![]() |
Rais Jakaya kikwete, Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa Mh Bernard Membe, Katibu Mkuu Kiongozi Mh Ombeni Sefue na waombolezaji wengine wakiwa Mikocheni jijini Dar es salaam jioni hii muda mfupi kabla mwili wa marehemu Aziz Sheween haujasafirishwa kuelekea Moshi kwa maziko |
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inatangaza ratiba ya msiba wa aliyekuwa Mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania Riyadh, Saudi Arabia na Afisa Mambo ya Nje Mkuu wa Wizara Bw. Aziz Sheween.
Mwili wa Marehemu Aziz utawasili Dar es salaam leo tarehe 6/01/2012 Saa Saba Mchana na kupelekwa nyumbani kwake Mikocheni kwa ajili ya Dua na Kumsalia Marehemu.
![]() |
Sehemu ya waombolezaji |
Baada ya Kumsalia Marehemu, msafara wa Mwili wa Marehemu Aziz utaelekea Viwanja vya Ndege vya Mwl. J.K. Nyerere kwa ajili ya safari ya kuelekea Moshi, Kilimanjaro kwa mazishi.
Marehemu Aziz Sheween anatarajiwa kuzikwa kesho tarehe 7/01/2012 baada ya Sala ya Adhuhuri Moshi Mkoani Kilimanjaro.
![]() |
Swala kabla ya kuanza safari |
Kwa niaba ya Uongozi na Wafanyakazi wote wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Katibu Mkuu wa Wizara Bw. John Haule anatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huo.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
P.O. Box 9000
Dar Es Salaam
Tanzania
www.foreigntanzania.blogspot.com
UPUMZIKE KWA AMANI SHEMEJI YETU NA MOLA AKUPUNGUZIE ADHABU YA AKHERA. AMEEN
ReplyDeletenamuamba allah akuweke mahili pema,your one of the kind you will be missed.
ReplyDeleteInnalillah wainaillah rajioun.
ReplyDeleteKweli tumeondokewa na kipenzi chetu Aziz.hapa London tunafanya hitma yake Jumamosi 28.mwezi huu.
Mwnyezi Mungu amlaze mahala pema peponi.
Tanzania Community in London.
Its still hard to believe that you are really gone. Rest in eternal peace Aziz. We will surely miss you.
ReplyDeleteAziz, kweli umetutoka mapema, mwenyezi mungu akulaze peponi.Umeacha pengo kubwa kwa ndugu na marafiki. Upendo wako kwa mdogo na mkubwa haukuwa na mfano.
ReplyDeleteUtaka kwenye roho zetu daima.
Amina.
Rest in peace my dear Brother Sheween! You were so friendly and encouraging person to me during my short stay at the Ministry of Foreign Affairs! Heavenly Father give the family left behind hope and faith of accepting this reality of life!
ReplyDeletehuyu raisi wetu kikwete na yeye mungu amzidishie kwa moyo anaouonyeshe. Misiba mingi kwa viongozi na wasio viongozi ni alama ya ya moyo wake ulivyokuwa mzuri.
ReplyDeleteMWENYEZI MUNGU AKUREHEM NA AWAPE SUBRA WAZEE WAKO,MKEO, WATOTO WAKO,NDUGU ZAKO NA JAMAA WOTE AMEEN.MTANZANIA KUTOKA MAKKAHE
ReplyDeleteTutakukumbuka daima kaka yetu Aziz, mungu akurehemu
ReplyDeleteshemeji yetu mungu akupe raha ya milele,hakuna mfano kama wewe hapa dunia upumzike kwa amani pole rafiki yangu Sophia mungu akupe faraja
ReplyDeleteINNA LILLAHI WA INNA ILLAHI RAJIUN, SISI WA TZ TUISHIO QATAR TUMESHTUSHWA NA KIFO CHA BWANA AZIZ SHEWEEN AMBAE HANA MUDA MREFU UBALOZINI SAUDIA, LICHA YA HIVYO TABIA YAKE NZURI IMETUFANYA WOTE TUMPENDE KWA KASI KUBWA.TUNAWAPA POLE FAMILIA YAKE NA WOTE WANAOHUSIKA. MWENYEEZI MUNGU S.W. AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI -AMEEN.
ReplyDeleteFOR/ TANZANIA COMMUNITY IN QATAR
Kwa taarifa za hitma watu wa UK wasilianeni na Shabaan Kawawa +447731802787.
ReplyDelete