Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa Timu za Yanga na Simba ambazo zinadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzani (TBL) kupitia Bia yake ya Kilimanjaro iliyofanyika leo.Kulia ni Katibu Mkuu wa TFF,Angetile Oseah na Kushoto ni Mkurugenzi wa Mahusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steven Kilindo.
Katibu Mkuu wa timu ya Yanga,Selestine Mwesigwa akitoa shukrani zake kwa TBL ikiwa ni kwa niaba ya timu ya Yanga mara baada ya kukabidhiwa vifaa vya michezo kwa ajili ya timu hiyo leo.
Katibu Mkuu wa timu ya Simba,Evodius Mtawala akitoa shukrani zake kwa TBL ikiwa ni kwa niaba ya timu ya Yanga mara baada ya kukabidhiwa vifaa vya michezo kwa ajili ya timu hiyo leo.
Mkurugenzi wa Mahusiano na Sheria wa kampuni ya bia ya Tanzania (TBL), Steven Kilindo (kushoto) akikabidhi jezi kwa Katibu Mkuu wa timu ya Yanga,Selestine Mwesigwa katika hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu za Yanga na Sima iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa TFF.katikati ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe.
Mkurugenzi wa Mahusiano na Sheria wa kampuni ya bia ya Tanzania (TBL), Steven Kilindo (kushoto) akikabidhi jezi kwa  Katibu Mkuu wa timu ya Simba,Evodius Mtawala  katika hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu za Yanga na Sima iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa TFF.katikati ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe.
Baadhi ya Wachezaji wa timu za Yanga na Simba wakiwa wamevalia jezi mpya zilizokabidjiwa leo na TBL kupitia Bia yake ya Kilimanjaro huku wakiwa na viongozi wao na Viongozi wa TBL kwenye picha ya pamoja.

Kampuni ya Bia nchini Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager ambacho ndio mdhamini mkuu wa vilabu vya Simba na Yanga, leo imezipa timu hizo vifaa vipya vya michezo kwa ajili ya kuvitumia katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania 2011/2012, maarufu kama Vodacom Premier League ambayo imepangwa kuanza Januari 21, 2012.

Hii ni mara nyingine kwa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambao ni wadhamini wa vilabu hivi vikongwe kabisa katika historia ya mchezo wa soka hapa nchini vya Simba na Yanga, kuzipatia vifaa vingi vya michezo kwa ajili ya matumizi yao ya michezo ya ligi ya nyumbani na ile ya kimataifa.

Akiongea jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Meneja wa Kilimanjaro George Kavishe alisema “Ikiwa zimebaki siku chache tu kabla ya kuanza kwa ligi kuu mzunguko wa pili wa 2011/2012, TBL ingependa kutangaza tena kwa namna ya kipekee tunavyoguswa na mchezo wa soka hapa nchini. Kwa kuvidhamini vilabu hivi vikongwe vyenye mashabiki wengi zaidi hapa nchini inaonyesha wazi jinsi tunavyothamini maendeleo ya mchezo huu na tunaamini kuwa kwa kufanya hivi tunawapa motisha wachezaji ili waweze kucheza vizuri katika msimu mzima wa ligi ya nyumbani na michezo ya kimataifa”.

Baadhi ya vifaa vya michezo vilivyotolewa na TBL ni pamoja na;-
NO AINA YA KIFAA IDADI
1 Goal Keeper Gloves 6 Pcs
2 Shin – Guard 30 Pairs
3 Football and Training balls 30 Pcs
4 Stop Watch 5 Pcs
5 Captain hamband 5 Pcs
7 Training Shoes 40 Pairs
9 Bibs 60 Pcs
10 Ankle Support 10 Pcs
11 Football boots 35 Pairs
12 Track Suit 40 Pairs
13 Official wear 20 Pairs
14 Training Wear 60 Pairs
15 Match Wear – Local Matches 2 Sets
16 Match Wear – International Matches 2 Sets
17 Casual Wear 20 Pairs


Katika msimu uliopita wa ligi wa 2010/2011, timu ya Yanga iliibuka bingwa wa ligi kuu ya Vodacom na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 25 kutoka TBL huku timu ya Simba iliyoshika nafasi ya pili ikajinyakulia shilingi milioni 15 pia.

Akizungumzia udhamini huu wa TBL kwa timu kongwe za Simba na Yanga, Katibu Mkuu wa TFF Angetile Hosea alisema “TFF inathamini mchango wa TBL katika kukuza mchezo wa soka hapa nchini ambao kwa kiasi kikubwa umesaidia kukuza ari ya mchezo huu kwa wachezaji wa timu hizi kongwe. Pia ni matarajio yetu makubwa kuwa msimu huu utakuwa wenye upinzani na wa kuburudisha sana hata ikiwezekana kuzidi msimu uliopita kwani timu zimefanya usajili mzuri na kuna changamoto pia kutoka timu zilizopanda daraja kwani kwa sasa zimeongezeka na kufikia timu 14.”

Katika kumalizia kikao hicho, Meneja Masoko wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe, alisema, “Ni kweli kuwa TBL tunafanya kile tulichoazimia kwa kufikisha soka la Tanzania katika kilele cha mafanikio. Timu zetu kwa sasa ziko katika hali bora na tunatoa vifaa hivi kaheshimu mkataba wetu, hivyo basi nasi tunaomba hizi timu zetu nazo ziheshimu mkataba wetu vifaa hivi ni kwa ajili ya wachezaji, bechi la ufundi, na hata makocha wa kilabu, Kile ambacho Yanga na Simba zimefanya katika msimu uliopita ndicho walichostahili.

Bila kujali itikadi zao za upinzani wa jadi viongozi hao waliishukuru TBL kwa kuendeleza uhusiano imara na wa muda mrefu katika nyanja ya michezo na kusema kuwa hii ni moja kutimia kwa ndoto za mchezo wa soka kwa timu yeyote hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Tumewachoka hawa TBL, utasidiaje timu mbili tu ambazo tayari zina uwezo?

    Kila siku bingwa ni Saimba ama Yanga, eti wanasema mbona spain ni Barca na Madrid wanasahau kwamba ho wa spain mziki wao ni ulaya yote.

    Kama simba na yanga wata-dominate afrika it is okay.

    ReplyDelete
  2. mjomba mithupu vipi naona lugha gongana captain hamband au captain armband?tujuze pengine mie ndio nimechemsha

    ReplyDelete
  3. kaka Michuzi siye watu wa Simba tumevuta midomo; maana katibu wetu umesema wa Yanga. Ooooh tutaanza kukuona na wewe ni mtani.

    Mdau HK.

    ReplyDelete
  4. ama kweli Ulabu bongo umeshamiri siku hizi, duh.
    Hao mameneja hapa macho yanaonyesha ulabu kama kazi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...