Na Woinde Shizza,Arusha
Jumla ya shilingi milioni 15 pamoja na jezi mbili na mipira mitano zimetolewa na wafanyabiashara mbalimbali wa mkoa wa Arusha kwa ajili ya kuisaidia timu ya Jkt Oljoro ambayo inashiriki katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya vodacom Tanzania.
Wafanya biashara hao ambao ni wadau waliongozwa na mkuu wa mkoa wa Arusha walichangia fedha hizo kwa ajali ya kusaidia timu hiyo ambayo ni timu pekee ya mkoani hapa inayoshiriki ligi kuu.
Akiongea wakati wa kukabidhi fedha hizo mkuu wa mkoa wa Arusha Mulongo Magesa alisema kuwa wameamua kuchangia timu hiyo kwakuwa ni timu pekee ya mpira wa miguu ambayo inawakilisha mkoa wa Arusha katika ligi kuu
Alibainisha kuwa amefurahishwa sana kukutana na timu hiyo kwani alivyofika hapa aliulizia kwanza kuhusiana na michezo kwani swala hili la michezo ata raisi ameelezea kuwa iendelezwe.
“kama mkoa kama mkoa na kiongozi wa mkoa michezo ni kipaumbelele katika shughuli zangu zote hivyo nitaakikisha michezo inaendelea katika mkoa wa Arusha na ifikie tuwe na timu hata nne zilizopo ligi kuu’’alisema Mulongo
Alisema kuwa michezo ni ajira hivyo wachezaji wakienda kuwakilisha mkoa wawakilishe vizuri vyema mkoa kwani kwa kupitia michezo pia wanaweza wakapata ajira.
“mnapokuwa mnacheza vizuri kwa amani basi mtaweka washabiki katika amani na upendo na kupitia michezo hii mnatakiwa kuunganisha mkoa ili mkoa uwe mkoa wa amani hili ndio jambo la kwanza nataka mlifanye mtumie michezo yenu kuimarisha amani ya mkoa na wananchi kwa ujumla’alisema Mulungo
Alisema kuwa iwapo watafanya hivyo itawasaidia hata wao wenyewe katika swala zima la ajira kwani kupitia amani yao wanayoonyesha katika michezo wanaweza kupata ajira hata heshima kwa ujumla.
Alisema kuwa yeye akiwa kama mkuu wa mkoa atakuwa na bega kwa bega kuhakikisha hawapati shida iwapo watacheza vizuri na kuonyesha moyo na kubainisha kuwa iwapo watafanya vizuri zaidi watazidi kuwahamashisha wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia michezo.
Alibanisha kuwa kwakuwa timu hii ya Jkt Oljoro inasaidia kutangaza timu ya mkoa wa Arusha hivyo wadau mbalimbali washabiki wajitokeze kuisaidia kwa fedha na kama fedha hamna basi japo kwa kujitokeza katika mechi zao ambazo watazicheza hapa nyumbani pamoja na nje kwa wale ambao wataweza kwenda kuwashangilia.
Aliwataka wachezaji kujituma vilivyo ili kuweza kuendelea kuwapa moyo washabiki wa mpira wa mkoa wa Arusha na nje ya mkoa na wasiiige mambo ya wachezaji wengine ambao wakipata majina kidogo wanabadilika.
“unakuta mchezaji akishaandikwa mara mbilil tatu anaanza kuvuta bangi kutoga masikio na wakati maandalizi yale ya kutoga masiko na hayo yote bora ukafanye zoezi na mengine mengi akiambiwa na mwalimu amsikilizi kisa kaandikwa na kutajwa kwenye radio mara mbili tatu kitu ambacho kinawapoteza wachezaji wengi kwani jamani nyie hamuwaoni wachezaji wa nje wanamahela mabilioni ya mahela lakini bado hawafanyi ujinga hawaridhiki na umaarufuwanatafuta hela japo wanazo hivyo nachotaka kusema msiige jitaidini na mfanye kitu kwa malengo hapo mtafanikiwa”aluisema Mulugo.
Mulugo aliwataka wachezaji wa timu ya Jkt Oljoro kuendelea kuwa na nithamu ili kuweza kuendeleza mkoa pamoja na kutangaza mkoa wao na iwapo watafanya hivyo wadau wengi watajitokeza kwa wingi kuwashika mkono na kuwasadia kwa hali na mali.
katika kikao hicho kulikuwa na wadau wengi waliojitokeza kuishika mkono timu hiyo wakiwemo benki ya NMB ambayo imehaidi jezi mbili pamoja na mipira mitano na vifaa vingine vya mazoezi,mamlaka ya maji safi na maji taka mkoa wa Arusha (AUSA)ambao walitoa milioni moja,|Meya wa jiji la Arusha ambaye alitoa laki tano,Huseni Gonga ambaye alitoa shilingi milioni moja.
Wengine ni Dalia ambaye alitoa milioni mbili,Papa king ambaye alitoa shilingi milioni moja,Matiasi Manga ambaye alitoa milioni moja ,mkuu wa mkoa ambaye ametoa milioni tano pamoja na mkoa ambao wameungana na wilaya ambao walitoa shilingi milioni nne pamoja na mdau mengine ambaye jina lake alikuweza kufahamika mara moja ambaye alitoa viatu pea 30 vya wachezaji.
Pia Mmoja wa wafanyabiashara hao aliyejulikana kwa jina moja la Dalia aliiaidi timu hii kuwa iwapo itafika hatua ya nusu fainali itawazawadia kiasi cha shilingi milionil kumi kwa timu nzima.
Samahani Ankal, naomba unipitishie habari kwa jamaa wa mkoa Mbeya. Waone wenzao wa Arusha walivyokuwa na uzalendo ya kusaida timu zao zifanye vizuri, kwani Mbeya wote (changanya Mbeya TFF, na watu wote wa Mbeya)walifanya uzembe kuachia timu zote mbili, Tukuyu Stars na Magereza zitelemke dalaja. Mpaka kesho nawalaumu kwani wachezaji wetu inabidi waende sehemu nyingine kuchezea timu nyingine za Premier.
ReplyDeleteIts really good to know about the people playing soccer. Good narration.
ReplyDeleteLearn parkour