Katika hili la nauli za kigamboni, na udhibiti wa mapato yatokanayo na kivuko mimi nina mawazo yafuatayo:

1. kwenye udhibiti wa mapato, ziliwahi kufungwa machine za electronic ticketing pale. Pamoja na machine hizi kugharimu fedha nyingi (mtaani wanasema ziligharimu zaidi ya USD 69,000, labda pengine Mh.Mbunge anaweza kuwa na takwimu sahihi), machine hizo hazikuwahi kufanya kazi hata siku moja tokea zifungwe. Nadhani hatua ya kwanza kuelekea kwenye mipango wa udhibiti wa mapato yatokanayo na kivuko ni kuamsha mashine hizi, na kama hazifahi basi mkandarasi abanwe zifungwe zinazofaa mara moja

2. Suala la nyongeza ya tozo za kivuko linaweza likawa ni sawa. tatizo ni approach yenyewe. Itakumbukwa kuwa hata gharama za usafiri wa mabasi, yote ya mikoani na ndani ya dar, SUMATRA iliwaita wadau wote, wakiwemo wasafirishaji, abiria, nk kujadili suala hilo na makubaliano yalifikiwa. Sasa iweje TEMESA wapange bei mpya bila majadiliano katika suala hili? Sidhani hata kama hao viongozi wa TEMESA ni wakazi wa maeneo ya kigamboni, au ni watumiaji wa mara nyingi wa huduma za kivuko husika, hivyo haikuwa busara wao kufanya maamuzi yahusuyo watu wa kigamboni na watumiaji wa huduma ya kivuko mara kwa mara. lazima kuwe na ushirikishwaji wa kutosha katika suala hili

3. Ni wakati sasa wa kuboresha huduma zitolewazo katika eneo hili. Sijui ni kwa nini mpaka leo serikali imeshindwa kuruhusu huduma za kivuko kutolewa na watu binafsi. Sioni unyeti wowote katika suala hili linaloweza kuzuia huduma hiyo ikatolewa na sekta binafsi, pamoja na serikali kuendelea kutoa huduma katika eneo hilo. Kama kuna watu binafsi wana nia ya kutoa huduma, wapaewe fursa hiyo. Ni kwa kupitia ushindani tu ndipo bei halali ya soko itaweza kupatikana bila misuguano ya namna hii

, na uhakika wa kupata huduma bora kabisa utakuwepo

4. Mwisho, ni ukweli usiopingika kuwa kuna wizi mkubwa sana wa mapato, pamoja na mafuta katika uendeshaji wa kivuko hichi ambao unaligharimu taifa pesa nying sana. Hoja ya Wabunge wa mkoa ya kuomba wapewe wiki mbili kuendesha kivuko ili kuthibitisha hili suala sio nyepesi kama ambavyo watendaji wa wizarani watependa jamii ifikirie kuwa ni hoja ya kisiasa. Ubungo bus terminal, kampuni ya familia moja ilikuwa inakusanya 1.5m kwa siku, lakini jiji walipoamua kukusanya wenyewe, walifikia kupata 4.5m kwa siku. Hii haikuwa siasa. Ilikuwa ni uamuzi uliozingatia hali halisi. Uamuzi kama huo unahitajika kigamboni kwa sasa, kwa mazingira yaliyopo. Kwa ufupi, hatuwaamini tena.
Kauli ya mtu aliyejijengea heshima kwa muda mrefu kuwaambia watu wa kigamboni wapige mbizi ni ishara ya kujisahau, na kufikia mahali watawala wakajiona kuwa wao ni miungu, na maisha ya watanzania yako kwenye utashi wao. Watu hao ni wavivu wa kufikiri, vipofu wa kuona yanayoendelea duniani, na ni malimbukeni wa madaraka. Shafi Adam Shafi aliandika kweneye ukurasa wa mwisho wa kitabu chake cha KULI, "yana mwisho haya".

Wasalaam

Francis Mafuru

Kigamboni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. UWIIIIII,,,,Maisha yanatuendea mrama wakazi au waendaji wa Kigamboni!

    Ile tozo ya Shs. 100/= nanga ilikuwa inapaa na sasa Shs. 200/= itatufikisha kuomba Udhamini tuweze kupata ''SWIMMING COURSE'' Kozi ya kuogelea ili kuwa na uhakika wa safari za kwenda na kurudi Kigamboni, kwa vile siku hazifanani inaweza tokea mtu huna hata ndururu mfukoni unatafuta mfuko wa plastiki unavua nguo unaziweka ndani halafu unajitoza Puuuu,,,Dibwiii unatokea upande wa pili!

    ReplyDelete
  2. Lahaula lakwata!
    Mia moja ilikuwa kama laki kwetu, sasa hii mia mbili tutakuwaje makabwela?

    ReplyDelete
  3. Vingozi wetu inabidi wavae viatu vya watu wanaowangoza kabla ya kuamua maamuzi ambayo mimi ninayaita(irretional decisions) .Kwa vile wao mambo swafi basi hawaoni adhari hasi za maamuzi yao kwa wananchi.Tatizo la kivuko cha kigamboni, sio nauli kua ndogo. Kivuko kinashindwa kujiendesha kwa sababu ya usimamizi mbovu wa mapato, kwa hiyo basi kapandisha bei ya kivuko sio suluhisho la kudumu bali linazua balaa nyingine ambayo mimi naiita sio ya kisiasa kama magufuli anavyodai. Hali ya uchumi ni mbovu hasa kwa wananchi wa hali ya chini wanaotegemea biashara ndogondogo. Kupandisha gharama za usafiri bila sababu za msingi, kutoa matusi( kupiga mbizi) kwa kweli ni ukosefu wa uwajibikaji katika uongozi ambao ni matokeo ya kujisahau. Siombei mabaya, kama viongozi wetu hawatafuata misingi ya uongozi bora ipo siku , wananchi wataweka busara chini na kushikisha viongozi wao adabu. Makufuli inabidi aombe radhi kwa wananchi wa kigamboni,inawezekana tu ni hasira. Asipoomba msamaha,basi hiyo ni dalilili nyingine ya dharau, inabidi tuikeemee na kumwajibisha.

    ReplyDelete
  4. Jamani ningeomba wadau waangalie Woolwich Ferry, London. Ngoma ni free, serikali ndio inalipa. Ninajua huwezi kulinganisha TZ n UK lakini angalau watembea miguu ingekuwa bure kwa wao. Gari moja la mbunge linaeza kuwalipia wadau wangapi?

    ReplyDelete
  5. Naungana na mawazo ya mtoa hoja vivuko viendeshwe na kampuni binafsi ili hali iangaliwe kwa makini, isije kuwa mgogoro wa vituo vya mafuta.

    ReplyDelete
  6. SIKU MOJA, RAFIKI YANGU ALIWAHI KUNIAMBIA YA KUWA MH. MAGUFULI NI DICTATOR

    ReplyDelete
  7. Hongera kwa hoja safi na makini. Naunga mkono. Tembelea www.drfaustine.wordpress.com kusoma barua nilizoandika Serikalini kuhusiana na suala hili.
    Dkt. Faustine Ndugulile M
    Mbunge Kigamboni

    ReplyDelete
  8. Kwani wameshindwa kujifunza hata feri ya Mombasa ni Dree kabisa mtu halipi hata senti moja isipokuwa Magari hulipa kiwango kidogo!!

    ReplyDelete
  9. Mdau Mtoa Maoni wa nne juu
    Anonyomus wa Tue Jan 03,07:37 PM 2012

    Uliyelinganisha Woolwich Ferry ya London UK kwa ''waenda kwa miguu'' wenye nafuu ya maisha ni Free na hapa Kigamboni Tanzania kwenye ''waenda kwa miguu'' maskini waliochoka zaidi watu wanalipa.

    LICHA YA TOFAUTI KATI YA UK NA TANZANIA NAKUUNGA MKONO MDAU KWA DALILI UKIONA MTU ANAENDA KWA MGUU UJUE BUNDI ANAUNGURUMA NA KUWA AMEPIGIKA!

    ReplyDelete
  10. MwanamazingiraJanuary 04, 2012

    Temesa ni Taasisi inayojiendesha yenyewe gharama za uendeshaji zimepanda sana kivuko cha MV magogoni hakisimami kinafanya kazi muda wote,mwaka 1997 lita ya diseli ilikuwa kama Sh.400 now 2000, hivyo kupandishwa kwa nauli hakukwepeki kabisa. Pili swala la kudhibiti mapato ya kivuko limeimarishwa sana sana ila watu wanadai kuna wizi watukamatie basi hao wezi tuwaone sio kulalamika tu bila kuprove hiyo itasaidia hata utendaji kazi. na pale hata wanajeshi wapo wanasimamia zoezi hilo pamoja na Yono Auction mart so watu wanajua kulalamika sana

    ReplyDelete
  11. Wabongo kwa kelele bwana! Sasa mnataka chombo kishindwe fanya kazi kabisa muanze malalamiko mengine:

    1.Kama kuna uvujaji wa mapato wapo wapi PCCB,Polisi,wanaharakati.......?

    2.Kama hao tuliowapa dhamana ya kutuendeshea kivuko wameshindwa kwanini hatuwawajibishi?

    3.Kuteleza kwa ulimi kwa viongozi wetu ni jambo la kawaida mbona aliposema wengine wajinyonge kabla hajawashukia mbona hamkusema?

    Jamani tusiwapotoshe wananchi wetu kwa ubinafsi na ulafi wetu. Tuwaamini wataalamu wetu na tuwaabane pale wanaposhindwa kuwajibika badala kuwavunja moyo.

    ReplyDelete
  12. Mimi naomba kupingana na maoni yenu hata huyo mbuge wa Kigamboni. Hivi kwa gharama za maisha zilivyo panda mbona walivyopandisha nauli za daladala mlikaa kimya, vyakula vimepanda mko kimya, kuna familia hata mchele kwao siku hizi ni kituo cha polisi wakipata unga wakanywa uji wanashukuru Mungu siku inapita mko kimya. Leo 200 ya kivuko imezua mashairi au kuna agenda ya siri???? Ndo yaleyale wakazi wa jangwani eti pale wanatembea kwa miguu kuja mjini hawalipi nauli ndo maana wanapendelea kuishi pale lakini maafa yamewakuta wabunge kimya mbona hampigi kauli za kuwahamisha kuwa hela ya nauli watapata wapi wakitoka jangwani. Tuwe wawazi jamani na wakweli tuache mambo ya siasi. Wakiamishwa mabondeni na mimi naachia ubunge yako wapi???? mbona kimya.

    ReplyDelete
  13. Tatizo ni kivuko kuendeshwa na Serikali lakini ingekuwa ni mtu binafsi wala watu wasingeongea chochote. Lakini mkumbuke nyie wenyewe ndo mnailaumu serikali kila siku kuwa haitoi maamuzi magamu, angalia foleni za morogoro road sisi tunaoishi mbezi ili uwahi mjini saa 11 alfajiri uwe mbezi mwisho ukifika 12 imekula kwako, kwanza magari hakuna nauli ni sh.500 hadi posta ila utajikuta unatumia hata sh.2000 kufika posta, hayo yote mko kimya. Magufuli aliposema kubomoa nyumba ili kuongeza upana wa barabara watu walikuja juu awe na utu sijui nini yote yaliwatoka, sasa angalia tabu tunayopata barabarani ukiondoka mjini saa 11 jioni mbezi saa 3 usiku hivi tutafika kweli bila maamuzi magumu??? wala siona haja ya kuomba msamaha kwa kauli ya kupiga mbizi, sasa kama hataki kulipa nauli ya 200 unategemea nini zunguka mbagala au piga mbizi. Nyerere aliposema tufunge mkanda hali ni mbaya hakukuwa na kuomba radhi hadi kesho tumefunga mikanda wala hakuna wa kusema ifutwe kauli.

    ReplyDelete
  14. Yaani tunaomba Mbunge usitetereke tupo nyuma yako! by the way kuna mashimo pale maeneneo ya Mikadi tunaomba uyafanyie ukarabati yatasababisha ajali kubwa siku moja !

    Ahsante na tunaziona juhudi zako na tupo pamoja !

    Mdau , Kigamboni

    ReplyDelete
  15. David cameroon ameshauri tuhalalishe usho.. mkakataa mambo yetu yangekuwa safi saa hizi hata tungeomba vivuko viwe vingiiii. Kazi ni kwetu

    ReplyDelete
  16. Nimesoma baadhi ya magazeti yanaelezea kuwa watu wa kigamboni hawako rational, mbona nauli za dala dala zinapanda na watu wengine hawalalamiki. Magazeti hayo yamemkariri Azim Dewji. lakini nadhani huu ni mtazamo usio makini. Azim Dewji na wengine wanaosema maneno hayo wanasahau pia kuwa hata wananchi wa kigamboni pia wanatumia usafiri wa dala dala kabla na baada ya kutumia kivuko. Hivyo Kupanda kwa gharama za Kivuko, ni nyongeza nyingine katika mahitaji ya mwananchi wa kigamboni ukilinganisha na mwananchi wa Tabata ambae kwake yeye atalipa ile ya dala dala tu (hana gharama nyingine ya kulipia kama ambavyo mwananchi wa kigamboni anayolazimika kulipia kivuko). Ni suala linalohitaji umakini mkubwa katika kuliangalia.

    Mdau Mtoa mada
    Kigamboni

    ReplyDelete
  17. Gordon ChiggsJanuary 04, 2012

    This is what happens when we have RULERS and NOT LEADERS... Mafuru umeiweka sawia kabisa hii kitu kaka. Tunaenda wapi nchi hii jamani?? huyo huyo Magufuli anajua kiasi cha pesa zinazoibwa kila siku pale kivukoni.. Na jinsi jamaa wanavyoziiba (ikiwamo kuwa na vitabu vya risiti feki) iweje leo ame-side nao kwenye hili??!!! (au ndo 'keshaonwa') INAKERA SANA..

    ReplyDelete
  18. Nilijua tu kuwa Michu utaibania comment yangu. Hovyoooo, huna dira wewe unahemea tumbo kwa watu wa chama cha Magamba! Na hivyo vijipost wanavyokupa ndiyo wamekumaliza kabisa, utumwa huo, amka wewe. Kuna kizazi chako kijacho kitateseka kwa ubinafsi wa Magamba,zinduka weweeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  19. tz haiwezi kufanya hii kitu bure bado maendeleo yapo nyuma sana,mimi binafsi nimeshawahi kuvuka hapo kwa kuogolea lakini for fun nasikua na kazi maalum,nakuomba usijaribu current yake ni kali sana unaweza kuhatarisha maisha.mdau uk

    ReplyDelete
  20. Wadau naomba niulize maswali:

    HIVI HIZI NCHI ZINGINE MASIKINI KAMA SISI AMBAZO VIVUKO VYAO HAWATOZI GHARAMA WENDA KWA MIGUU, HIZI NCHI KUENDESHA VIVUKO VYAO WANA DHAMINIWA NA NANI?,,NA LEO IWE SERIKALI ''KUPE'' YA TANZANIA ISHINDWE?

    ReplyDelete
  21. Ama kweli Serikali yetu CHUMA ULETE!

    ReplyDelete
  22. Mdau mtoa mada, lazima mifano yetu iwe ileileeeeeee, Tabata Liwiti!

    Ila uliyoyaongea yana make sense kichizi. Imagine mtu anakaa Kigamboni alafu anafanya kazi labda Nyerere Rd, au Vingunguti au mbagala au popote pale ambapo sio mjini, jamani mzigo wa nauli unamuelemea acheni utani! Unajua mambo mengine mnayachukulia juujuu tu, lakini ukitafakari kwa makini utaona ugumu uliopo. Mi nawafahamu wananfunzi wanaosoma Mwl. Nyerere pale Kigamboni ambao wanatoka Kitunda, ebu nijumlishie nauli yake kwa siku ni kiasi gani, alafu umchukue mwanafunzi mwingine anayetoka Ilala kwa mfano, nani itakula kwake nauli? Jamani, ailimia 98% ya Watz ni walala hoi, msilisahau hilo, serikali isijasahau!

    Tutafakari, tuache porojo za wafanyabiashara, haohao ndio wenye hivyo vivuko mikoa tofautitofauti ndiyo maana wanachonga sana.

    Tupo pamoja sana mdau mtoa mada!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...