Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda za Mashariki wa Bohari ya Dawa (MSD), Lucy Nderimo (kushoto) akimkabidhi Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah hundi yenye thamani ya sh. mil. 10 ikiwa ni msaada kwa timu ya Taifa ya Soka ya Wanawake ya Twiga Stars, katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia makabidhiano hayo ni Meneja wa Huduma kwa Wateja na Uhusiano wa MSD, Salome Mallamia. Timu hiyo inapambana na Namibia kesho katika mechi ya marudiano ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake.
Katibu Mkuu TFF, Angetile Osiah (kushoto) akitoa shukurani kwa MSD kuipatia timu hiyo msaada. Kulia ni Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda za Mashariki wa Bohari ya Dawa (MSD), Lucy Nderimo.
Meneja wa Huduma kwa Wateja na Uhusiano wa MSD, Salome Mallamia (kushoto), akielezea umuhimu wa msaada huo kwa timu hiyo ya soka kwa wanawake. Kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...