JUMUIYA YA WATANZANIA ITALIA INASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MTANZANIA NDUGU  TWAHIR HUSSEIN OMARI  (PICHANI) KILICHOTEKEA JANA USIKU MJINI NAPOLI.

SABABU YA KIFO CHAKE ITAPATIKANA BAADAE BAADA YA UCHUNGUZI WA MADAKTARI.

MIPANGO YA MAZISHI TAYARI INAFANYWA  JUMUIYA INAWATAKA WATANZANIA KUJITOKEZA  KWA WINGI NA KUJITOLEA ZAIDI KATIKA MICHANGO ILI TUWEZE KUUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU NYUMBANI.

MAREHEMU NI MWENYEJI WA TANGA   BARABARA  15.NA HAPA ITALY ALIKUWA AKIISHI MJINI MODENA.

MATAWI YOTE YA JUMUIYA YA WATANZANIA ITALIA NA JUMUIYA ZOTE ZINAOMBWA KUKUTANA MARA MOJA ILI KUKUSANYA MICHANGO. KWA MAWASILIANO  WASILIANA NA  KATIBU N° +39 329 4149 712

 TUNAUNGANA NA  WATANZANIA WOTE WANAOMFAHAMU , NDUGU  NA WAZAZI KATIKA  WAKATI HUU MGUMU WA MAOMBOLEZO.  MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA! AMIN!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. poleni sana

    ReplyDelete
  2. poleni sana ndugu na marafiki,ni uchungu mkubwa sana mimi nilikua Italy Christmas iliyopita he was ok.
    very sad, very sad such a churming Guy
    mungu ailaze roho yake peponi. AMEN

    ReplyDelete
  3. Mungu ailaze roho yake peponi.Amen
    ni pengo kubwa kwa jamaa na marafiki poleni sana.
    MC pales

    ReplyDelete
  4. INNALILAHI WAINAILAYHI RAJIUNNN... POLENI WAFIWA, HII NI SAFARI YA KILA MTU, TUNAMUOMBA ALLAH AMUEPUSHIE ADHABU YA KABURI NA AMPE KITABU CHAKE KWA MKONO WA KULIA INSHALLAH

    ReplyDelete
  5. kaka mboga Zote, tutakukumbuka daima.
    marehemu alikua mpenzi sana wa Khadija Kopa na hata Kopa alipokuja marehemu alikuwa beneti sana.
    dah ni noma,

    ReplyDelete
  6. dah mboga kaka umetutoka!mungu akuweke mahala pema pepon aamin! na wewe kaka miaka 30 hujatia timu nyumbni tz duh!hiyo kali sasa jamaa watakujua kweli!jamani tuwe tunawakumbuka ndugu nyumbanihata kama tupo majuu kimaisha

    ReplyDelete
  7. Jamani tunapotoa maoni tuwe waangalifu na kile tunacho comment, kwani dini inatuamrisha tuwazungumzie Marehumu mema yao na sio maovu yao, na tuache kusimanga maiti. Ndugu yetu "Mboga Zote" (Kaka Twahiri) ni mwingi wa vichekesho na mkarimu. Mwenyezi mungu akumjaalia kurudi nyumbani maana marejeo ni majaaliwa sio kumsimanga. "Inna Lillah Wa-inna-Illaih Rajiuun" Mdau Mbegu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...