Hello bro Michuzi,
Pole na sshughuli ndugu yangu. Tafadhali wakee wanajamii na wadau wengine kwa ujumla picha hii ya timu ya Mt. Meru Warriors ya mwaka 1987, ambayo nadhani ndio inayofaa kuitwa "the Arusha Dream Team". Naanza kwa kumkumbuka Hamisi Gagarino (wa pili kulia nyuma). Wengine msaada tutani.
 
Wasalam,
Madau wako mkubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. pembeni ya Gagarinho yuko Team Coach Ally Mtumwa,Halafu namuona Victor John Bambo (kushoto kwa Gaga).Mbele kutoka kulia ni Charles Mngodo akifuatiwa na Christopher Gaga(mdogo wa Gagarinho).wengine wamenitoka kidogo lakini enzi hizo kikosi cha Mt.Meru Warrios kilikuwa na watu kama Juma Mkulila,Mohamed Mateneke,Mwanga Luheya,Mohamed Bob Chopa,Mahmoud Omary, Simon Kishoka,Mohamed Mwameja,Ali Pande, Lilla Shomari na wengine.ilikuwa raha tupu miaka hiyo katika mji wa Arusha

    ReplyDelete
  2. aisee ni moja ya kumbukumbu ya muhimu sana katika historia ya soka!!

    ReplyDelete
  3. mdau ungelisema gaga ni wapili kutoka kushoto na si wa pili kulia.lakini nakupa big up sana kwa hii picha watanzania tutamkumbuka sana hamisi gaga katika uelimwengu wa soka huyu jamaa namfananisha na zico wa brazil.

    ReplyDelete
  4. MNAONA WADAU WACHEZAJI ENZI HIZO WA LIKUWA HANDSOMS BOYS WANAMVUTO SIO SIKU HIZI WACHEZAJI HATA MAJINA YAO SIO MAZURI,SIJUI WAMETOKEA ISITU YA KONGO HUKO KWA KINA BANYAMULENGE, WAFUPI HATA HAWAONEKANI VIZURI KWENYE LUNINGA KAMA HAO KINA MWANAFULANI WA YANGA SIJUI KABILA GANI HUYO BEKI WA KULIA MBAYA KA MAVI YA MNYAKYUSA.

    MDAU VINGUNGUTI DAR

    ReplyDelete
  5. Ali Mtumwa wa kwanza kushoto nyuma

    ReplyDelete
  6. Inachekesha kuwa vijana wa siku hizi ni mambilikimo, unamaanisha Ngassa nini? Yaani mtu miaka 23 anawika mwaka ama miwili then mpira unakwisha, jamani....mtu mpira unapanda chati anapokuwa 27 - 30 yrs old ila bongo ndo kipaji kinakwisha, si dalili za kichawi hizi? Mpira si uchawi ni kipaji ila Bongo hatujuwi hili bado.

    ReplyDelete
  7. Huyo beki wa Yanga amekuwa mbaya kiasi hicho kwa sababu anawabania sio? Angekuwa mteremko mngemuita bonge la handsome. Fani ni tofauti na mtu, muheshimu mtu kama mtu usimchanganye na fani yake.

    Kumbuka, sisi tumeumbwa kwa mfamno wa Mungu.

    ReplyDelete
  8. Hapo hakuna heleni wala kusuka nywele wala kujichubua hapo ni boli linasakatwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...