Imamu wa msikiti wa masjid Nuhu Songea mjini,Shekhe Kitete (kushoto) akimfungisha ndoa mtoto wa mwisho wa mwanasiasa mkongwe hapa nchini Hassan Nassor Moyo, Bw Abdallah Moyo, iliyofungwa katika msikiti huo na kufuatiwa na sherehe ya kuwapongeza iliyofanyika katika ukumbi wa parokia ya bombambili manispaa ya songea
Bw Said Moyo ambaye ni kaka wa Bw. Harusi na mtoto wa kwanza wa mwanasiasa mkongwe hapa nchini Hassan Nassor moyo akigonga glass na mdogo wake Abdala moyo (katikati) na kulia ni mke wa mdogo wake Bi Scola Ntara baada ya maharusi hao kufunga ndoa.
Bw Abdala Moyo kushoto akiwa na mkewe Scola Ntara wakishuka jukwaani kuelekea kukata keki baada ya kufunga ndoa
Maharusi Bi Scola Ntara kulia na mumewe Abdala moyo wakikata keki waliyoandaliwa na ndugu,jamaa na marafiki zao baada ya kufunga ndoa katika msikiti wa wilaya ya Songea.PICHA NA MUHIDIN AMRI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Jamani chuo cha ngapi hiki??!

    ReplyDelete
  2. Ndoa hii imeozeshwa vipi msikitini? Naona Abdulla Moyo na Skola Ntara!

    Na halafu bi Skola amepiga 'green', kwa wale ndugu zangu wa kiislamu wataelewa nini namaanisha.

    Anyway tunawatakia kila la kheri katika hiyo ndoa yenu.

    ReplyDelete
  3. Moyo hilo panga,jambia au kisu mdau te ......te...te........

    ReplyDelete
  4. mdau uliyesema bibi arusi "amepiga green" sijui kama ndio colour blindness, iyo sio green bali ni "sky blue" labda nayo uitolee tafsiri

    ReplyDelete
  5. Songea mnajitahidi juzi juzi tumeone send off na kitchen party ya mtoto wa mheshimiwa mbunge jenister - mama kashikia kidedea ile mbaya wakati wenzake wanatuliaga tu huduma inapelekwa na wengine - tokeni na tembeleeni michuzi blog mara kwa mara mjinfunze kwa wenzenu.

    ReplyDelete
  6. Bi harusi ni mkongwe!!

    ReplyDelete
  7. Mzee Hassan Nassor Moyo ni mwanasiasa mkongwe na maarufu kule ZNZ.
    Amewahi kushika nafasi mbali mbali ikiwa ni pamoja na uwaziri. kiasi kwamba wengi wetu hatujui hata kama ni mtu wa huku bara seize kua ni mtu wa songea!
    ..Mambo ya muungano hayo!..CDM watakuja kuiweza kweli hii nchi kutokana na msimamo wao?..Mungu ibariki TZA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...