Khadija Khamis na Zahira Bilal-Maelezo Zanzibar.

Rais Mstaafu wa Awamu ya sita Dk Amani Abeid Karume (pichani) amewataka wavuvi kubadilika kwa kuvua kisasa katika bahari kuu ili wapate tija zaidi na kuondokana na umasikini.

Dk. Karume ametoa wito huo leo alipokuwa akizindua Jengo la Ofisi ya Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari kuu Fumba Wilaya ya Mjini magharibi ikiwa ni mwendelezo wa shamra shamra ya kuadhimisha miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Jengo hilo lililogharimu Dola Million mbili na laki tano hamsini limekusudiwa kuleta manufaa kwa Wavuvi ili waweze kulitumia kuinua kipato chao

Dk Karume aliwataka wavuvi waanze kubadilika kwa kutumia jengo la Mamlaka hiyo ili waweze kulinda rasilimali za bahari kuu kwani walindaji wa rasilimali hizo ni wavuvi wenyewe na sio Askari.

Aidha ameitaka mamlaka hiyo ijiimarishe katika kuandaa mikakati na sheria zitakazoweza kuwabana maharamia ambao huvamia sehemu za bahari kuu ya Zanzibar na kufanya shughuli za uvuvi bila idhini ya mamlaka husika.

Amesema kama kutakuwa na udhibiti wa bahari kuu na utekelezwaji wa sheria, mamlaka pia inaweza kuongeza pato la Taifa kutokana na kukata leseni na kulipia kodi kwa wageni ambao wanaitumia Bahari kuu.

Akielezea shughuli za Bahari kuu Dk.Karume amesema ni kubwa kwani uvuvi wa aina hiyo unaelekea kwenye kiwango cha viwanda na masoko ya ndani na nje ya nchi.
Amefahamisha kuwa uvuvi wa bahari kuu ili uweze kuimarika ni lazima kuwepo kwa vyombo vyenye ubora na hadhi ya kisasa ambavyo vinaweza kuhimili masafa marefu na muda mwingi katika bahari

Pia aliwataka wawekezaji kujitokeza kwa wingi katika sekta hiyo kwa ajili ya kuweza kuwapatia ajira wananchi pamoja na kukuza uchumi wa nchi.

Mapema Waziri Waziri wa Mifugo na Uvuvi Said Ali Mbarouk aliishukuru Benki ya Dunia kwa msaada wake kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kufanikisha ujenzi wa jengo hilo na sekta ya Uvuvi kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. YAANI USANII NI KITU IBAYAA SANA.SITOSEMA MENGI.naamini wapo wadau watakao nielewa kwa kusema kauli hii baadaya kusoma habari ambatana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...