Na Tiganya Vincent, MAELEZO- Dar es salaam
Zaidi ya washiriki 200 wa Kanisa la Kristo kutoka sehemu mbalimbali nchini wanatarajia kukutana jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuwajengea uwezo waumini wake kuanzia Jumatatu hadi Jumatano.
Hatua hiyo inalenga kuwajengea uwezo kwa ajili kuwafanya waondokane na utegemezi.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Katibu wa Kanisa la Kristo Magomeni Mwembechai Elikana Balandya wakati akiongea na waandishi wa habari .
Waumuni hao wanatarajia kutoka Kanisa la Kristo la Temeke (Mwembeyanga), Mbagala Rangi Tatu, Keko, Luhanga, Mjimwema, Mlandizi, Msasani, Banana, Kitunda, Kigogo, Kingugi, Singida, Arusha na Mbeya.
Alisema kauli mbiu ya mkutano huo ni kujenga uwezo wa waumini na makanisa ili kuondokana na utegemezi.
Balandya aliongeza kuwa Mkutano huu utaendeshwa kwa ushirikiano na Kanisa la Kristo la River-Road, Georgia (Marekani) pamoja na Kanisa la Kristo la Soweto (Afrika Kusini).
Aidha, miongoni mwa washiriki hao kutoka Marekani na Afrika kusini kuna timu ya madaktari itakayotoa huduma ya ushauri wa kitabibu na masuala mbali-mbali ya afya kwa jamii inayoizunguka Kanisa.
Matibabu hayoni ni pamoja na namna ya kujikinga na shinikizo la damu (blood pressure monitoring), uchunguzi wa sukari damuni (blood glucose tests), uchunguzi wa wingi wa mafuta mwilini (blood cholesterol tests), uchunguzi wa uzito unaostahili mwilini (body mass index), na elimu kuhusu saratani, mlango wa kizazi (cervix), matiti, malezi bora ya watoto, na chanjo muhimu.
Alisema kuwa katika mkutano wageni waalikwa wanaotarajiwa katika sherehe za ufunguzi wa mkutano huu ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni (Mgeni rasmi), Mhe. John Mnyika (Mbunge wa Jimbo la Ubungo) na Mhe. Idd Azzan (Mbunge wa Jimbo la Kinondoni
Yote yafanyike kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu na kuwatakatifuza wanadamu,hongereni viongozi wa dhehebu husika kwa kuanza mwaka huku mkionyesha mfano mzuri kwa madhehebu mengine,nawaomba sana washiriki kujituma kwa haki ya kweli ndio msingi wa maendeleo ya kanisa,familia,jamii,taifa na hata dunia."MUNGU amewabariki nyote,ila shetani ndio kwanza anazunguka na kalandinga lake kuwakabidhi kazi wasiomtumikia Mungu".
ReplyDeleteNothing is impossible to them that believe, God give to them that ask, not only proves great faith, it also prove to be a soul winner with great love. God be with you all.
ReplyDeleteOhio USA