Mery Ayo,arusha
Familia tano zenye watoto zaidi ya ishirini zimelazimika kukimbia makazi yao ya kudumu kwa kipindi cha wiki tano Hadi sasa kwa kuhofia kutembezwa uchi na kupigwa na vijana wa kabila la kimasai”Morani”mara baaada kufanya tohara kwa njia za kisasa sanjari na kuendesha ibada za kupinga maovu yanayoendelea nfdani ya jamii hiyo.
Familia hizo zimelazamika kufanya hivyo kwa kuhofia maisha yao pamoja na maisha ya watoto wao ambapo kundi kubwa la vijana wa kimasai wanawatafuta kwa makosa ya kuharibu na kuvunja mila zao kwa njia ya Sala pamoja na Kufanya tohara Mahospitalini.
Hayo yametokea katika eneo la ujamaa Oljoro Mkoani hapa ambapo kwa muda wa wiki tano familia hizo zimelazimika kukimbia makazi yao kwa kuhofia kutembezwa mitaani Uchi, pamoja na kupigwa kipigo kikali huku baadhi ya waumini wa kanisa la TAG Oljoro Jerusalem wakivunjiwa nyumba zao.
Akiongea na mmoja wa wanafamilia waliolazimika kukimbia nyumba zao kwa hofu ya kutembezwa mitaani Uchi Bw Korduni Wilson,alisema kuwa Morani hao wamekuwa wakifanya vibaya sana kwa kuwa mila wanazozitaka zina madhara sana.
Bw Korduni alieleza kuwa wameamua kufikia uamuzi huo wa kukimbia nyumba zao kwa kuwa wao tayari wameshajua na kufahamu madhara ya kufanya tohara kwa njia ya kienyeji sanjari na kuabudu mila ambazo Morani hao wanazitaka.
“kati ya hizi familia tano nyinginezo hazijakimbia kwa kuwa wamefanya tohara kwa watoto wao bali Morani hao wamekuwa wakidai kuwa wanaharibiwa mambo ya Kimila hasa pale wanaposali kwa maana hiyo wanakataa hata makanisa kwa kuhofia Matambiko, na Mila”aliongeza Bw. Korduni.
Aliongeza kuwa mara baada ya Morani hao kuona kuwa Kanisa linakubali na kusisitiza waumini wake kufanya Tohara kwa njia ya kisasa sanjari na kukataa Mila ambazo zina madhara kwa Mtanzania Morani hao walikataa amri hiyo na kuvunja Kanisa la T.A.G oljoro hali ambayo ilisababisha hasara kubwa sana.
Kwa upande wake Muangalizi wa makanisa ya T.A.G Arusha Oljoro mchungaji Simion Vomo aliwataka viongozi kuanzia ngazi za chini hadi za juu kulinda haki za wananchi kwa kuwa ni wajibu wao.
"Mambo haya yanasikitisha sana kuona sheria ya mila inageuka haki za binadamu na viongozi wa juu wanakuwa tayari wana taarifa za kudhalilishwa kwa watua hawa lakini cha ajabu hatua hazichukuliwi ipasavyo"alisema mchungaji Vomo.
Hata hivyo alisema kuwa wao kama kanisa hawataweza kuwasikiliza Morani hao kwa kuwa madai yao hayana Msingi Kisheria kwani nchi inatakiwa isimamiwe na sheria moja kwani ndio inampa mtu uhuru wa kuabudu popote anapotaka yeye. .
Aliongeza kuwa Kanisa litalazimika kuchukua hatua kali na za kisheria,kwa kuwa Morani hao wanasababisha amani ndani ya miji na Maboma ya wananchi kukosekana hali ambayo kama haitaweza kuchukuliwa tahadhari basi itazaa matatizo makubwa sana katika jamii.
Wazee wa kimasai lazima mlinde utamaduni maana kuna vijana wenu sasa wamejiingiza katika ushoga!!
ReplyDeleteHe he he haaaa,kazi kweli kweli hapa manake inabidi darasa la aina yake ili watu hawa wapate kuelewa dunia.Hizi dini za kimila kwakweli zinamatatizo sana maana kwa sisi tunaamini mungu mmoja tu na ametuumba na kutujaalia akili ya kutafiti mambo mbalimbali ya kisayansi na technologia ndio leo tumefika hapa mpka binaadamu anamfanyia upasuaji mgonjwa ili amtibu maradhi aliokua nayo,sasa hawa ndugu zetu kwani inamaana hawatumiagi kabisa dawa za mahospitali?au ndio dawa za kiasili tu ndio wanajitibu nazo?Akiumwa Malaria wanafanyaje?Sasa hajui haya mambo ya kujifanyia kienyeji wakati mwingine yana madhara makubwa kuliko faida?Hatari hii?
ReplyDeleteHii nchi utafikiri haina Serikali... juzi kuna mchungaji alitembeza mtaani uchi mitaa ya Sakina, hakuna hata mtu wa kuwakataza hawa Morani, kisa anapingana na tohara za Kimaasai kwani baada zinakuwa na mafundisho ambayo ni kinyume na Ukristo... sasa Serikali itakaa kimya hadi lini??
ReplyDeleteNkyason
Utamaduni hauendeshwi kwa kulazimishana bali ni kwa kuelimishana na kuhamasishana!.
ReplyDeleteKinyume cha hapo inakuwa ni uhalifu, ukiukwaji wa sheria, haki na misingi ya ki binaadamu!
Ndio utasikia mfano Nigeria watu wanahamasisha na kusisitiza kwa nguvu Utamaduni kwa msingi wa harakati kama za BOKO HARRAM!.
'Hizi dini za kimila zina matatizo sana' Tukumbuke ni kupitia dini hizi hizi, ndio mana leo hii wamasai wamebaki kama walivyo na utamaduni wao na wakati mwingine hua tunasawifia!
ReplyDeleteTukisoma historia tunajidai kulaani ukoloni pamoja na mambo yao waliotuletea huku tukidai kua tulikua na tamaduni pamoja na dini zetu..kumbe unafki mtupu!
Kumbuka anonymous wa pili,
unacho amini wewe mwenzako haamini
na maisha yake yanakwenda vile..vile!