Brother Issa,Salaam aleikum.

mie nikiwa kama mdau mkubwa wa libeneke la Globu ya jamii ninasikitika sana kuwa kama Mtanzania inafika wakati mtu analazimika kueleza namna gani anakerwa na mambo yanaendeshwa hapa nchini, hasa kuhusu huduma mbovu ama zisizotolewa kwa wakati.

Kampuni yenye mamlaka na dhamana ya kusambaza umeme nchini, Tanesco wana kitengo cha dharura, a mbacho kwa kuangalia tu kwa nje, inaonekana ni kitengo maalum kwa ajili ya kukabili dharura zote zinazotokea hasa kuhusiana na suala la umeme.

Ninajiuliza kitengo hiki cha dharura cha Tanesco kina tafsiri vipi “dharura”. Kwa mimi ninavyoelewa dharura ni tukiolililotokea bila kutarajiwa na linahitaji kushughulikiwa mapema ili lisilete madhara. Mfano nyaya za umeme zimeanguka ni dharura inayohitaji kushugulikiwa mapema, la sivyo inaweza kusababusha hata ajali. Nimeshangaa kugundua kuwa kwa kitengo hiki cha Tanesco dharura kwao inaweza kuchukua hata siku tatu, nne, tano………..hakuna haraka afrika, hata kwenye dharura?

Nina siku ya tatu sasa tangu kutoa taarifa katika kitengo cha dharura cha Tanesco kuwa nguzo ya umeme inayoleta umeme ninapoishi ina matatizo, inasababisha kutoa cheche na kusababisha umeme ndani ya nyumba kuwaka na kuzima. Zaidi ni kuwa kwa sasa wakati mwingine inaonekana kama moto unawaka kwenye nguzo na inatoa sauti ya kutisha.

Hakuna hatua zozote zimeshachukuliwa na Tanesco hadi sasa kushughulikia tatizo hili licha ya kuwa nimeshafika katika ofisi zao zaidi ya mara kumi na mbili kuulizia. Jawabu ninalopewa ni kuwa fundi yuko njiani atapita………..fikiria jana usiku mida ya saa nne nimepiga simu wakasema fundi yuko njiani kuja, lakini hadi saa saba usiku huyo fundi hakufika. 

Nikatoka kuwafuata ofisini kwao, cha mno sana walichonionyesha ni nakala ya karatasi aliyopewa huyo fundi yenye jina langu na kuambiwa niendelee kusubiri. Lakini hadi asubuhi huyo fundi wala hajafika na tatizo lingali lipo.

Sasa ninajiliza ni kwa nini waseme watashughuliia tatizo wakati wanajua hawatafanya hivyo? Kama mafundi walionao hawatoshi kwa nini wasiseme tarehe na wakati ambao ingewezekana kwa mafundi hao kufika ili kupunguza usumbufu wa wateja kuacha kazi zao kufuatilia huko ofisini kwao.

Hii inarudi palepale kwenye ubora wa huduma zinazotolewa Tanzania na watanzania kwa watanzania. Ni hovyo na tunadharauliana kwa kweli. Inakera mno.

Zaidi ni kuwa hapo Tanesco nimekutana na watanzania wengine ambao nao hiyo haikuwa mara yao ya kwanza kufika hapo na mmoja wao alikuwa kesiya nyaya za umeme kuangukia paa la nyumab yake.
Laiti ningekuwa ni raisi wa nchi hii, sasa waziri mwenye dhamana na kitengo hicho sasa angekuwa anawajibika mwenyewe kushughulikia tatizo hilo ikiwa watu wake wameshindwa!

Mwisho wa yote ninakaa chini na kufikiria kuwa hii ingalini Tanzania yangu na yetu, ninayoipenda na siwezi kuiacha kwenda kokote kwingine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Pole mdau. Hicho ni kitengo cha madili ya kuunganisha umeme nyumba mpya, sio cha dharura. Wanapiga double double. Overtime za miito ya dharura na malipo ya juu kwa juu ya kazi zilizopangwa. We ukitaka waje haraka waambie unaunganisha umeme nyumba mpya. Hata nane usiku wanakuja.

    ReplyDelete
  2. POLE SANA MDAU USHAURI WANGU WEWE BORA UWAPE KITU KIDOGO(RUSHWA)ITASAIDIA VINGINEVYO ITACHUKUA MUDA SANA

    ReplyDelete
  3. TANESCO imepata taarifa hiyo hivyo ndugu mteja nakuomba utupe contact zako na pia eneo lako ni lipi ambalo halijapata huduma.

    pole sana kwa usumbufu

    ReplyDelete
  4. TOA RUSHWA KAKA! NDIO UTAFANIKIWA. MPAKA IKULU UKIWA NA SHIDA LAZIMA UTOE RUSHWA,HIO NDIO TANZANIA. WOTE WANAKWAMBIA WATAKULA POLISI?

    AU WEWE KAKA HUISHI TANZANIA? HIO NDIYO SYSTEM YA MAISHA YA KITANZANIA. KILA KITU NI RUSHWA SIO TANESCO TU . MIMI LEO NI MWEZI WA NANE NYUMBANI KWANGU NAHITAJI LUKU 3 PHASE NAAMBIWA HAKUNA ILA ZIPO KAMA NINA MILLIONI2,5. SASA MIE SISHANGAI NA NIKILIPA RISITI NITAANDIKIWA NI shs LAKI SABA(700,000/=) SASA HIO NDIO TANESCO NENDA HOSPITALI MUHIMBILI AU TEMEKE,MWANANYAMALA KAMA UNA ROHO NDOGO UNAWEZA UKAFUNGWA MAISHA KWA JAZIBA . RUSHWA MPAKA MORTURY ZA MAITI. WEE ACHA TU LAKINI MUNGU YUPO. KUMBUKA LEO HII rAIS HOSSEN MOBARAK WA EGYPT KAHAUKUMIWA ADHABU YA KIFO KWA KUNYONGWA HADHARANI UWANJA WA TAIFA. NA ITAFIKA TANZANIA HATA WALE VIONGOZI WALIOKWISHA STAAFU WATALETWA MAHAKAMANI,NA WOTE WATAHUKUMIWA KIFO KAMA WENGINE AM,BAO TUNAIONA MIFANO YAO KILA SIKU. MUNGU SI ASUMANI

    ReplyDelete
  5. Ndiyo Tanzania ya KIkwete hio baba kama huijui lakini siku zao zitafika nani alijua Tunisia kitanuka,au Egypt au Libya wewe subiri matokeo hata kama maiti zao zitakuwa zimeishaoza lakini zitafufuliwa na kuhukumiwa . wee subiri tu

    ReplyDelete
  6. Dah, yaani hapa kwetu mtu utoe bahshishi ndio upate huduma wakati nchi zingine huduma zinatolewa nzuri na kwa wakati na ndio bahshishi zinatolewa na sisi tunaziita tip! utasikia mtu analalama kuwa watanzania hawatoi tip, kwa huduma za aina hii? yaanihata kamani mimi hapo rushwa nisingetoa, kuteseka kote na bado hela itoke? kwa nini wafanye vituko badala ya kusema tu kuwa fundi angeenda lakini mapatano yafanyike...! na kwanini iwe hivyo? inatia hasira sana!na huyo hao viongozi wengine wamelala kwa raha zao wakakti sisi tunateseka huku uraiani, na wanasahau kuwa ni kodi zetu ndizo zinazolipa mishahara yao......!

    ReplyDelete
  7. Inabidi watanzania tuchukue hatua. Tanesco ni hovyo mno. Huku Tabata meneo ya chama kuna Transforma ili sumbua kipindi cha mvua basi wiki nzima hatukupata umeme pamoja na watu kuwapigia na kuwapigia wakija wanazuga zuga umeme unawaka kidogo chini ya dk 30 unakata hali ilitengemaa baada ya wiki!
    Mimi nimelipia kuingiziwa umeme tangu novemba, nimesubiri baada ya mwezi wameweka tu bracket meter hakuna.Najua tuko wengi wenye kesi kama hiyo. KAMA INGEKUWA NI HIARI YANGU NINGEWAADHIBU TANESCO KWA NJIA YOYOTE AMBAYO INGEFAA KILA NINAPOWAONA NA MAGARI YAO WAKIPITA KUKUSANYA RUSHWA

    ReplyDelete
  8. Pole sana mdau kwa usumbufu. Hii ndiyo Tanzania ya JK. Mawaziri na wabunge wake wanwajibika kwenye kujiongezea posho kwa kisingizio cha gharama za maisha zipo juu. Lakini wanasahau kuwa hata wengine tunaishi Tanzania hiyo hiyo wanayoishi wao. Ugoniwa wa viongozi kuwajibika kwenye maslahi yao tu kumemfanya kila mtanzania mwenye nafasi ale kwa urefu wa kamba yake. Hali hii imezaa rushwa inayotisha. Mtu hataki kufanya kazi aliyoajiriwa kufanya mpaka apewe kitu kidogo (rushwa). Viongozi wakae wakijua haya yana mwisho. Nani alitegemea Mubarak angekuwa anapelekwa mahakamani kwa gari la wagonjwa. Viongozi husika msiweke nta kwenye masikio yenu. Tanzueni matatizo yanayowakabili wananchi wenu. Simamieni dhamana mliyopewa. Msisubiri mpaka mkachelewa. Mdau wa Beijing.

    ReplyDelete
  9. Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.
    KAKA MICHUZI TUFAFANULIE AU TUSIKUINGILIE BINAFSI . WENGINE RUKSA.

    ReplyDelete
  10. kwa sasa tanesco wameshindwa kazi,na wameshindwa kuwaelezea watanzania kwanini wanafahivyo, kama umenunua umeme tarehe 1/1/2012 unapewa lisiti inayohonyesha umenunua umeme tarehe 27/12/2011,na hawajatuambia ni sababu gani himesababisha ilo tatizo au watanzania wenzangu halijawakuta hilo!!!

    ReplyDelete
  11. pole ndugu yangu,kwa sasa tanesco wameshindwda kazi kwa aliye enda kununu umeme tarehe 1/1/2012,unapata lisiti hinaonyesha 27/12/2011 ndo umenunu umeme na hawajasema kitu chochote,au watanzania wenzangu hamjaligundua hilo,

    ReplyDelete
  12. Mdau hapa umenenna la msingi ila usishangae wakaja watu humu globuni kukupinga wewe na haya unayosema. Juzi tu hapa kuna mdau wa majuu aliandika uozo wa kweli hapa nyumbani wahusika (aliowataja) wakaja juu na kuanza kupinga yale aliyoyasema wakati ukweli upo tunauona kila siku. Hivyo usishangae meneja wa Tanesco ama wafanya kazi wake wakaandika majibu kukuambia wewe ni muongo. Ndo TZ hii, yaani raia wanalazimishwa kukubali uozo wa nchi hii, mtu haki yaki yako mpaka ushugulikiwe lazima uonge? Kikwete why na unafanya nini Babaaa?

    ReplyDelete
  13. Hao jamaa ni magamba wote (by the way, ishu ya magamba imeishia wapi, nywele nyeupe kaiua au?).

    ReplyDelete
  14. hATA MIMI NIMEPIGA SIMU TOKA MWAKA JANA 2011 TAREHE 28.12 KUWA UMEME HAUNGII KATIKA LUKU LAKINI CHA AJABU MPAKA SASA HAWAJAFIKA NA KILA SIKU WANASEMA WAPO TEMEKE WATAKUJA MANA MIMI NAKAA MBAGALA!INACHOSHA NIMELALA MKESHA GIZA NA JUZI NIMEKOMBEWA FLAT TV AINA YA PANASONIC INCHI 32,SIMU 4,PESA NA BAADHI YA VITU!KESHO YAKE NILIENDA TENA NIKAMKUTA DADA MMOJA PALE DHARAURA AKAMPIGIA SIMU HUYO FUNDI AKADAI YUPO MBAGALA KONA BAR KIBURUGWA NA NI NJIA HIYOHIYO YA KURUDI KWAO OFISINI CHA AJABU MPAKA SASA HAWAJAFIKA BADO NINA KIZA ILA LEO KUNA MTU ANASEMA NIGONGE WAYA UTAWAKA NAIMI NAOGOPA JAMANI TANESCO MNATUKWAZA!
    tENA MICHUZI NAPENDA UIWEKE HII HAPO JUU NA SIO MAONI SEMA MIMI SIELEWI NAMNA YA KUKUTUMIA NIMEWEKA KAMA MAONI TU ILA IRUSHE LABDA BOSS WA TANESCO ATAISOMA NITAPATA MSAADA!WEZI WANANISUMBUA SANA KISA UMEME SINA!

    ReplyDelete
  15. Hakikisha siku nyingine ukienda kuripoti unavaa magwanda ya kijani na sio ya kaki utapata hudumu baada ya dakika kumi.

    ReplyDelete
  16. mdau-speck dispensary, sinza kwa remmyJanuary 07, 2012

    poleni wadau wenzangu.
    Mimi pia nilishapata tatizo kama hilo cheche zilikuwa zinatoka kwenye nguzo iliyokuwa karibu na geti la kuingilia ndani na kila ukifungua geti nguzo inatema cheche tatizo lilidumu kwa siku nne,kila ukipiga simu wanasema mafundi wana taarifa wanakuja wapo njiani. mbaya zaidi kila ukipiga simu wanaanza upya kunifungulia file na kuchukua maelezo na kuja wala hawaonekani.

    TANESCO HOVYOOOO......

    Mdau-Speck Dispensary(Sinza kwa Remmy)

    ReplyDelete
  17. kama kweli glob hii ni ya jamii tunaomba majibu kutoka tanesco juu ya hili tatizo la kuuziwa umeme tarehe ya mwaka 2012 lakini lisiti zao zinaonyesha umenunua umeme tarehe ya mwaka 2011.WATANZANIA TUNAIBIWA TUNAONA,TUSAIDIE JAMANI MAANA TUKO WENGI TULIOKUTANA NA TATIZO HILO,

    ReplyDelete
  18. kama glob hii ni ya jamii tunaomba itutafutie majibu ya hili la kunua umeme tarehe ya leo 2012 lakini unaandikiwa lisita ya mwaka 2011.TUSAIDIEN JAMANI MAANA NI WATU WENGI TUMEPATA HILI TATIZO

    ReplyDelete
  19. Bila ya kutoa rushwa hilo tatizo utaka nalo milele.

    ReplyDelete
  20. Anony Fri Jan 06, 09:10:00 PM 2012 hebu fafanua.

    ReplyDelete
  21. watanzania bla bla nyingi no action serikali yote imeoza. haina hata pa kuanzia. rahisi zaidi ni kutawaliwa tena na wazungu mambo yatakuwa mazuri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...