Ankal na wadau,
Ninavyofahamu mimi wingi wa viongozi ni gharama sana, uwajibikaji
unapungua, urasimu unakuwa mwingi na mbaya zaidi panatokea kutupiana
mpira kwenye mambo muhimu sana hasa yaliyo na utata.

Kwa mfano katika wilaya moja utakuta viongozi weengi kuanzia balozi wa
nyumba kumikumi, mtendaji wa mtaa, mtendaji wa kata, diwani, mkuu wa
wilaya, mbunge wao, bila kusahau mwenyekiti wa kijiji etc. Na wote
hawa wanahitaji kula kwa nyazifa zao.

Niambieni wadau, hatuwezi kupunguza haya?

Mdau mwenzenu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Kila mtu ana majukumu yake. Kwa mfano, Mkuu wa wilaya kuja kushughulikia ugomvi wa mpaka kati ya majirani kijijini ni kaazi kwelikweli. Kwenye hao uliowataja, ni mmbunge tu ndiyo hana kazi maalumu, wengine wote ni muhimu!

    ReplyDelete
  2. kwa upande wangu naona ni kweli kabisa viongozi wamekuwa wengi kupita kiasi na ukiangalia utendaji mbovu.

    ningependelea kila wilaya kuwepo na mbunge na mtendaji wake ambae anaweza kuwa karibu na wilaya hiyo na kufatilia mambo hapo inatosha.

    labda tu kuongezea kuwepo na mwenyekiti wa kila kijiji basi hao wanatosha kuwakilisha wilaya na kuendesha shughuli za wilaya nzima.

    wingi wa viongozi kunapunguza imani kwa wananchi.


    mwana mapinduzi wa badae.

    ReplyDelete
  3. kwa kuwa hawa vingozi kwa mtazamo wako unaona ni wengi wewe ungependelea iweje au katika hao uliowataja ni yupi kiongozi ambaye hastahili.

    ReplyDelete
  4. Manaibu waziri wanakazi gani zaidi ya kusoma ripoti bungeni na ukiwapigia simu kujibu waziri ana taarifa zaidi. Uchumi mbovu, Wizara utitiri, bado zina, waziri, naibu waziri, katibu mkuu, nyingine hata katibu mkuu ana msaidizi wakati wakurugenzi wapo msaidizi, siendi huko kwenye idara, uongozi weeeeeee na wote ni kuhudumiwa na fedha za wafuja jasho.

    ReplyDelete
  5. Kweli kabisa mdau. Hata mimi huwa nashangaa system yetu.
    Mfano mkoa wa Dar. Kuna Meya, Mkuu wa mkoa.
    Kati ya Meya wa jiji na mkuu wa mkoa nani mkubwa kwa yupi.
    wakuu wa wilaya/Manispaa(3)
    Wabunge zaidi ya 3. Bado kuna mkuu wa Polisi wa mkoa. Wakuu wa polisi wilaya.Diwani zaidi ya 3.
    Na hizi nyadhifa ni according na ninavyojua tangu miaka ya 90 nina uhakika sasa hivi wameongezeka zaidi.Afu kitu kingine kila Rais anakuja na wizara zake za ajabu ajabu.. kwanini Wizara zisiwe constant kikatiba haijalishi rais yupi yupo madarakani pawe na wizara zinazojulikana sio kupeana nyadhifa.

    ReplyDelete
  6. Utitiri wa Viongozi una madhara makubwa sana zaidi ya faida kama hivi:

    1.Ufisadi kwa kutenda kibinafsi,
    2.Baadhi ya Viongozi kuhujumu,
    3.Viongozi kutumia madaraka vibaya,
    4.Upendeleo,
    5.Rushwa,
    6.Gharama za uendeshaji zinazidi,
    7.Ubabaishaji kwa kutupiana mpira ni vile hakuna mipaka ya majukumu kwa utitiri, watendaji wanaingiliana na kukwepa mambo.

    Zaidi ya Utitiri wa Viongozi pana maradhi makubwa sana nchini mfano ugonjwa huu wa (Kofia zaidi ya Moja)
    -----------------------------------
    HEBU TUANGALIE, Mfano MTU MMOJA ANA KOFIA TATU NA KATIKA KOFIA HIZO 3 NDANI YA MUDA MMOJA NA SIKU MOJA PANA VIKAO VITATU, SASA ATAHUDHURIA VIPI HAPO?
    -----------------------------------

    Sasa ukiangalia unakuta mtu Mmoja anakuwa Mbunge, Mjumbe wa Bodi sio moja ,bodi kadhaa, anakuwa Mkurugenzi, na kadha wa kadha upuku puku wa vyeo mtu mmoja inakuwa ,utafikiri kama vile watu wengine hawana akili vile au wengine kama vile hawakusoma!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...