Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, sasa amemgeukia Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, na kumtaka aache mara moja kuingilia maamuzi yaliyofanywa na chama hicho.

Badala yake amemtaka afuate sheria na kanuni ya uendeshaji wa Taasisi yake na kwamba hadi anazungumza hajapokea amri yoyote ya mahakama.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha Manzese Bakhresa jijini Dar es Salaam leo, Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, alisema anashangazwa kuona Tendwa mwenye jukumu la kulinda Katiba za vyama vyote anakuwa mtetezi mkuu wa Mbunge wa Jimbo la Wawi, Hamad Rashid Mohamed, ambaye amefukuzwa uanachama kwa kufuata sheria na taratibu zote. 
Mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya wanachama wa chama hicho, ulikuwa maalum kutoa ufafanuzi wa hatua iliyochukuliwa na Baraza Kuu la Uongozi wa chama hicho wa kuwafukuza uanachama watu wanne akiwemo Hamad.

Alisema kwa ujumla anamheshimu sana Tendwa kutokana na majukumu yake ya kitaifa lakini kwa hatua yake anayoichukua ya kumtetea Hamad ni jambo linalomshangaza, "Baada ya kuchukuliwa maamuzi yale, Msajili wa vyama vya siasa leo amejitokeza hadharani kumtetea Hamad, jambo hili linanishangaza sana, nilitegemea yeye angetuunga mkono kutokana na kutumia Katiba yetu vizuri," alisema.

Alhamisi iliyopita Tendwa, alisema tabia ya kufukuzana uanachama kwenye vyama vya siasa sio mzuri na unalisababishia hasara taifa na wananchi wanakosa haki yao ya msingi ya kuwakilishwa bungeni.

Maalim Seif alisema nia ya Msajili kutetea jambo hilo ni kuona chama hicho kinaendeshwa kihuni bila kufuata taratibu kitu ambacho kamwe hakitafanyika, "Kweli Msajili anatetea kwa maana gani hasa, anataka kuona CUF ikiendeshwa kihuni? Kamwe haitawezekana kwani chama hiki hapendwi mtu," alisema huku akionekana kuchukizwa na jambo hilo. 
Aidha amemtaka Msajili huyo pamoja na watu wengine waliojitokeza kusimama mstari wa mbele kupinga maamuzi hayo waache mara moja kwa sababu chama hicho sio mali ya mtu bali ni taasisi inayomilikiwa na Watanzania.

Akizungumzia mazingira ya kufukuzwa Hamad na wenzake watatu, Seif alisema kabla ya kuchukua maamuzi hayo kwanza walijaribu kuitisha vikao viwili vya kumuonya kuhusu mwenendo wake mbaya, lakini hakuonyesha kubadilisha mwenendo wake.

Alisema kikao kimoja kilifanyika Zanzibar na kikao cha pili kilifanyika jijini Dar es Salaam na kuwashirikisha watu mashuhuri.

Alieleza kwa ujumla baada ya hali hiyo kushindikana waliamua kufuata taratibu za chama hicho ikiwemo kuwaita watu wote wanaotuhumiwa kukihujumu chama kwa ajili ya kujitetea na walifanya hivyo.

Alisema Baraza Kuu la uongozi wa chama hicho lilichukua maamuzi hayo kwa kuangalia haki ya mwanachama na sio ubunge wa mtu, kwani ndani ya chama hicho mtu yeyote hata akiwa kiongozi akionekana kwenda kinyume na taratibu anachukuliwa hatua.

Pamoja na hayo alisema CUF imefuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kumtaarifu Spika wa Bunge juu ya uamuzi huo na kama haikutekelezwa hayo chama chake hakitahusika, "Hakuna atakayeweza kurudisha nyuma jambo hili, tumemwambia Spika kuwa huyu Hamad sio mwanachama wetu, akitaka kumlea hilo lake," aliongeza kusema.
Akizungumzia tishio la mahakama, Maalim Seif alisema kamwe hatishiki na jambo hilo kupelekwa mahakamani kwa sababu anatambua kila kitu kiliendeshwa kisheria na hakuna kitu kilichokiukwa.

Alisema watu kuwafukuza ndani ya chama hicho sio mara ya kwanza na wote walikimbilia mahakamni lakini baadae ukweli ulibaki palepale. Hata Mahakama ikimrudishia Hamad ubunge wake, watamtambua na ataendelea kuwa Mbunge wa mahakama.

Alisema amegundua kuna ajenda za siri zinazofanywa na baadhi ya watu waliochukizwa na muafaka wa Zanzibar ambapo sasa wanafanya kila juhudi kuwarudisha nyuma Wazanzibari walioanza kupata faida ya amani.

Alisema CUF itazidi kusimama imara kupinga njama zozote zitakazosababisha visiwa vya Zanzibar kukosa amani na kurudi katika hali ya siasa za huko nyuma.

Awali Naibu Katibu Mkuu wa chama hichoTanzania Bara, Julius Mtatiro, alisema zoezi la kuwasafisha viongozi wanaoaminika ni waasi litaendelea katika ngazi zote kuanzia Wilaya, Kata hadi Matawi ya chama hicho.

Alisema kuanzia sasa wanachama wote wawe makini kuwatambua watu wa aina hiyo na baadae wafanye utaratibu wa kuwafukuza kulingana na katiba na kanuni ya chama hicho. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. well done,baadhi ya watu wanajaribu bahati yao na Maalim,dont push your luck with this guy,cha kushangaza huyu Hamadi aliefukuzwa alishika nyadhifa nyeti serikalini inaonesha anatakiwa nini na chama tawala?
    lakini ataishia kama kina mapalala sijui hata wako wapi pumbafffffffffff

    ReplyDelete
  2. Hamadi Rashid kaonewa sana na CUF.namshangaa huyu Mtatiro. kweli yeye anaijua CUF kuliko Hamadi Rashid?

    Demokrasia ina safari ndefu sana kwetu.Maalim Seif unataka umakamu wa Rais hapo hapo hutaki kuachia ukatibu mkuu wa CUF. hapo hapo unataka kuwa mhasibu mkuu wa Chama.
    lakini wapemba kwa Hamad Seif utafikiri wamepewa limbwata.
    Hamad uko nasi.

    ReplyDelete
  3. huyu mtatiro ajiandae nae kufukuzwa. hwenda zamu itakayokuja ikawa yake.....leo mwema kesho watamgeuzia kibao.....

    ReplyDelete
  4. Uchaguzi wa TZ wapiga kura wanachagua chama sio mtu. Hata akijiunga na chama chengine hatochaguliwa maana waliomchagua walichagua chama sio yeye. Kilichobakia Hamad Rashid akamuangukia Maalim Seif ili amrudishie uanachama. Kwa tamaduni za Zanzibar Hamad Rashid akatafute mashua aaze uvuvi.

    ReplyDelete
  5. TENDWA LAZIMA AMTETEE HAMAD RASHID KAMA ALIVYOMTETEA KAFULILA KWASABABU 2.

    MOJA,WAO CCM HAWANA UTAMADUNI WA KUWAJIBISHANA HATA MTU AKIENDA KINYUME CHA KATIBA/MAADILI.

    MBILI,KAMA HAMAD AU KAFULILA WANGETOKA MAJIMBO AMBAYO CCM WANAWEZA KUSHINDA,TENDWA ANGEITISHA UCHAGUZI MDOGO HARAKA,LAKINI KWASABABU CCM HAWAWEZI KUSHINDA WAWI WALA KIGOMA,BASI ANAPATA TABU SANA KUKUBALI.

    ReplyDelete
  6. duuuu,hatari sana,cuf bwana,wamemvua gamba hamadiiiiii,kweli hawa kiboko

    ReplyDelete
  7. Welldone CUF. Kungekuwepo jasiri wa namana ya Seif huko Magambani, tungekuwa tumepiga hatua kuubwa!

    ReplyDelete
  8. Kilichobaki baada ya Hamad Rashid Mohamed katika CHAMA CHA WAPEMBA(sio CUF) ni majungu, maslahi binafsi na unafiki!

    ReplyDelete
  9. Na huyo aliyebebwa na Mtatiro ni mwanachama mpya au!

    ReplyDelete
  10. malim thumb up amenifurahisha chama hakiendeshwi kihuni<<hi hi ihi very interesting,hamadi na shoka watabakia magazetini tu,they have done very big mistake,hiki kiumbe si cha kuchezea,aliona muasisi atamuweza malim,wapii? na huyomsajili imehusu nini kuingilia? au ni mweka hazina wa serikali yeye akomeee chama si wahuni pale kuna wasomi watupuuuu,kama walivosema washakufa basi washakufa kweli

    ReplyDelete
  11. Hamad Rashid amekwisha kisiasa sasa lilobaki uendeleze tu hizo biashara zako za kuuza madafu wacha watu waendelee mbele kujenga nchi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...