Meya wa jiji la Arusha,Gaudence Lyimo
Na Mary Ayo,Arusha

MEYA wa jiji la Arusha,Gaudence Lyimo akiungana na baadhi ya madiwani jijini humo wamemshukia mbunge wa jimbo la Arusha mjini,Godbless Lema kwa kumtaka aache tabia ya kupinga kila jambo la maendeleo wakati akiwa vijiweni na kumtaka mbunge huyo awasilishe malalamiko yake kwenye vikao.

Hatua hiyo inafuatia baada ya hivi karibuni mbunge huyo kupinga mradi wa kisasa wa uboreshaji wa mji wa Kaloleni kwa madai kuwa una harufu ya rushwa huku akitabiri hali ya machafuko katika jiji la Arusha endapo halmashauri ya jiji ikithubutu kutekeleza mradi huo.

Lema,alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari hivi karibuni akipinga kwa nguvu zote utekelezaji wa mradi huo hususani kitendo cha kuwahamisha baadhi ya wakazi wa eneo la Kaloleni watakaolazimika kuupisha mradi huo mara utakapo anza .

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake meya wa jiji hilo,Gaudence Lyimo alimtaka mbunge kuachana na tabia ya kupinga kila jambo la maendeleo katika jiji la Arusha kupitia mitaani na kumtaka ayawasilishe malalamiko yake kwenye vikao husika

“Ni vyema tumeona tumshauri mwenzetu kwanza ashiriki kwenye vikao vya baraza la madiwani ili ajue kinachoendelea,lakini siyo kukurupuka kwenye vijiwe kueneza siasa badala ya maendeleo”alisema Lyimo

Hatahivyo,meya huyo alisema kuwa ni vyema wakashirikiana kwa pamoja ili kurekebisha jiji la Arusha kwani mambo mengi hufanyika katika jiji hilo na nivyema likawekwa katika jiji la kisasa ili kuendana na hadhi ya jiji kama yalivyo majiji mengine mashuhuri

Hatahivyo,alifafanua ya kwamba lengo la utekelezaji wa mradi huo ni kupunguza kero katika jiji la Arusha,kukuza ajira,uchumi , kuondoa makazi holela sanjari na kuufanya mji wa Arusha kuwa wa kuvutia zaidi huku ajira zikiwa lukuki kwa vijana ambao hadi leo hawana ajira.

"Elimu kwa Wananchi ni muhimu ili kuweza kuwaelimisha kuhusu miradi mbalimbali ambayo inaendelea kwani sisi kama Halmashauri hatuwezi kufanya lolote bila kuwashirikisha wananchi kwani na wao wanamchango mkubwa sana"alisisitiza Lyimo

Alifafanua kuwa uongozi wa halmashauri hiyo bado haujaingia mkataba na mwekezaji yoyote katika mradi huo na kinachofanyika kwa sasa ni hatua ya awali ya kuusoma mradi huo ambapo mwisho wake watakwenda kuzungumza na wakazi wa eneo husika kujua nini cha kufanya.

“Hatujampa mwarabu,hatujaingia mkataba wowote bado tuko katika hatua za awali kabisa za kuusoma mradi wenyewe kama una manufaa au la na mwisho wa siku ni lazima twende tukazungumze na wakazi wa Kaloleni na mwisho wa siku hakuna atakayehamishwa kinyemela bila kujua anakwenda wapi kama atalazimika kuondoka’alisisitiza Lyimo.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Sokon I,Michael Kivuyo(TLP) pamoja na diwani wa kata ya Baraa,Loota Laiser (CCM) walimtuhumu, Lema kwamba amekuwa akipinga kila jambo la maendeleo katika maeneo ambayo hayastahili kulalamika.

Walidai ya kwamba wakazi wa Arusha hawahitaji siasa za vijiweni na badala yake walimshauri mbunge huyo kujenga desturi ya kuhudhuria vikao husika na kisha kuwasilisha malalamiko na kero mbalimbali zinazomkera.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Mh Meya pamoja na madiwani wa Arusha nawapongeza kwa hatua mnazoendelea kuchukua kwa ajili ya kuleta maendeleo ya jiji la Arusha. Nashukuru pia kwa kumshauri mbunge Lema kuacha siasa za ushabiki za kupotosha umma wa wapenda maendeleo,kwani yeye kama mbunge kinamshinda nini kuhudhuria vikao kwa ajili ya maendeleo ya wananchi !!!! akumbuke tu kwamba uwakilishi si kushabikia au kuchochea unaowawakilisha bali ni kufanya kila jitihada kushiriki ktk kuwaletea hoja za maendeleo...mambo ya kimtaani ayaache sasa...hajajitambua bado !!!!!!

    ReplyDelete
  2. ATASHIRIKI SAA NGAPI VIKAO VYA MAENDELEO WAKATI MAANDAMANO YANAMUHITAJI? AU HAMJUI KUWA MAENDELEO HUPATIKANA KWA MAANDAMANO NA POROJO?

    ReplyDelete
  3. Cha muhimu hukuchaguliwa kihalali kubali hilo na cha muhimu uchaguzi urudiwe ili kieleweke!

    Unafikiri Lema ni kichaa? anasema ukweli na siku zote ukweli ni SUMU kwa asiyeutaka au kwa mtu mbinafsi!

    ReplyDelete
  4. He we meya unadhani tumesahau hukuchaguliwa kihalali? huo mzimu utakufuata kila utakapotokezea.

    ReplyDelete
  5. lema ni chizi akilizake anazijua mwenyewe bangi la utotoni mpaka ukubwani unafikiri utakuwa mzima? anaubishi wa kimtaani si wakisomi wenzake kina lisu hawaoni?

    ReplyDelete
  6. Mkibosho, huyu Lema kama mbunge anaelekea hajui kinachoendelea, na anachukulia habari kisiasa ambayo ni hatari sana, kuna namna nyingi za kupisha maendeleo, kariakoo mbona kila siku watu wanapisha maendeleo kwa hiari zao????? Hii ni kuchochea maandamano na kuwachota watu kisiasa.

    Lema sio kichaa ila mbinu zake za kizamani, wananchi wakaloleni acheni kumsikiliza ongeeni moja kwa moja na manispaa mjue kinachoendelea. Pengine kitakuwa cha manufaa makubwa kwenu kuliko hizo siasa za bei rahisi zitakazowatumbukiza kwenye shimo badala ya kufaidika, mwisho wa siku anayefaidika ni yeye na nyie mnaendelea kuishi maisha duni.

    ReplyDelete
  7. Kumbe ni wewe!

    ReplyDelete
  8. huyo lema ndio hakuchaguliwa kihalali ameiba kura ndio maana hana pakusemea zaidi ya kwa wahuni wenzie.

    ReplyDelete
  9. Sio jambo la busara kabisa,kwa yeye kama kiongozi kupayuka payuka na kupiga debe mitaani.la msingi kama anahoja,ni lazima aipeleke hoja katika vikao na wenye kuhusika,ili tatizo liweze kutatuliwa kitaalam,na pande zote,ziwe zimeshirikiswa na maana ya kwamba kamati ya halmashauri ya jiji na wananchi.

    ReplyDelete
  10. Sio jambo la busara kabisa,kwa yeye kama kiongozi kupayuka payuka na kupiga debe mitaani.la msingi kama anahoja,ni lazima aipeleke hoja katika vikao na wenye kuhusika,ili tatizo liweze kutatuliwa kitaalam,na pande zote,ziwe zimeshirikiswa na maana ya kwamba kamati ya halmashauri ya jiji na wananchi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...