Kauli Mbiu hiyo ndio iliuyokuwa ikitimiwa na Uongozi wa Wilaya Kinondoni mwaka uliopita,sasa leo sijui kwa kuwa ni mwaka mwingine hivyo kauli mbiu hiyo inakuwa imepitwa na wakati?? Maana hapa ni kwenye Kituo cha Daladala cha Kinondoni Manyanya ambapo kuna mrundikano mkubwa sana wa takataka ngumu huku wahusika wakiendelea na mambo yao kana kwamba hakuna kitu chochote kinachoendelea hapa.ama kweli ile kauli mbiu ilikuwa ni mbwembwe tu.
Ukiwa Kinondoni Manyanya hiyo hiyo,katikati ya Barabara ya Kawawa Rodi kuna Takataka zingine zimehifadhiwa.
Ukifika pale kwenye mataa ya kuongozea magari ambapo napo kulikuwa na mambo kama hayo hayo ya kuhifadhi taka.unakutana na kibao hiki kama kinavyosomeka hapa pichani.
Kuna mgomo. UK hapa mshahara wa mfagiaji mitaani ni sawa na mwenye degree. Imefika wakati Bongo nau wafagiaji wakapewa mshahara mzuri. Ni kazi ya hatari na inabidi ifanywe!!
ReplyDeleteSisi watanzania ni wachafu kusema kweli sijui tunaona sifa nchi au jiji letu kuwa na uchafu kila sehemu wazi wazi, Watalii wanatucheka na tunawafukuza kuja nchi yetu kwa namna hii ya uchafu huu.
ReplyDeleteMtoto umleavo ndivo akuavo!!Unapomwambia mtu usitupe taka hapa inabidi umuongoze wapi pakutupa.Na kama utamkataza kutupa taka bila ya kumuonyesha wapi pakutupa basi atatupa hapohapo hata saa nane ya usiku akivizia watu wamelala.Lakini kama tungezoeshwa tokea zamani kwa kujengewa sehemu za kutupa taka na kuchukuliwa kila wiki na serikali nadhani watu wengi tungestaarabika na kuacha uchafu wetu.
ReplyDeleteHivi zile kampeni zilizopigiwa debe mpaka...............zimeishia wapi? Kweli Watanzania kwa kiswahili mrefu hatujambo!
ReplyDeletekwenye bango, hajatupa takataka bali ameegesha mzigo.
ReplyDeleteMichuzi..by any chance have you visited Kigali City?This is not about the Government but it is about the people themselves,a dirty ignorant person is the one that would throw garbage in his own room or backyard but if he goes to throw it outside then he is intelligent enough to know that it is wrong.
ReplyDeleteEbu tuacheni sie ndio tumejizoelea hivi mbona kwingineko pako zaidi ya hii kelele hamna?
ReplyDeleteHapo bila NGOs au WAHISANI hakifanyiki kitu. Pita vile vichochoro baina ya TOGO na Ufipa ndio utaona kasheshe ya UCHAFU.
ReplyDeleteNa nyie nao? mnasema sisi sisi sasa kama wewe huwezi kufanya unataka nani akufanyie? onesha mfano wewe na mimi. Tuamke jamani, sio kupiga domo tu kwenye mtandao
ReplyDeleteile kampeini ya kinondoni uchafu basi imeishia wapi?
ReplyDelete