo ambapo haziwagharimu gharama nyingine za usafiri. Je kama hutumia usafiri mwingine kabla ya kivuko huko watokako na baada ya kivuko huko waendako ni kiasi gani mkazi wa kigamboni atakitumia kwa siku katika safari yake?, Je wenye kipato cha chini wataweza kujimudu na gharama hizi za usafiri na ugumu huu wa maisha?
ReplyDeleteMbona mnang'ang'ania ongezeko la 100tsh tu?je ni halali guta kulipa 1800tsh na prado. 1500tsh?au mtoto wa miaka mitano kulipa 100tsh na akivaa uniform 50tsh?au mzigo wa 50kg kulipiwa 500tsh?msiwe wavivu wa kuchambua na mnadanganywa na mtu kama dewji!mbona yeye alitaka kuvunja madaraja na boti zake kwenda mwanza au mlikua hamjazaliwa?he is another spinning dr.
ReplyDeleteDewji hongera ukweli unahitajika ili kuondokana na umaskini wa waheshimiwa wetu. Mimi nashauri kwa wabunge hebu fikirini kuhusu kupata mapato toka katika fukwe zetu km. kutoza mia kwa kila mpunga hewa ili wazipeleke kgamboni kusaidia gharama za usafiri.
ReplyDeleteYaleyale wabunge wa Daslam wanafikiri kwa kutumia Makali$&@?*%#<¥£<~\_?!',
ReplyDeleteKauli hii ya Azim Dewji ni ya kusikitisha. Lakini tusisahau, kuwa Azim Dewji nae ni mfanyabiashara. Kauli hii inaweza kumjenga kibiashara. Mwaka 2005 Magufuli alimzuia kupitisha maboti yake kwa njia ya barabara. Yakapitia Kenya na alilalamika sana. Na tangu mwaka 2007 kampuni ya Azim Dewji ya Lake Fast Ferries inafanya biashara kule Kanda ya Ziwa. Kwanini basi tusiamini kwa Azim Dewji kujitoa muhanga kumtetea Magufuli nako kunamjenga kibiashara kwa vile biashara zake za vivuko ziko kwenye chini ya wizara ya Magufuli?
ReplyDeleteSerekali nzima imekosa mikaati na Ubunifu wa kuendesha mambo mengi, nina hakika upo uwezekano wa hicho kivuko kutoa huduma bure. Kuna sekta nyingi zinazopoteza Pesa wachilia mbali zinazoibiwa katika Wimbi la Ufisadi na Rushwa. Serekali ya Jiji itakuwa na vitega uchumi chungu tele na vitakuwa havina uongozi na usimamizi mzuri hivyo Pesa nyingi Hupotea ambazo zingeweza kuendesha huduma hiyo muhimu bila kuwalipisha Wananchi ambao tayari wanakabiliwa na Malipo kila Kona.
ReplyDeleteKinachoudhi zaidi ni Viongozi Kukosa Lugha ya kistaarabu kwa Waajiri wao (Wananchi) Na hii hutokea hasa kiongozi akishapewa sifa mbili tatu basi Anapanda kichwa na kusahau alikwenda mikono nyuma akitoa Shkamoo mpaka kwa walio wadogo kwake wakati akiomba kura.
Magufuli anaingia katika kundi hilo, wapo wengi, Jihadarini tutawaumbua Uchaguzi unapiga hodi....................!
Good on you Dewji, watu lazima tutafakari sana, wabunge wetu wanalipwa posho ya Sh 200,000 kwa siku ambazo ni more than the minimum wage. Mbone hawaiambii serikali kuongeza mishahara kama kweli hali ya maisha yamepanda. Hao wabunge in wanafiki. Nashangaa kuona Mwanyika naye yuko ku-wassuport - siamini. Come 2015 lazima tuwatupilie mbali hata kama watakuja kwa tiketi ya CCM.
ReplyDeleteMh. Magufuli chapa kazi achana na hao wabunge wanafiki. Waache tabia ya unafiki. Waende majimboni kwao kutatua kero za wananchi. Matatizo majimboni ni mengi sana tena yamekuwa sugu. Mfano kwetu jimbo la ubungo mbunge wetu amekuwa msanii wa kuonekana kwenye media wakati wananchi wamezidiwa na kero - mfano: Barabara mbovu sana hazipitiki! Rudi jimboni mkuu upite kila kata kushirikiana na wananchi kutatua kero Kama ulivyokuwa ukitafuta 'KULA'.
ReplyDeleteMjengwa, Boti za Lake Fast Ferries hazifanyi kazi huku ziwani kama ulivyosema. Zimezuiwa na serikali kufanya kazi kwa sababu zisizoeleweka! mimi niko Mwanza na ninajua ninachokiandika. Siku nyingine kabla hujaandika ufanye uchunguzi kwanza hasa ukichukulia wewe ni mwandishi unayeheshimika.
ReplyDeleteNamuunga mkono Magufuli na Dewji katika jambo hili.
wabunge wapuuzi
ReplyDeleteDewji anatafuta UMAARUFU ! hivi kweli anazungumzia ths 200? mbona haasemi kuhusu maguta na magari? kwanza huyu dewji si alipewa tenda ya kuweka TV pale ferry na kule kiamboni ? mbona ile ya kigamboni haifanyi kazi? NAJIPENDEKEZA KWA MAGUFULI?! na michuzi inaonesha comments nyingi zitakuwa zinamsema huyu umebania ...
ReplyDeleteAsidhani amefika tunajua machafu yake huyu
Namuunga mkono Dewji. Mh Ndugulile nafikiri kuna mambo mengine ulitakiwa kuyashugulikia kabla ya kuanza kupiga kelele kuhusu hili la ongezeko la nauli ya kivuko. Ni lini barabara za mitaa ya Kibada zitachongwa kuwezesha watu kupita kwa urahisi? Naishi kibada. Je ni lini barabara za mitaa zitatengenezwa?
ReplyDeletekuhusu nauli za kivuko. Je ni watu wangapi wa Kigamboni wanaolalamika? mbona idadi ya wanaovuka haijapungua? Mbona idadi ya magari yanayovuka inazidi kula kukicha?
Hawa wabunge wanalalamikia hivyo viwango vipya wanamwakilisha nani? kama ni mwananchi nafikiri waanzie kwenye bei za Umeme, mafuta ya taa, Sukari na bidhaa zingine ambazo ni matumizi ya kila siku
Mjengwa wewe ni mwandishi uliyesomea au mubabaishaji???? kama alizuiwa kupisha barabarani kwa usalama wa madaraja na akatii amri hapo tatizo liko wapi au ulitaka wabunge wa kanda ya ziwa nao waandamane kwa nini amezuiwa wakati alikuwa anawapelekea usafiri. Au na wewe ndo walewale unataka ubunge 2015 ndo maana unajiunga kwenye kundi hilo??? Mnyika fika ubungo uone jioni usafiri nauli inavyoongezwa utakuta gari linaenda kibamba ila linatangaza mwisho kimara 300, ukifika kimara linaenda mbezi 300 likifika mbezi ndo linatangaza kibamba mbezi tu mtu unatumia 600 badala ya 300 na lazima uilipe au vinginevyo utakesha ubungo sasa hapo konda akitangaza nauli yake anasema mitatu kimara kama huna piga chini, ni sawa na kauli ya Magufuli 200 huna piga mbizi au zunguka au ulitaka asemeje??? heko Dewji. Siku hizi hakuna kitu cha 100 hata pipi 200
ReplyDeleteZanziber ng`ang`anieni nchi yenu uku bara kumezidi Ufisadi, kelele majukwahani tu wizi mtupu.
ReplyDeletewanafiki wanafiki kweli kweli wabunge wa dar isitoshe mimi ninayeishi ubungo sisi wakazi wa ubungo tunakero kero balau maji foleni usipyme lakini sijaona mpango madhubuti wa mbunge wetu wa kupita kata kwa kata mtaa kwa mtaa kuwashirikisha wananchi jinsi ya kutatua hizi kero kama si umbea kigamboni wewe mnyika pa kuhusu nini wakati yakwako yamedoda "umbea tu
ReplyDeleteJamani watanzania acheni tabia za kulalamika kila serikali inapopanga vitu. Huyo na hao wanaompinga magufuli nawashangaa sana. Unajua kwanini alisema wapige mbizi. Mimi ni mkazi wa kigamboni hata ungekuwa wewe ungekasirika tu. Watu na nyie wabunge acheni unafiki. Tukubali tukatae Magufuli ni mchapa kazi. Na sisi watanzania kwa sasa tulipofikia tunatakiwa kuwa na viongozi wa aina hiyo ya magufuli sio kuchekeana chekeana kwenye kazi.aNGALIA NCHI ZA WENZETU KAMA RWANDA NA BURUNDI WALIKUWA NA VITA SANA LAKINI BAADA YA KUPATA VIONGOZI AMBAO HAWATAKI MCHEZO WATU WAMEKUWA NA DISCIPLINE. SISI TUMEZOEA KUBEMBELEZWA. WE KIONGOZI AWEZI KUSIMAMA SEHEMU WANANCHI MKAANZA KUMZOMEA HALAFU HAO WABUNGE WANAOKULA PESA ZETU BURE WANASHABIKIAA. KWANZA TUNAPOELEKA JAMANI ITABIDI KWA WATANZANI KIBOKO KITUMIKE ILI HESHIMA IWEPO. KUSEMA KWELI MI NILIKUWA SIAMINI KUMBE KWELI BUNGE LETU SAFARI HII LINA WABUNGE MBUMBUMBU WAENDE SHULE KIDOGO
ReplyDeleteHuu ni upuuzi kweli!wacheni Magufuli atende kazi yake jamani!heee tooo much complain,mbona kigamboni kivuko chake ni bei cheee sana ukilinganisha na vivuko vya mikoa mingine na hakuna ulalamishi?jamani watanzania tusiwe walalamishi wakushinikizwa na baadhi ya wabunge wachokozi tuuu,wamekalia ushabiki usio na maaendeleo kwao kumedoda!Bi up John Pombe Magufuli!kaza uzi baba!
ReplyDeleteHongera Magufuli. ila kwa swala la dewji kuongea hivyo ni siasa tu hapo za kujikomba kwa magufuli na serikalini. zile boti zilikataliwa kupita tz kisa kuvunja madaraja na hatimae zikapita kenya, mbona hatujasikia kama madaraja yalivunjika kenya? serikali ilikataa zisiende ziwa victoria kwa kuhofia kwamba vivuko vinavyo milikiwa na serikali ziwa victoria mf mv bukoba zitakosa wateja, mtu atapanda fast boat yupo bukoba na sio limeli ambalo linaondoka usiku na kufika asubuhi. na kuthibitisha hili, mbona boti zilipofika mwanza hawakuziruhusu kufanya kazi?mwanzo walizuia zisipite kwenye barabara, kwahiyo kauli ya dewji ni siasa ili serikili au waziri husika amfikirie boti zake. tena serikali ni ya kipuuzi, mtu ana leta boti kusaidia usafiri alafu wao wana mzuia, ujinga sana huu.
ReplyDeleteWabunge waache unafiki wanatafuta umaarufu tu. Nakubali inawezekana structure ya upandishaji wa nauli za vyombo ikawa na tatizo sasa badala ya kupendekeza namna ya kuangalia kuwe na uwiano wa upandishaji wa hizo nauli wabunge wanaibuka na kupinga na kumwambia Magufuli aombe radhi? awaombe radhi watu waliokuwa wanamzomea tena kiongozi wao? Mbona mnataka kulea uozo na utovu wa nidhamu kwa ajili ya kujijenga kisiasa kwani sisi hatujui? Mnaona watanzania ni mbumbumbu sana eti?
ReplyDeleteKwa hili mmechemka wabunge wangu poleni hebu shughulikieni matatizo ya msingi ya wananchi wenu.
Big up Magufuli!
Big up Dewji umesema mwanawani.
yaani nikisoma hizo comments,naona wengi wa hao wachangiaji hawaishi kigamboni,nafikiri hawajui wanachoongea. Pia waache ubinafsi, maana inaonekana wanajiangalia wao uwezo wao hawaangalii mtu wa hali ya chini,mtu wa kawaida ambaye kupata riziki inabidi avuke kuja upande wa pili kutafuta wateja,atoke nyumbani kwake apande daladala,afike kivukoni alipie nauli,aje upande wa pili apande tena daladala,tofauti na mtu wa magomeni anaweza akatembea kwa miguu hadi kariakoo,mtu tabata,mwenge,ubungo anapanda gari moja tu hadi kariakoo au posta.
ReplyDeleteTujaribu kutafakari kwa makini sana, mtu alipie guta sh 1800 kuleta nazi upande wa pili,hivi inaingia akilini kweli?
Dewji na wenzio mnao suport kupanda kwa nauli mnaa agenda za siri au sio watanzania maana mnaropokwa tu.
ReplyDeleteDewji na wenzio mnao suport kupanda kwa nauli mnaa agenda za siri au sio watanzania maana mnaropokwa tu.
ReplyDeleteJamani wabunge wa dar es salaam, acheni kuingilia maswala ya maendeleo, mbona mama alipowaongezea posho hamkujibu lolote, mlikaa kimya? wewe mbunge wa ubungo hebu njoo kimara ujioonee mashimo barabarani sehemu za Kimara King'ongo na Bonyokwa ni mahandaki
ReplyDeleteumekaa tu unasubiri kwenda bungeni wakati hata hupiti kuangalia wananchi wako.
Madaraja yamebebwa na maji maeneo ya King'ongo Matosa wananchi wanapita kwa kulipishwa nauli na mateja, umakaa kimya tu.
Hebu tembelea wananchi wako kijana, la sivyo 2015 tunakupiga chini, hakuna danganya toto tena. Njoo Matosa haraka pitia barabara ya King'ongo kwa Komba uone tunavyopata shida na mahandaki, wewe unakula raha tu mjini.
Michu ibanie hii, tena wakati nampa ujumbe maana yeye hajui yanayojili mtaani
Jamani wabunge wa dar es salaam, acheni kuingilia maswala ya maendeleo, mbona mama alipowaongezea posho hamkujibu lolote, mlikaa kimya? wewe mbunge wa ubungo hebu njoo kimara ujioonee mashimo barabarani sehemu za Kimara King'ongo na Bonyokwa ni mahandaki
ReplyDeleteumekaa tu unasubiri kwenda bungeni wakati hata hupiti kuangalia wananchi wako.
Madaraja yamebebwa na maji maeneo ya King'ongo Matosa wananchi wanapita kwa kulipishwa nauli na mateja, umakaa kimya tu.
Hebu tembelea wananchi wako kijana, la sivyo 2015 tunakupiga chini, hakuna danganya toto tena. Njoo Matosa haraka pitia barabara ya King'ongo kwa Komba uone tunavyopata shida na mahandaki, wewe unakula raha tu mjini.
Michu ibanie hii, tena wakati nampa ujumbe maana yeye hajui yanayojili mtaani
Na hicho kivuko kikishindwa kufanya kazi ndiyo itakuwaje? maana msiwe mnasema tu mnatarajia kitatunzwa na nini au kinatumia hayohayo maji kutembelea kulainishia hiyo mitambo?
ReplyDeleteKuweni wakweli mbona sehemu nyingine vipo vivuko kama hiki na nauli zake ziko juu hadi mia tano kwa kichwa?
Acheni mambo yenu hayo na siasa zenu uchwara!