Gari la Naibu Waziri wa viwanda, biashara na masoko,Mhe. Lazaro Nyalandu likiwa limekwama katika eneo la kijiji cha Migugu Kata ya Makuro Tarafa ya Mtinko Singida vijijini wakati Naibu Waziri akienda kukagua mradi wa maji katika shule ya Migugu.
Naibu Waziri wa Viwanda na masoko,Mh. Lazaro Nyalandu akizungumza na wananachi katika eneo la mradi wa maji katika kijiji cha Migugu jana.
Naibu Waziri Nyalandu akizungumza kwa msisitizo kwenye mkutano wa hadhara.
Naibu Waziri wa viwanda, Biashara na masoko,Mh. Lazaro Nyalandu (wa pili kulia) akiongozana na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Singida,Illuminata Mwenda (kulia) wakielekea kwenye mradi wa maji katika shule ya msingi Migugu.
Wananchi wa kijiji cha Kijota wakimpa zawadi ya Mbuzi Mbunge wao Lazaro Nyalandu mara baada ya kuhutubia wananchi hao.
Wananchi na Wanafunzi Wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini,Mh. Lazaro Nyalandu.
WATOTO HAO WAMEVAA SWETA ZA BENDERA YA TAIFA NIMEWAPENDAJE JAMANI!WAMEONEKANA KWA MBALI MASIKINI,,,AHLAM UK
ReplyDeleteMheshimiwa, hebu hamasisha utengenezaji wa hizo barabara kwanza. Hiyo itakuwa hatua moja kubwa sana.
ReplyDeleteLeo VX lako linaharibika bure kwenye hizo barabara.
Hao wazee wenye vibaragashia na vitambaa vichwani 'huwambii kitu' kuhusu CCM hao ndio mara nyingi wanaleta "ushindi wa kishindo" kwa CCM.Usipime
ReplyDeleteDavid V
Kama ameenda kutembelea Jimbo lake kwa nn anatumia Gari ya ofisi kwa shughuli zake za kijombo ili hali wanapewa magari yao binafsi na viwezesho vyote (Posho za mafuta, kukaa jimboni) haya ndio tunayaita matumizi mabovu ya mali ya uma hata kama ameenda kwa nia njema.
ReplyDeletei wish wabunge wangekuwa nao wanakaa huko huko kwenye majimbo yao kuwa karibu na wananchi wao.kwenda dar or dodoma bungeni kikazi.
ReplyDeletekwani mipaka ya matumizi ya haya magari ni wapi mpaka wapi?
ReplyDeletei dont think this is right. Anatumiaje gari la Serikali kwenda kutembelea wapiga kura wake? Really this is Tanzania. Hivi hatuna sheria inayoweka mipaka ya matumizi ya magari ya serikali. No wonder why magari ya Serikali yanatumika kupelekea watoto wa wakubwa shule.
ReplyDeleteHuu ni UBADHIRIFU wa mali ya umma, yaani shughuli zake za kibunge anatumia gari la Wizara? na huyo dereva nae posho analipwa na nani? Jamani kuweni waungwana maana hapo mpaka PA wa Wizara nae atakua kafuatana nae. Tusifanye mazoea katika hili maana hata Maalim Sefu nae anakuja huku kwa shughuli za kichama anatumia usafiri wa Serikali. Uwe Rais, Waziri Mkuu au yeyeyote yule, shughuli zisizohusiana na Serikali ni kivyako sio mnatuongezea matumizi yasio lazima. Na hizo V8 mayai nunueni Landcruiser 2 acheni kuleta ubishoo.
ReplyDeleteHuyu dereva kilaza kweli gari kama hiyo inakwama kwenye vijitope manake sio tope hilo. nazani bado hajalijulia fresh....
ReplyDeletejamani huyu Mh hajui kuvaa kulingana na sehemu mumusaidie jamani
ReplyDeleteHuyo dereva wa Waziri kazoea barabara za mjini, ndo sababu anakwamisha VX V8 4WD mahali hapo. Hilo gari si la kukwama katika barabara nzuri kama hiyo. Ni mtazamo tu
ReplyDeleteWaheshimiwa kama hawa acha wakwame labda ndiyo watajua matatizo wanayoyapata wapiga kura wao huko vijijini!!
ReplyDeleteLearn through practical Experience!
ReplyDelete''Kujifunza kupitia vitendo/matukio halisia''
Gari la Mhe. XV V8 kukwama ni tukio zuri sana ili iwe ni uamsho wa kuzingatia ahadi za kuboresha Mioundo mbinu na barabara zinazotoka wakati wa kuomba kura na matekelezo yake baada ya Uchaguzi!
Mbio zimeanza eenhe?
ReplyDeleteItatia kinyaa na inasikitisha sana!
ReplyDeletehivi naibu waziri naye anakuwaga na mpambe(kama wa rais) wakati akiongea/kuhutubia ?
ReplyDeleteIweje shughuli za kichama (kutembelea jimbo la uchaguzi) azifanye kwa kutumia mali ya walipa kodi ilhali alishakopeshwa gari na anapewa mafuta na pesa ya dereva? That is embezzlement of public properties.
ReplyDeletehuyu jamaa attention seeker sana! Naibu waziri lakini kila kitu lazima anataka watu wamnote!
ReplyDeleteHUYU JAMAA HUKO BUNGENI ANAFANYA NINI?? KWAO HAKUNA HATA BARABARA AIBU SANA, SASA ANGALIENI JAMANI HAWA VIONGOZI HAWADHAMINI WATU WALIOWAWEKA MADARAKANI, ANASAHAU HATA KUWAPATIA BASICS.
ReplyDeleteukweli wa matumizi mabaya ya vyombe vya serikali yapo wapi na hili ni moja wapo kiongozi kijana na mchapa kazi anathubutu kutumia gari la wizara kwa shughuli zake binafsi hapa tunajiuliza je hili gari kufanyiwa service ni kiasi gani na nani anaingia gharama hii yeye mwenyewe au wizara? kwa gharama hizi tu wasifu wa kuwa kiongozi bora unapotea.
ReplyDeleteWanatunia VX kwenye matope lakini wajawazito watawapa bajaji weruu dani siasa bora uongozi bora saafi sana si unaona watu wanavyowashangilia hayo ndio matumizi mazuri ya madaraka
ReplyDeleteHao wazee wenye vibaragashia na vitambaa vichwani ndio walioleta uhuru wa nchi hii. Ndio hao waliomlea Nyerere na ndo waliomfundisha siasa Nyerere ndo waliomfundisha Nyerere Kuvaa suruali Ndo waliomlea Nyerere pale mjini Dar es Salaam (Mzizima).
ReplyDeleteAbdallah Y
Mawazo yenu wabongo yakoje? Angalieni mantiki siyo gari.
ReplyDeleteCan you decipher sense from nonsense?
Hii XV V8 ilistahili Muheshimiwa aiache Zahanati Jimboni ili kubebea Wajawazito majumbani kwenda kujifungua, angeokoa hela ya mafuta ikanunulia chakula kwa Watoto wenye Utapiamlo Jimboni,,,halafu yeye katika ziara yake atumie Bajaj au Toyo ya Kichina ya matairi matatu kwa safari yake hiyo maana ingekuwa ni rahisi hata kwa kuibeba badala ya kuisukuma kwenye tope kama ingekwama!
ReplyDeletejamani hamsifii shule iko katika mandhari mazuri, miti na upepo baridi safi kwa kujisomea , sauti za ndege kwa mbali, pia angalieni sura na miili ya hao wanafunzi walivyo fresh-hakuna anayeonekana over weight au obessy-spelling wadau, wengi wenu mlichokiona hapa ni gari, na huyo jamaa mwenye mkoti na viatu vya ngozi vilivyopigwa kiwi kama cha polisi, eti amekwenda kutembelea mradi wa maji kijijini-badala ya kuvaa jeans na raba (running shoes), lakini kwa vile wananchi hasa wabongo, wametanguliza wema badala ya makuu, na wameacha shughuli zao kuja kumsikiliza
ReplyDeleteHilo gari siyo XV hilo linaitwa VX wapi shule ndo maana mna dwell kwenye shallow issues badala ya kuangalia maji kwa ajili ya wapigakura. Vema sana Mbunge na wananchi wa Migugu, pamoja tunaweza.
ReplyDeleteWabongo kwa longolongo tu, mmh kiboko. Asipoenda jimboni kwake maneno, akienda pia maneno, sasa afanyeje? Ni mtazamo tu!
ReplyDeleteInaoenekana vijana hamjui historia ya nchi yenu vizuri. April 13, Nyerere angefikisha miaka 90. Hakuna mwenye kibarakashea hapo ambaye angeweza kumlea!
ReplyDeleteWewe Anonymous wa Thu Jan19 11:14:00AM 2012
ReplyDeleteCan you decipher sense from nonsense!
Hapa tunatahtimini Tija na Faida hivyo hatuwezi kuvutiwa na ''Contents'' zinazohusu ziara yake huko Jimboni kwake bali tuna chambua kilichomo na kitu kama XV V8 gari aliyotumia ni LAZIMA IJADILIWE!
Hiyo zawadi ya Mheshimiwa ni Mbuzi au Mbwa haieleweki hapo,kanaonekana kama ka-mbwa!
ReplyDeleteVX
ReplyDeleteWandugu Mhe. kwa sasa anazo kofia mbili (2) yaani Mbunge na pia Naobu Waziri.
ReplyDeleteSasa kwenda na gari la kazi ya Serikali katika eneo lake la Ubunge inaweza tokea kwa vile mfano wewe umepewa na Bosi wako Baiskeli ya kazi ya kubebea Mchicha, ukipata taarifa za Mgonjwa au Msiba uiegeshe Baiskeli ili uende kumuona Mgonjwa au Msibani kwa mguu?
Hapo itakuwa imekaa sawa kweli?