Kamera Ya Globu ya Jamii iliwanasa watoto hawa ambao waliokuwa wakifanya biashara ya kuuza kuku wa kienyeji  ili hali umri wao ni wakutakiwa kuwa shule kwa wakati huo,kwenye moja ya kituo cha mabasi kilichopo nje kidogo ya mji wa Manyoni,Mkoani Singida.
 Baada ya kukutana na watoto wanaofanya biashara ya kuku,Mbele kidogo iliwanasa hawa ambao walikuwa wamevalia kabisa sare za shule lakini wao walikuwa wakimsaidia bibi yao kupanga magunia ya mkaa barabarani ili wasafiri wanaotumia barabara hiyo waweze kununua na wao waweze kupata chochote.
 Hawa nao walinaswa wakiwa wamebeba mzigo mkubwa kwenye kokoteni.
 Hawa wakipeleka kuni nyumbani ambazo wanazipata mbali na makazi yao hivyo inawalazimu kutembea umbali mrefu kwa kutafuta kuni hizo.
Huyu akielekea shambani na ng'ombe kwa ajili ya kulima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Hayo ndio maisha ya mtoto halisi wa kitanzania. Sio wanaoishi Dar. Hii inathibitisha umasikini uliokithiri wa mtanzania.

    ReplyDelete
  2. inasikitisha sana wabunge wanapoendelea kuomba kuongezwa kwa posho hali ya kuwa viongozi wetu hao hawafikiri maisha ya watoto wetu huko vijijini

    serikali utasema ipo mjini tu maana kila jambo lipo mjini na wananchi wanaoangaliwa sana ni wale wa mjini na wale wa vijijini ndio wamesahauliwa kana kwamba wao sio wananchi

    haya twendeni tu ipo siku itafika ule wakati tunaosubiri kwa hamu.

    ReplyDelete
  3. tuna kazi kubwa ila kuna wabunge huko kuna mmoja wa wabunge wao ili marekani ndiyo ujue kuwa viongozi wa kiafrica ni wabinafsi kazi yao ni kuishi dar tena mmoja wa wabunge ni waziri mwingine alikuwa nishati ,majambazi yanaongezeka badala la kuzalisha wataalamu,kazi yetu ni kuomba misaada na kusaini mikataba ya madini ya ovyo,na kuimba posho za wabunge na kwenda kuzika serikali yote hizi ni gharama kubwa .na sherehe si zizoisha,ila kuna siku wote hao watachoka,jairo si anatoka huku,du

    ReplyDelete
  4. Yaani mbona hiyo kidogo. Machozi yananilenga......

    ReplyDelete
  5. Hao mabinti bado wakienda kuchanja kuni wanapelekewa moto vichakani huko kwa nguvu au kwa kupenda wenyewe..matokeo yake mimba za utotoni.Ni mambo ya kusikitisha

    ReplyDelete
  6. Watoto wa Vijijini wanakula shida kwenda mbele kama yalivyo mazingira magumu huko,,,,wakati Watoto wa Mijini kama Dar hawaendi Shule mpaka wapewe Shs. 500/= ya Viazi!

    ReplyDelete
  7. Yes wakati wa ukombozi utafika tu. Mafisadi na chama chao wana mwisho wao pia, Mungu nimkubwa.

    ReplyDelete
  8. Mara nyingi tatizo linaonekana ugenini tu lakini pale ulipo huwezi kuliona.Afadhali ya hawa wanaouza kuku kuliko wale wa Ubungo kwenye mataa wanaoibia watu na kuomba omba. Ina maana pale Dar hamuwaoni wanaouza karanga, maji baridi, Ice cream n.k?
    Usiseme kwamba ni maisha halisi ya mtoto wa kijijini bali mtoto wa kiafrica. Je, tunafanya lolote kuwasaidia au tunaongea tu huku wengine wakiwapiga picha na kuwaanzishia NGOs ili wapewe misaada kwa wazungu na kunufaika wao huku wakisomesha watoto wao kwa fedha iliyotolewa kuwasaidia maskini na yatima. (Walaaniwe na wajue wanalofanya ni laana).
    Nafikiri tatizo ni nchi nzima na kama tuna posti picha basi hata wale wa Ubungo mataa ambapo wabunge wote huishi hakuna wanalofaidika kuwa karibu na viongozi hata wao uwaposti huku.
    Leteni mipango ya kuwasaidia na isiwe ya kinafiki kama wanavyofanya baadhi ya NGO. "You wanna make change, ask the man in the mirror to change" - Michael Jackson. Charity begin at home so start closer to you- Ubungo mataa, kariakoo round about, mnazi mmoja, faya e.t.c.

    ReplyDelete
  9. Hilo ndilo linatakiwa hata mijini. watoto kama hao wakikua nakuhakikishia wanaweza ishi maisha yao bila shida wala kuwa tegemezi tofauti na mitoto ya mijini ambayo hata ikimaliza chuo kikuu haiwezi jitegemea isipopata ajira.Hao watoto hata wazazi wao wafe leo huwezi kuwakuta kituo cha kulelea yatima wanaweza endelea na maisha kwa kujitegemea.Watoto wa mijini kazi kushinda tuisheni tu kujitegemea na kufanya kazi hawawezi.Wanachelewa mno kujitegemea tofauti na hao wa vijijini.Si kila kitu tuige wazungu.Haio watoto wamefunzwa kupambana na mazingira tangia wadogo tofauti na kuku wa kizungu.

    ReplyDelete
  10. tukiendelea kusema hapa tu bila kutenda mambo yatabaki hivyo hivyo hadi tunaondoka na kuwaachia kizazi kijacho upupu uliotukuka na woga usio kifani!

    ReplyDelete
  11. Mhe. Mbunge anapewa posho yake kwa siku Shs. 200,000/= akitoka kikaoni anawahi Bar analewa na kula nyama choma,,,Watoto Jimboni wanauza KUKU WA KIENYEJI NA MKAA ILI WAWEZE KUSOMA!

    ReplyDelete
  12. Pesa anazotumia raisi kwenda safari za nje kama ya hivi karibuni Davos,Switzerland na posho za wabunge zingewekwa kwenye special fund za watoto wa chini ya miaka 15 wapewe posho ya wiki za kujikimu.sidhani trip za muheshimiwa na posho za wabunge ni muhimu sana kama maisha bora kwa taifa la kesho

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...